Wadau mbalimbali wanaoshiriki Maonesho ya Madini na Uwekezaji mkoani Lindi wamevutiwa na bidhaa zilizozalishwa na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) katika banda la Wizara ya Madini.
Bidhaa hizo ni pamoja na hereni, Pete pamoja na bangili za mawe.
Pia, wadau hao wameshauri kuwepo na vituo vya mauzo na mafunzo ya uongeza thamani madini katika maeneo mbalimbali nchini ili kuongeza uelewa wa uongezaji thamani madini.
Aidha, Afisa Biashara kutoka TGC ametumia fursa hiyo kutoa fomu za kujiunga na mafunzo ya uongezaji thamani madini yanayotarajiwa kufanza mapema mwezi Oktoba jijini Arusha.
Mafunzo yatakayotolewa ni pamoja na Stashahada ya Uongezaji thamani madini ya Vito na kozi fupi za utambuzi wa madini, ukataji wa madini na usonara.
Social Plugin