Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo mkoa wa Kilimanjaro, Askofu Mjema Robinson,akizungumza wakati wa kikao kazi cha kupitia mwongozo wa Malezi Bora, Taifa Imara, kinachofanyika mkoani Tanga kwa siku nne kuanzia Julai 31, hadi Agosti 03, 2023.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amoni Mpanju,akizungumza na Viongozi wa Dini wakati wa kikao kazi cha kupitia mwongozo wa Malezi Bora, Taifa Imara, kinachofanyika mkoani Tanga kwa siku nne kuanzia Julai 31, hadi Agosti 03, 2023.
Mkurugenzi wa Idara ya watoto, kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Sebastian Kitiku,akizungumza wakati wa kikao kazi cha kupitia mwongozo wa Malezi Bora, Taifa Imara, kinachofanyika mkoani Tanga kwa siku nne kuanzia Julai 31, hadi Agosti 03, 2023.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amoni Mpanju,akisalimiana na Viongozi wa Dini wakati wa kikao kazi cha kupitia mwongozo wa Malezi Bora, Taifa Imara, kinachofanyika mkoani Tanga kwa siku nne kuanzia Julai 31, hadi Agosti 03, 2023.
Sehemu ya Viongozi wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amoni Mpanju,(hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha kupitia mwongozo wa Malezi Bora, Taifa Imara, kinachofanyika mkoani Tanga kwa siku nne kuanzia Julai 31, hadi Agosti 03, 2023.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amoni Mpanju,akiwa katika picha na Viongozi wa Dini wakati wa kikao kazi cha kupitia mwongozo wa Malezi Bora, Taifa Imara, kinachofanyika mkoani Tanga kwa siku nne kuanzia Julai 31, hadi Agosti 03, 2023.
Na MJJWM, Tanga
Viongozi wa dini kutoka mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara wameipongeza Serikali kwa hatua ya kuandaa mwongozo wa malezi bora utakaojumuisha watu wa kada mbalimbali ndani ya jamii.
Viongozi hao wametoa pongezi hizo, wakati wa kikao kazi cha kupitia mwongozo wa Malezi Bora, Taifa Imara, kinachofanyika mkoani Tanga kwa siku nne kuanzia Julai 31, hadi Agosti 03, 2023.
Akiongea wakati wa kikao hicho, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo mkoa wa Kilimanjaro, Askofu Mjema Robinson, amesema, wamefurahi kuona Serikali ipo bega kwa bega na viongozi wa dini kushughulika na masuala ya maadili.
“Mhe Mgeni Rasmi, kama kuna kitu viongozi wa dini tunafurahi kuona kinatokea wakati huu wa sasa ni hatua ya Serikali kuja na Mwongozo huu wa malezi Bora, lakini mbali ya uwepo wa Mwongozo ni hii hatua ya kutushirikisha viongozi wa dini, ni ukweli kwamba mmetambua nafasi yetu, hivyo kwa niaba ya viongozi wenzangu tunawaahidi ushirikano wetu” amesema Baba Askofu Robinson
Akifungua kikao kazi hicho Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amoni Mpanju amesema kundi la viongozi wa dini ni muhimu sana katika suala zima la malezi na makuzi.
“Ninyi Viongozi wa dini, mnaangalia roho lakini pia mnaangalia mahitaji ya mwili, hivyo nafasi yenu ni kubwa sana, wajibu wetu kama Serikali nikuandaa miongozo lakini miongozo hii itakuwa na maana endapo ninyi ambao mnatutunza kiroho mtatusaidia kufikisha jumbe kwa wanajamii” amesema Mpanju.
Mpanju vilevile amewaomba viongozi wa dini, kubadili mbinu na mikakati ya kuwatayarisha wanandoa, kwani taasisi ya ndoa ndio msingi wa kuwa na familia bora.
“Viongozi wa dini, siku hizi watu wanatafuta walezi wa ndoa kwa kuangalia sura, badala ya kuangalia nani ana maadili ambaye atakuwa mshauri wa ndoa, vema viongozi wa dini tunapokwenda kuutekeleza mwongozo huu, tuwafundishe waumini wetu namna bora ya kuimarisha taasisi ya ndoa” amefafanua Mpanju.
Aidha, Mpanju amekemea vikali baadhi ya watu wazima wenye mahusiano na watoto wadogo na kusema hiyo ni kwenda kinyume na maadili ya kitanzania.
Akitoa maelezo ya awali Mkurugenzi wa Idara ya watoto, kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Sebastian Kitiku alisema shabaha ya kuandaa mwongozo huo wa Malezi Bora ni tafiti iliyofanywa na Serikali kwa kushirikiana na UNICEF, ambapo nguzo kuu tatu zitazingalitiwa kwenye mwongozo huo za Kujali, Kulinda na Kuwasiliana na mtoto
Social Plugin