WIZARA, WADAU WA MADINI WATEMBELEA SOKO LA KIMATAIFA LA YIWU NCHINI CHINA



Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo akiambatana na Rais wa Shirikisho la Vyama Vya Wachimbaji Tanzania (FEMATA) John Bina pamoja na ujumbe wa  wadau wa madini, leo Agosti 14, 2023 wametembelea Soko la Kimataifa la Yiwu  nchini China  kujionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa kwa kutumia madini ikiwa ni sehemu ya kujifunza.

Bidhaa hizo ni pamoja na vito, vifaa vya umeme ikiwemo magari, vyombo na mapambo ya ndani.

Safari ya wadau wa madini nchini China inajumuisha wafanyabiashara wa madini, wachimbaji na  watoa huduma migodini .

Aidha, mbali na wadau hao, pia, watendaji wa taasisi  chini ya wizara pamoja na taasisi za fedha wanashiriki katika ziara hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post