Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya imetoa uamuzi mkataba wa Ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai (IGA) hauna tatizo hivyo pingamizi lililowekwa na walalamikaji halina mashiko.
Uamuzi huo umesomwa Alhamisi Agosti 10, 2023 na jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akishirikiana na Mustafa Ismail na Abdi Kagomba.
Madai yaliyotolewa uamuzi na mahakama hiyo ni pamoja na: Kama ibara ya 2, 4(2)... zinakiuka Ibara namba 1, 8 na 28(1) na (3) za Katiba ya nchi na pia kama IGA ni mkataba kwa muktadha wa Sheria ya Mikataba.
Katika madai hayo mahakama imesema IGA si mkataba unaoweza kusimamiwa na sheria ya mkataba.
“Mahakama imekubali kuwa Dubai ina mamlaka ya kuingia mikataba kama hiyo. Walalamikaji hawajaeleza kama Dubai imezuiliwa kuingia mkataba wa ushirikiano wa uwekezaji kwani ni suala la ushahidi,”amesema Jaji Ndunguru.