MWENGE WA UHURU WAMULIKA MIRADI YA BILIONI 10 KARAGWE, WATEMBELEA KIWANDA CHA MAZIWA 'KAHAMA FRESH'


Mkurugenzi wa kiwanda cha kuchakata maziwa wilayani Karagwe Josam Ntangeki (kulia) akipokea Mwenge wa uhuru baada ya kufika na kutembelea kiwanda hicho
Mkurugenzi wa kiwanda cha kuchakata maziwa wilayani Karagwe Josam Ntangeki (kulia) akipokea Mwenge wa uhuru baada ya kufika na kutembelea kiwanda hicho


Na Mariam Kagenda _ Karagwe

Mwenge wa Uhuru 2023 umekagua , kutembelea na kuzindua  jumla ya miradi  8 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya  shilingi Bilioni  10 wilayani Karagwe Mkoani Kagera. 


 Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa na mbio za Mwenge katika wilaya hiyo  ni pamoja na    mradi wa shamba la miti Kigarama,mradi wa vijana wa bodaboda,  vyumba vya madarasa Katembe, kuzindua jengo la huduma za upimaji na utengamano zahanati ya Kishoju, kiwanda cha kuchakata Maziwa cha  Kahama Fresh na mradi wa maji Bisheshe  .


Kiongozi wa mbio za Mwenge   kitaifa  2023   Abdallah Shaib Kaim baada ya kukagua na kutembelea  kiwanda cha Kahama Fresh amesema kuwa serikali ya awamu ya sita imeendelea kuweka mazingira bora na rafiki kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ili waweze kufanya uwekezaji wenye tija. 


Amempongeza mwekezaji wa kiwanda cha Kahama Fresh kwa kutengeneza ajira zisizopungua 300  kwa vijana  wa kitanzania kupitia kiwanda hicho.


Kwa upande wake mkurugenzi wa kiwanda cha Kahama Fresh Josam Ntangeki   amesema kuwa   kiwanda hicho kitakuwa na  uwezo wa kuchakata maziwa  lita elfu 10  kwa siku na maziwa hayo yatakusanywa kwa  wafugaji wanaozunguka mkoa wa Kagera na wataanza hivi karibuni.

Ameongeza  kuwa  kiwanda hicho  ni  mkombozi kwa wafugaji  kwani  wataweza kuwa na soko la uhakika  la maziwa kwa wafugaji wa ndani na nje na wanategemea kutoa ajira zisizopungua mia tatu kwa vijana wa Kitanzania.


Aidha amesema kuwa  kiwanda hicho kimeshaanza program maalum ya kopa Ng'ombe lipa Maziwa  na tayari wameanza  zoezi hilo kwa kukopesha ngombe mia tatu tangu mwaka jana na baada ya mwaka mmoja mfugaji anakuwa ameshamaliza deni lake na kubaki na  n'gombe.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post