Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UWT YATAKIWA KUONGEZA NGUVU HARAKATI ZA MAREKEBISHO YA SHERIA YA NDOA, MCHUNGAJI LUDABANJA AWAGEUKIA VIONGOZI WA DINI


Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Afrika Bi. Anne Makinda akiingia ukumbini na mwenyekiti wa Bodi ya WILDAF Bi. Monica Mhoja.

Na Rose Mwalongo _ Dar es salaam

Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi ( UWT) umeaswa kujiunga na harakati za kupigania marekebisho ya Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 na kufanya umri kuwa miaka 18 ili kuwakomboa mabinti na ndoa za utotoni.


Rai hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Bodi ya WILDAF Monica Mhoja wakati wa Kongamano la kuadhimisha Siku ya Wanawake Afrika jijini Dar es Salaam ambalo liliandaliwa na shirika hilo pamoja na Women Think Tank.
Kwa upande wake, Mchungaji James Lubadanja alisema ni vema viongozi wa dini wakaelimishwa kuwa na msimamo mmoja wa kuhakikisha kuwa mtoto wa wa chini ya miaka 18 haozwi.

Alisema kuwa masuala ya imani yamegubikwa na utata na kukemea baadhi ya viongozi wa dini ambao wamekuwa wakiamuru waumini wa kike kuvua nguo wakati wa maombi au kuwashika maziwa jambo ambalo alisema ni kinyume na maandiko ya vitabu vya dini.


Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Wakili Harold Sungusia alisisitiza kuwa ni
vema tukaweka mizania na kamwe tusitumie Mungu katika kukumbatia ukatili dhidi ya binadamu wengine huku akiiomba Serikali kurekebisha Sheria ya Ndoa hususani umri wa kuolewa kuwa miaka 18 kwa mustakabali wa nchi.


Maadhimisho hayo pia yalitumika kumkumbuka mwandishi nguli Leila Sheikh na kutambua Mchango wake katika kutetea haki za wanawake Tanzania.


Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa ni Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Anne Makinda.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com