Mkurugenzi Msaidizi wa Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Robert Masingiri akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwa washiriki wa mafunzo ya wiki moja ya kukuza ujuzi kwa wafanyakazi wa hotelini 700 wa mkoani Arusha.
Wafanyakazi wa hotelini mkoani Arusha wakipata elimu ya namna ya kutoa huduma kwa mteja kutoka kwa Mwezeshaji Leopold Kabendera kwenye mafunzo ya kukuza ujuzi kwa wafanyakazi hao yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi yanayofanyika jijini Arusha kwa wiki moja.
Mshiriki wa mafunzo ya kukuza ujuzi kwa wafanyakazi wa hotelini mkoani Arusha yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi, Ruben Masaga akionesha utaalamu wake wa kubeba sahani tano kwa mara moja anapomhudumia mteja kwenye mafunzo hayo yanayofanyika kwa wiki moja jijini Arusha.
Mwezeshaji wa masuala ya huduma na chakula hotelini Richard Makori(aliyebeba sahani) akimsikiliza mmoja wa washiriki wa mafunzo ya kukuza ujuzi kwa wafanyakazi wa hotelini mkoani Arusha (kulia) namna alivyoelewa somo la kumhudumia mteja, mafunzo hayo yanayofanyika kwa wiki moja.
Social Plugin