Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) imefanya mkutano wa hadhara ( taftishi) baada ya kupokea maombi ya marekebisho ya bei za maji kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) ambapo wananchi wamepata fursa ya kutoa maoni yao kuhusu ombi la kurekebisha bei za majisafi na usafi wa mazingira kwa miaka mitatu 2023/24 hadi 2025/26.
Mkutano huo wa hadhara (Taftishi) umefanyika leo Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme.
Mhe. Mkude amesema mkutano huo wa kutoa maoni unalenga kuchochea ufanisi katika utoaji wa huduma ya majisafi na usafi wa Mazingira mjini Shinyanga hivyo kuwataka wadau kushiriki kikamilifu kutoa maoni yao.
“Mkutano huu unaleta taswira njema kwamba Serikali ya awamu ya sita na taasisi zake siku zote imekuwa mstari wa mbele katika kuwashirikisha wananchi juu ya hatma na mipango ya kujiletea maendeleo. Serikali imekuwa ikifanya jitihada kubwa katika kufanya mabadiliko na maboresho makubwa katika sekta ya maji ikiwa ni pamoja na kuongeza uwekezaji katika sekta ya maji ili kuendana na changamoto mpya zilizo mbele yetu na pia kuendana na mabadiliko makubwa kiuchumi na kijamii yanayoendelea kwa sasa”,amesema .
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakati akifungua Mkutano wa hadhara (Taftishi) juu ya maombi ya kurekebisha bei za huduma ya maji safi na usafi wa mazingira yaliyotolewa na SHUWASA.
Mkude amewaomba watumiaji wa huduma za maji kuwa makini, kujenga hoja na kushirikiana kutoa maoni bila upendeleo wowote kwa dhamira ya kuhakikisha kuwa kuna mizania kati ya watumiaji huduma za maji safi na usafi wa mazingira, SHUWASA na taifa linafikia malengo yake ya upatikanaji wa huduma kwa watu wengi zaidi na ubora unaokidhi viwango.
Mkude amesema watumiaji wa huduma za maji wanayo haki ya kupata huduma kwa wakati, kwa bei halali, kuhoji ubora wa huduma wanazopata na kutoa malalamiko kwa watoa huduma lakini pia wana wajibu wa kulipia huduma kikamilifu kwa muda muafaka.
Akiwasilisha hoja ya marekebisho ya bei za maji, Mkurugenzi wa SHUWASA Mhandisi Yusuph Katopola amesema Maombi ya marekebisho ya bei ya maji, waliyoyawasilisha EWURA yanalenga kupata fedha za kutosha kukidhi gharama halisi za uendeshaji na matengenezo kwa lengo la kuboresha huduma zitolewazo na kwamba bei zinazopendekezwa zitaiwezesha Mamlaka kumudu gharama zote za utoaji huduma na hivyo kuendelea kuongeza ubora wa maji, kuiwezesha mamlaka kuwa endelevu na kukidhi matarajio ya wana Shinyanga ya kupata huduma za maji safi na salama.
Mhandisi Katopola amezitaja sababu za kuomba marekebisho ya bei za maji zinazotarajiwa kuanza kutumika kuanzia Septemba 2023 kuwa ni pamoja na kuisha kwa muda wa bei za awali, kuongezeka kwa bei ya jumla ya kununua maji kutoka KASHWASA, uwepo wa kodi na ushuru mbalimbali, kupanda kwa gharama za uendeshaji kuongezeka kwa maeneo ya kutoa huduma mfano Mwamalili, Didia, Iselamagazi na Tinde.
Amesema bei za bei walizopendekeza kwa kundi la wateja wa majumbani ni shilingi 2550/= (2023/2023), sh 3,190/= (2024/2025) na 3,630/= (2025/2026) kutoka sh. 1740/= kwa sasa kwa unit moja na huduma za kurejeshewa huduma ya maji baada ya kusitishiwa kutoka sh. 10,000/= hadi sh. 15,000/=.
“SHUWASA inahudumia Manispaa ya Shinyanga na Miji Midogo ya Tinde, Didia na Iselamagazi ili kuboresha huduma za utoaji maji safi tumeomba marekebisho ya bei mpya za maji. Kwa miaka yote tumeendelea kupata hati safi kutoka ripoti za CAG, SHUWASA imeendelea kuwa mamlaka bora kwa udhibiti wa upotevu wa maji tumepata tuzo. Tuwashukuru wananchi kwa kuendelea kutupa taarifa za uvujaji maji”,amesema Mhandisi Katopola.
Amesema baadhi ya changamoto zilizopo kuwa ni pamoja na mwamko mdogo wa wananchi kulipia bili ndani ya siku 30 hali inayosababisha wakati mwingine Mamlaka kusitisha huduma za maji kwa wananchi.
Ameyataja miongoni mwa malengo ya SHUWASA ni kusafirisha maji safi na bora kwa wateja, kuendelea kusambaza mabomba hadi kwenye maeneo ya nje ya mji, kujenga mitambo ya kuchakata majitaka na kwa kutumia TEHAMA wanataka kuboresha huduma zinazoridhisha wateja wao.
Akizungumza wakati wa Mkutano huo, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) George Mhina ambaye ni Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa amesema mkutano huu ni sehemu ya uchunguzi unaofanywa na EWURA kupata maoni ya wadau wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kabla ya kutoa maamuzi kuhusu maombi yaliyowasilishwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga ya kurekebisha bei za huduma za majisafi na usafi wa mazingira.
“Taratibu zinazitaka mamlaka za maji nchi nzima kufanya mapitio ya gharama zake kila baada ya miaka mitatu ili kubaini ikiwa bei ya maji inayotozwa inawezesha utoaji wa maji kwa ubora huku maslahi ya wateja na wadau yakizingatiwa. Hivyo katika maombi haya, SHUWASA imeomba kufanya marekebisho ya bei zitakazotumika kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2023/24 hadi 2025/26. Sisi EWURA matumaini yetu ni kuwa maoni yenu katika mkutano huu yatatusaidia kufikia uamuzi wa haki kuhusiana na maombi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga”,amesema Mhina.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) George Mhina ambaye ni Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara (Taftishi) juu ya maombi ya kurekebisha bei za huduma ya maji safi na usafi wa mazingira yaliyotolewa na SHUWASA.
“Sisi EWURA, pamoja na mambo mengine, majukumu yetu ni pamoja na kuhakikisha kuwa huduma ya maji na usafi wa mazingira inawafikia watu wengi na kwa gharama yenye kukidhi matakwa ya uendeshaji na katika ubora unaokidhi viwango kwa kuzingatia pia uwezo wa wananchi”,ameongeza Mhina.
Amesema utaratibu huo wa kukusanya maoni ni moja ya njia za kutekeleza azma ya Serikali ya utawala bora kwa maana ya kuwashirikisha wananchi katika kufanya maamuzi mazito kama ya kubadilisha bei za huduma ya maji kwa kutoa maoni yao kwa njia ya uwazi bila kificho.
“Tangu kuanzishwa kwake, EWURA imefanya mapitio na tathmini ya maombi ya kubadilisha bei za huduma za maji kwa Mamlaka za Maji za majiji na miji yote mikuu ya mikoa .EWURA imekuwa na mfumo shirikishi wa kushirikisha wadau wote wakiwemo watumiaji wa huduma kama inavyofanyika SHUWASA kabla ya kupitisha maombi husika. EWURA bado haijatoa maamuzi, tunachojadili hapa leo ni rasimu ya mapendekezo ”,amesema.
“Utaratibu wa kupitisha maombi ya kurekebisha bei za huduma una hatua kuu saba ambazo ni; (1) Kupokea maombi; (2) Kupitia maombi na kuomba ufafanuzi pale inapohitajika; (3) Mkutano wa hadhara (taftishi) ndani ya eneo ambalo mamlaka imeomba; (4) Kupokea maoni ya maandishi; (5) Kufanya uchambuzi wa kina na kuwasilisha mapendekezo kwenye Bodi ya EWURA; (6) Maamuzi ya Bodi; na (7) hatua ya mwisho ni Kutangaza maamuzi ya Bodi (Agizo) kwenye Gazeti la Serikali. Katika Agizo hilo, EWURA itaainisha bayana misingi na hoja zilizozingatiwa katika kufikia maamuzi yake na masharti ambayo Mamlaka ya Maji Shinyanga itatakiwa kuyazingatia katika utekelezaji wa agizo la bei. Sehemu kubwa ya masharti hayo yanalenga kuboresha huduma ya maji kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kufikisha huduma ya maji katika maeneo ambayo kwa sasa hayana huduma hiyo”,ameongeza
Amebainisha kuwa, kwa mujibu wa Sheria ya EWURA, mtu yeyote asiyeridhika na uamuzi wa EWURA anayo haki ya kukata rufaa kwenye Baraza la Ushindani wa Haki Katika Biashara yaani (Fair Competition Tribunal), kwa kifupi FCT.
“Pamoja na maoni yaliyotolewa leo, wadau wanakaribishwa kuwasilisha maoni ya maandishi kwa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, S.L.P. 2857, Dodoma ama kuwasilisha kwenye Ofisi za Makao Makuu ya EWURA, zilizopo Jengo la EWURA, Kiwanja Na 3, Kitalu Ad, Medeli Magharibi, au Ofisi ya EWURA Kanda Ya Ziwa Iliyopo Jengo la PSSF Ghorofa Ya 4 Upande wa Mbele, 33101 Nyamagana, 05 Barabara ya Kenyatta Jijini Mwanza. Maoni hayo yawasilishwe kabla ya tarehe 29 Agosti 2023 saa 100:00 Jioni. Maoni yatakayotolewa ndani ya wakati huo yatatumika pia katika kufikia maamuzi ya mwisho”,ameongeza.
Katika mkutano, Baraza la Ushauri la Serikali (GCC), Baraza la watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC Mkoa wa Shinyanga) na wananchi wamepata fursa ya kutoa maoni kuhusu bei hizo mpya za maji wengine wakisema bei zimepanda sana na wengine wakibariki mapendekezo hayo.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza wakati akifungua Mkutano wa hadhara (Taftishi) juu ya maombi ya kurekebisha bei za huduma ya maji safi na usafi wa mazingira yaliyotolewa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) leo Jumanne Agosti 22,2023. Picha na Kadama Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza wakati akifungua Mkutano wa hadhara (Taftishi) juu ya maombi ya kurekebisha bei za huduma ya maji safi na usafi wa mazingira yaliyotolewa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) George Mhina ambaye ni Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara (Taftishi) juu ya maombi ya kurekebisha bei za huduma ya maji safi na usafi wa mazingira yaliyotolewa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)

Mkurugenzi wa SHUWASA Mhandisi Yusuph Katopola akiwasilisha hoja ya ongezeko la bei kwenye Mkutano wa hadhara (Taftishi) juu ya maombi ya kurekebisha bei za huduma ya maji safi na usafi wa mazingira yaliyotolewa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Mkutano wa hadhara (Taftishi) juu ya maombi ya kurekebisha bei za huduma ya maji safi na usafi wa mazingira yaliyotolewa na SHUWASA ukiendelea
Wadau wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara (Taftishi) juu ya maombi ya kurekebisha bei za huduma ya maji safi na usafi wa mazingira yaliyotolewa na SHUWASA
Wadau wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara (Taftishi) juu ya maombi ya kurekebisha bei za huduma ya maji safi na usafi wa mazingira yaliyotolewa na SHUWASA
Mwenyekiti wa Baraza la watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC Mkoa wa Shinyanga, Joseph Ndatala akizungumza kwenye mkutano huo

Wadau wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara (Taftishi) juu ya maombi ya kurekebisha bei za huduma ya maji safi na usafi wa mazingira yaliyotolewa na SHUWASA.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin