Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JAMAA ABEBWA NA UPEPO MKALI AKIJARIBU KUOKOA MWAMVULI WAKE

 

Mfanyakazi wa duka la mboga Burak Abuc mwenye umri wa miaka 26, nchini Uturuki ameponea kifo kwa tundu la sindano baada ya kujeruhiwa vibaya pale ambapo alijaribu kuokoa mwamvuli wake kutokana na dhoruba kali ya upepo.

Mwanamume huyo alikuwa akiuza bidhaa zake wakati upepo mkali ulipolipuka, ukitishia kupeperusha mwavuli kwenye kioski chake.

Mchuuzi huyo ameishia kusimulia yaliyomfika yote yalianza pale alipokimbilia kuokoa mwamvuli wa duka lake uliokuwa ukipeperushwa na upepo mkali wa upepo ambapo alihisi kwamba kwa kuung'ang'ania, angetumia nguvu na kuuweka imara chini, lakini badala yake akabebwa



Katika kujaribu kuuokoa mwavuli huo usipepee angani, aliruka na kuunyaka, akitumaini kuuweka sawa. Ni wazi kwamba mchuuzi hangeweza kufikiria kitu hicho alichopenda sana kikianguka juu ya rundo la chakula au kupeperushwa kuelekea mahali kusikojulikana.

Mwamvuli huo, hata hivyo, ulionekana kumzidi nguvu ukapeperushwa na upepo na kuwaacha waliokuwa pale wakiwa wameduwaa na kuwa na wasiwasi juu ya usalama wake.

Tukio hilo lililotokea katika jimbo la Mashariki la Erzurum na kunaswa kwenye video limesambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Katika mahojiano na TRT World, mfanyakazi huyo wa duka la aliyetambulika kama Burak Abuc alifichua kwamba aliruhusiwa kutoka hospitali baada ya kukaa kwa siku mbili katika ICU. 

"Nilivutwa kwa umbali wa takriban mita tano, nilipofungua macho, nilikuwa hospitalini," kijana huyo wa miaka 26 alisema. 

Video hiyo ilionekana kama tukio la sinema ya Hollywood, miguu ya Abuc ilipotoka kwenye lami na kupaa angani, akiwa ameshika mwaMvuli wake kama mtoto anayeng'ang'ania kwenye mdoli.

Abuc amepona kabisa na sasa anaona tukio zima kuwa la ucheshi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com