WATUMISHI MADINI WATEMBELEA MGODI WA BULYANHULU



#Katibu Mkuu Madini aanza Utekelezaji Maazimio


Timu ya Watumishi wapatao 13 kutoka kada mbalimbali za Wizara ya Madini ikihusisha Makatibu Mahususi, Watunza Kumbukumbu na Wahudumu wametembelea Mgodi wa Barrick - Bulyanhulu uliopo Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.

Ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio na ahadi alizotoa Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo lililofanyika mwezi Mei, 2023, jijini Dodoma.

Aidha, ziara hiyo inalenga kuwajengea uelewa wa pamoja  watumishi wote wa Wizara kuhusu shughuli zinazofanywa katika  Sekta ya Madini hususan shughuli za uchimbaji wa madini  katika migodi mikubwa, ya kati na midogo  ili kuwezesha malengo mahususi ya wizara kutekelezwa kwa pamoja kama familia moja ya Madini. 

Watumishi hao wamepata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali katika mgodi huo ikiwemo mgodi wa chini ( underground mining), sehemu  ya uchenjuaji (processing plant) bwawa la huifadhi tope sumu ( TSF) , sehemu ya upokeaji na utunzanji wa vifaa vinavyotumika katika mgodi pamoja na kutembelea miradi ya jamii inayotekelezwa na migodi hiyo kupitia  Mpango wa Uwajibikaji wa Migodi kwa Jamii (CSR).

Hili ni kundi la kwanza la watumishi wa kada hizo kutembelea maeneo ya migodi ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa. Kundi lingine la watumishi kutoka kada hizo linatarajiwa kutembelea migodi mbalimbali  mapema mwezi Septemba.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post