SERIKALI YAIPONGEZA BARRICK KWA KUFANIKISHA MIRADI MIKUBWA YA KIJAMII


Ujumbe kutoka Tume ya madini ukipatiwa maelezo ya miradi ya kijamii inayotekelezwa na mgodi wa Barrick North Mara.


Ujumbe kutoka Tume ya madini ukipatiwa maelezo ya miradi ya kijamii inayotekelezwa na mgodi wa Barrick North Mara
Ujumbe wa Maofisa wa Tume ya Madini na Barrick katika picha ya pamoja
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara, Apolinary Lyambiko akiongea wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo.
Washiriki la warsha ya Local content wakifuatilia mada mbalimbali
Washiriki la warsha ya Local content wakifuatilia mada mbalimbali
****

Tarime: Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Madini na Biashara kutoka Tume ya Madini, Andrew Mgaya, amepongeza mgodi wa Barrick North Mara, kwa kuendelea kutekeleza miradi ya kijamii na kutoa wito kwa mgodi, viongozi wa Serikali katika maeneo ya miradi na wananchi kushirikiana na kuhakikisha kila mradi unakuwa endelevu.

Bw.Mgaya, aliyasema hayo baada ya ujumbe kutoka Tume ya Madini kutembelea baadhi ya miradi ya kijamii inayofadhiliwa na mgodi wa Barrick North Mara, ukiwemo mradi mkubwa wa maji uliopo kijiji cha Nyangoto uliogharimu shilingi takriban bilioni moja kupitia fedha za uwajibikaji wa jamii (CSR) zilizotolewa na mgodi huo , ujenzi wa shule mpya ya msingi Kenyangi katika kijiji cha Matongo na mradi wa kilimo biashara wa vijana kijijini Matongo .

“Niwapongeze Barrick kwa juhudi hizi lakini suala la sustainability (uendelevu) kwa kila mradi ni muhimu,” alisema Mgaya ambaye ndiye kiongozi wa ujumbe wa maafisa kutoka Tume ya Madini waliofika mgodini kwa ajili ya kuendesha warsha ya siku 2 kuhusu ushirikishwaji wa Watanzania kwenye sekta ya madini iliyomalizika jana (Local content).

Utekelezaji wa miradi ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) ni moja ya mada iliyopewa kipaumbele kikubwa katika warsha hiyo ambapo washiriki walijadili changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika utekelezaji wa miradi hiyo na kutoa mapendekezo ya jinsi ya kuziondoa.

Akizungumza kuhusu warsha hiyo,Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara, Apolinary Lyambiko, warsha hiyo ni muhimu katika kuimarisha na kuboresha ushirikishwaji wa Watanzania katika kutoa huduma mbalimbali mgodini hapo. “Mategemeo yetu ni kwamba tutaendeleakuwa na maboresho zaidi baada ya warsha hii ambayo iliwajumuisha maofisa kutoka migodi ya barrick nchini”alisema.

Ujumbe kutoka Tume ya Madini pia ulipata fursa ya kutembelea na kujionea shughuli za uchimbaji madini kwenye shimo la chini (underground) katika eneo la Gokona.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post