WANANCHI WAALIKWA KUSHIRIKI KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA JKT

Waziri wa Jeshi la ulinzi na Kujenga taifa Innocent Bashungwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari Maelezo Dodoma.

Na Dotto Kwilasa,Dodoma 

Waziri wa Jeshi la Ulinzi na Kujenga Taifa(JKT) Innocent Bashungwa amewalika Wananchi wa mkoa wa Dodoma na watanzania kwa ujumla  kujitokeza kwa wingi kuhudhuria siku ya kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi hilo ifikapo Julai 10,2023 Jijini Dodoma.

Bashungwa ameeleza hayo leo Julai 8,2023 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu kilele Cha Maadhimisho hayo na kueleza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele hicho.

Bashungwa pia ametumia nafasi kueleza,"Napenda kuwashukuru JKT kwa maandalizi ya Maadhimisho haya wadhamini na wote wanaoshirikiana na sisi katika maandalizi ya Julai 10 ya Miaka 60 ya JKT, " 

Na Kwa namna ya pekee nishukuru uongozi wa mkoa wa Dodoma kwa uratibu unaoendelea  katika kufanikisha Maadhimisho haya ya kihistoria," amesema Waziri Bashungwa

Amesema kilele Cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT,kimetanguliwa na shughuli Mbalimbali ikiwa ni  pamoja na JKT Marathon 2023 iliyofanyika Juni 25 .

"Julai 1,2023 Makamu wa Rais , Dkt Philip Mpango alifanya uzinduzi wa Mnara wa Kumbukumbu katika makao makuu ya JKT (Chamwino Dodoma) na Kufungua maonesho ya bidhaa  ambayo yanaendelea hadi sasa  viwanja vya Medeli East Mkabala na SUMAJKT House,

"Tumefanya pia huduma za kijamii Kama kutembelea  Hospitali ya Uhuru uliopo wilayani Chamwino pamoja na vituo vya kulelea  Watoto wenye uhitaji zimefanyika ," amesema Waziri huyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post