MBUNGE DKT. JASON RWEIKIZA ACHANGIA SH. MIL 3 UJENZI WA KITUO CHA AFYA RUHIJA KINACHOJENGWA NA BAKWATA

Na Mariam Kagenda _ Bukoba

Mbunge wa jimbo la Bukoba Vijijini Dkt Jason Rweikiza amechangia shilingi milioni tatu katika ujenzi wa kituo cha afya Ruhija kinachojengwa na Baraza Kuu la Waislam Tanzania BAKWATA.

Dkt. Rweikiza amewasilisha mchango wake mbele ya viongozi wa BAKWATA wilaya ya Bukoba Vijijini huku akiwaahidi kuwaongezea shilingi milioni saba nyingine kadri wanavyoendelea na ujenzi.

Mwaka 2021 aliwachangia shilingi milioni Moja na ahadi ya mabati ya shilingi laki tano

Sheikh wa Bakwata  wilaya ya Bukoba ,Twahili Said amemshukru Dkt Rweikiza kwa kuendelea kuwa nao bega kwa bega katika ujenzi huo huku akimuomba kuendelea kuwatafutia wahisani wengine.

Shekhe Said amefafanua kuwa kituo hicho ni cha Waislam lakini kitatoa huduma kwa watu wote hivyo wanapokea mchango wa kila mmoja atakaye wiwa.

Awali akisoma taarifa ya ujenzi Katibu wa Bakwata wilaya ya Bukoba Vijijini ndugu Hamed Baitu amebainisha kuwa mradi huo utakuwa na majengo Zaidi ya  saba lakini wameamua kuanza na jengo la wagonjwa wa nje ambalo mpaka kukamilika kwake litagharimu fedha zaidi ya  milioni 100 ambapo mpaka sasa shilingi milioni 47 zimeishatumika.

Ujenzi wa jengo hilo upo katika hatua ya umaliziaji(Finishing) na ukikamilika utasajiliwa kama zahanati ili ianze kutoa huduma Kwa Wananchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post