Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi wakibadilisha Mkataba mara baada ya kusaini Makubaliano Kati ya Wizara hiyo na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya ufadhili wa wanafunzi 1,000 wa Vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) huku Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akishuhudia hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesaini Mkataba wa Makubaliano na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya ufadhili wa wanafunzi 1,000 wa Vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ikiwa ni Mkakati wa Benki ya NBC kukuza ujuzi kwa vijana ili waweze kujiari wenyewe.
Akizungumza jijini Dodoma Kwenye hafla ya utiaji saini Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameishukuru Bodi na Menejmenti ya Benki ya NBC kwa kuja na mpango huo kwani utasaidia mkakati wa Serikali katika kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.
Prof.Mkenda amesema kuwa ufadhili huo unakwenda kutimiza azma ya Serikali ya kutoa Elimu na Mafunzo yatakayo wawezesha vijana wa kitanzania kupata ujuzi wa kujiajiri ama kuajiriwa.
“Tunaishukuru Benki ya NBC kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika jitihada za kutoa Elimu na ujuzi kwa vijana hapa nchini katika kukabiliana na tatizo la ajira hasa kwa vijana wetu wanapofika umri wa kujitegemea” amesema Prof. Mkenda.
Hata hivyo Prof.Mkenda ameihakikishia Benki ya NBC kuwa Wizara hiyo itatengeneza mfumo wa uwazi wa matumizi ya fedha hizo ili ziweze kutoa matokeo yaliyokusudiwa katika kuwajengea ujuzi vijana ili waweze kujitegemea badala ya kusubiri kuajiliwa pekee.
Aidha amesema kuwa kupitia mpango huo wataainisha maeneo yenye uhitaji zaidi au yenye fulsa nyingi za vijana kujiajiri wenyewe na maeneo hayo yatapewa kipaumbele zaidi katika mpango huo.
Ameongeza kuwa “ Makampuni yanayoanzishwa hasa katika Mkoa wa Pwani niwatake tu VETA kwa kushirikiana na Katibu Mkuu kukaa na uongozi wa Mkoa wa Pwani na kuwakutanisha makampuni yanayoanzisha viwanda ili kubaini maeneo ya ujuzi yanayohitajika Zaidi ili tuzalishe wataalamu wengi” amesema.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi amesema Benki hiyo itatoa kiasi cha shilingi Milioni 100 kwa ajili ya kufadhili vijana 1000 watakaokwenda kusomea kozi katika Vyuo Mbalimbali vya VETA hapa nchini.
“Mpango huu unaitwa NBC Wajibika Scholarship tunatambua tatizo la ajira kwa Vijana na ni kilio cha Dunia nzima kupitia ufadhili huu tutatoa ufadhili kwa vijana 1000 na huu ni mwanzo tu idadi itakuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka tunaamini hawa wakiweza kujiajiri tutakuwa tumepunguza kwa kiasi flani” amesema Sabi.
Ametaja baadhi za kozi zitakazofadhiliwa kuwa ni Ushonaji, Uselemara, Ufundi wa Magari, Ufundi Ujenzi, Upambaji na kozi nyingine tutakazobaini zina fulsa nyingi kwa vijana kujiari na kuendesha maisha yao.
Ameongeza kuwa “ Mbali na ufadhili huu Benki itawaingiza vijana hao 100 katika mpango maalumu wa Elimu ya Fedha ujulikanao kama NBC Busness Club na tutaweza kuwafungulia akaunti Maalumu zijulikanazo kama NBC Kuwa Nasi Akaunt zisizokuwa na makato yoyote ili wajiwekee akiba” amesema.
Amesema ufadhili huo utaratibiwa na Wizara ya Elimu na kutekelezwa na Vyuo vya Ufundi Stadi VETA na NBC itaendelea na dhamira yake ya kuwa mdau muhimu wa elimu na uwezeshaji wa vijana.
Amesema kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita NBC imewekeza kiasi cha shilingi milioni 350 katika kutoa ufadhili wa vijana 70 wa ngazi za elimu ya juu, na imekuwa ikishiriki katika ujenzi na ukarabati wa miondombinu ya shule mbalimbali hapa nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) CPA Anthony Kasore ameishukuru Wizara kwa kuwezesha kupatikana ufadhili huo kutoka Benki ya NBC ambao utawezesha Vyuo hivyo kutoa Mafunzo ya Ujuzi kwa vijana wengi.
CPA Kasore amesema kuwa VETA imepokea Mradi huu pamoja na maelekezo ya kuhahakisha zinatumika kwa uwazi na kwa kutoa mafunzo yenye uhitaji na kuleta matokeo chanya kwa haraka.
''Mradi huo utaleta tija na kuahidi kuwazi katika upatikanaji wa vijana wanaotakiwa ili mradi huo uweze kuleta tija iliyokusudiwa na maagizo yote yatatekelezwa kama inavyotakiwa.''amesema CPA Kasore
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akishuhudia utiaji saini Makubaliano Kati ya Wizara hiyo na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya ufadhili wa wanafunzi 1,000 wa Vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe,Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi wakisaini Mkataba huo hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi wakibadilisha Mkataba mara baada ya kusaini Makubaliano Kati ya Wizara hiyo na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya ufadhili wa wanafunzi 1,000 wa Vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) huku Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akishuhudia hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini kati ya Wizara hiyo na Benki ya Taifa ya Biashara NBC kwa ajili ya ufadhili wa wanafunzi 1,000 wa Vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi,akizungumza wakati wa utiaji saini kati ya Benki hiyo na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya ufadhili wa wanafunzi 1,000 wa Vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe,akizungumza wakati utiaji saini kati ya Wizara hiyo na Benki ya Taifa ya Biashara NBC kwa ajili ya ufadhili wa wanafunzi 1,000 wa Vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia utiaji saini kati ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia na Benki ya Taifa ya Biashara NBC kwa ajili ya ufadhili wa wanafunzi 1,000 wa Vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akijadili jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi wakati wakishuhudia saini kati ya Wizara hiyo na Benki ya Taifa ya Biashara NBC kwa ajili ya ufadhili wa wanafunzi 1,000 wa Vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) CPA Anthony Kasore,akitoa neno la shukrani mara baada ya kusainiwa Mkataba kati ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia na Benki ya Taifa ya Biashara NBC kwa ajili ya ufadhili wa wanafunzi 1,000 wa Vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi akimkabidhi jezi ya ushiriki wa Mbio za NBC Marathoni Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,zinazotarajia kufanyika Julai 23,2023 katika uwanja wa Jamhuri ya Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushuhudia utiaji saini kati ya Wizara hiyo na Benki ya Taifa ya Biashara NBC kwa ajili ya ufadhili wa wanafunzi 1,000 wa Vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Social Plugin