UVCCM DR. SAMIA FOOTBALL SUPER LEAGUE 2023 KUZINDULIWA RASMI AGOSTI 26 SHINYANGA

Kamati ya Mashindano Wilaya ya Shinyanga Mjini ikitambulisha Jezi zitakazotumika kwenye mashindano ya UVCCM Dr. Samia Football Super League 2023 leo Agosti 08 2023 kwenye Ukumbi wa CCM Wilaya Shinyanga Mjini.

Na Halima Khoya-Malunde 1 Blog

Mashindano ya UVCCM Dr. Samia Football Super League 2023 Wilaya ya Shinyanga Mjini yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi Agosti 26, 2023 yakiongozwa na kauli mbiu "SHINYANGA BALL LIMERUDI",ambapo fomu za usajili kwa timu zitakazoshiriki zitaanza kuchukuliwa Agosti 9 2023 na kurudishwa Agosti 16 2023 na jumla ya timu zitakazoshiriki mashindano hayo ni Timu 32.

Akisoma taarifa kwa Viongozi wa Timu kwenye kikao kilichofanyika Agosti 08 2023 katika ukumbi wa CCM Wilaya Shinyanga mjini, Katibu wa Uhamasishaji UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini, Samson Suleiman amesema siku ya kuzinduliwa mashindano hayo kutakuwa na zoezi la kugawa jezi kwa Timu shiriki na ratiba ya mashindano itatolewa.

Amesema UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini 
wakishirikiana na Taasisi ya Bega kwa Bega na Mama Samia
wameandaa mashindano hayo ya mpira wa miguu wilaya ya Shinyanga mjini yatakayojulikana kama DR SAMIA FOOTBALL SUPER LEAGUE  yanayotarajia kuzinduliwa tarehe 26/08/2023 yanayotarajia kushirikisha jumla ya timu 32.

Suleiman amesema kuwa mashindano yatakuwa ya mtoano (Knock out) huku timu zitakazoshiriki ni 32 na baada ya hatua ya mtoano zitatakiwa kubaki timu 16 ambazo zitagawanyishwa kwa makundi manne (4) (kila kundi litakuwa na timu (4)) ambapo kila kundi litatoa timu mbili (2) kwa ajili ya kuingia hatua ya robo fainali.

“Baada ya kuingia hatua ya robo fainali litafunguliwa dirisha dogo kw aajili ya kufanya usajili kwa timu zeye uhitaji,mashindano haya yanashirikisha makundi maalum (Boda Boda,Wafanyakazi wa Sokoni,Wanafunzi wa vyuo kama VETA,chuo cha Kolandoto,S.t Joseph,Shy com na Mwasele”,amesema Suleiman.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mashindano Wilaya Shinyanga Mjini, Jackline Isaro amesema mashindano hayo ni tija na fursa kwa vijana sambamba na kusisitiza nidhamu kwenye michezo hali itakayosaidia kupata ushindi na zawadi mbali mbali kwa timu hadi kwa mchezaji mmoja mmoja.
Mwenyekiti wa Mashindano,Jackline Isaro akizungumza na viongozi wa timu leo Agosti 08 2023 kwenye ukumbi wa CCM Wilaya Shinyanga mjini.
Mwenyekiti wa Mashindano,Jackline Isaro na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Madete wakiwa kwenye picha ya pamoja na kombe litakalotolewa kwa mshindi katika mashindano ya UVCCM Dr. Samia Football Super League 2023.
Mwenyekiti wa Mashindano,Jackline Isaro na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Madete wakiwa kwenye picha ya pamoja na kombe litakalotolewa kwa mshindi katika mashindano ya UVCCM Dr. Samia Football Super League 2023.
Mwenyekiti wa Mashindano, Jackline Isaro akiwa kwenye picha na kombe litakalotolewa kwa mshindi katika mashindano ya UVCCM Dr. Samia Football Super League 2023.
Viongozi wa Timu mbali mbali wakiendelea na kikao kilichofanyika Agosti 08 2023 kwenye ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini.
Viongozi wa Timu mbali mbali wakiendelea na kikao kilichofanyika Agasti,08,2023 kwenye ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini
Picha na Halima Khoya

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post