WANANCHI KITOBO MISENYI WAANZA KUPATA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA



Na Mariam Kagenda _ Kagera

Wakazi zaidi ya 5000   wa  kata ya Kitobo wilaya ya  Missenyi mkoani Kagera wameondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama baada ya serikali kutekeleza mradi wa maji Kitobo uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 802.

Wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi huo Meneja wa Ruwasa wilaya ya Missenyi Mhandisi Andrew Kilembe amesema kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa January 18 mwaka 2022.

Mhandisi Kilembe amesema kuwa mradi huo umekamilika Juni 30 mwaka huu na kaya 102 kati ya kaya 973 na Taasisi 7 zimeunganishiwa huduma ya maji majumbani na zoezi la kuunganisha linaendelea.


Miundombinu ya mradi iliyojengwa ni pamoja na tenki la maji lenye ujazo wa lita 135000,tenki dogo lenye ujazo wa lita 50000, vituo 10 vya kuchotea maji , nyumba ya mtambo1 na ulazaji wa mabomba yenye urefu wa kilo mita 27.1 .

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2023 Abdalla Shaib Kaim ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa namna inavyoendelea kuisaidia jamii kwa kuondokana na  changamoto ya maji.

Baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo wameshukuru kuletewa mradi huo kwani walikuwa wanaancha shughuli za uzalishaji na kwenda kufata huduma ya maji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post