Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KITUO CHA TAARIFA NA MAARIFA CHA KIVULE CHAELEZA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KUTOKANA NA HARAKATI ZA NGUVU ZA PAMOJA


Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule kimeelezea mafanikio yaliyojitokeza kutokana na harakati za nguvu ya pamoja na wakishirikiana na Viongozi kwenye kata pamoja na Wananchi walipotembelea na kukagua ufanisi wa miradi hiyo ikiwa na lengo la kuwafikishia wananchi karibu hudama za muhimu.


Akizungumza wakati kutembelea miradi hiyo Afisa Maendeleo kata ya Kivule Anna Massawe amesema Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule kimekuwa na mchango mkubwa sana katika kuibua changamoto hasa zinazotokana na ukatili unaohusisha watoto, wanawake katika sehemu mbalimbali za Kata hiyo.


Pia amesema Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule imepambania kupaza sauti katika suala la ukeketaji ambapo kata ya Kivule ilikuwa ni miongoni mwa kata zilizokuwa zinaongoza kwa ukatili wa ukeketeji kwa watoto wa kike lakini kwa takribani miaka mitatu sasa kesi hizo zimeisha kabisa na kama zikiwepo hazifanyiki ndani ya kata hiyo, hivyo ikiwa ni faida ya elimu wanayoitoa Kituo hicho hasa kwa sauti zao wanazozitoa mashuleni na kwenye mikutano ya hadhara ndizo zilizosaidia kwa kiasi kikubwa chanamoto hii kuisha katika kata hiyo.


“Nimeweza kupokea watoto wengi wanaokimbia ukeketaji kwamba wengi wamepata uelewa mkubwa kuanzia kwa watoto, wazazi pamoja na jamii kwa ujumla.” Alisema Afisa Maendeleo


Pia amesema Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule kimeweza kuibua migogoro ya ndoa ambayo ilikuwa inasababisha wakinamama wanaonyanyaswa sana mfano vikiwemo vipigo, kunyimwa matumizi ya familia kwani hapo mwanzo hizo changamoto zilikuwa zinafichwa chini ya kapeti lakini kwa sasa zinazungumzwa na wengi wamejua kuwa ni makosa hivyo jamii imeendelea kuelimika.


Pia amesema KC Kivule imehamasha vijana kujiunga kwenye vikundi na mpaka sasa vikundi vya vijana vipatavyo 17 vimeweza kupata mikopo ya Halmashauri na vingine vingi vimeomba ambapo tunasubiria dirisha likifunguliwa wanaweza kupata mikopo hiyo ili kujikimu kimaisha na hamasa ya vijana kujiunga kwenye mikopo imekuwa kubwa katika kata ya Kivule.


Kupitia hamasa walizotumia Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule mpaka sasa Mtaa wa Magole wamepata shule kupitia nguvu zao za kuzungumza na wananchi, viongozi hata vyombo vya habari mbalimbali ambapo mwanzo mtaa huo haukuwa na Shule ya Msingi na Sekondari ambapo wanafunzi wengi walikuwa wanatembea umbali mrefu kwenda shule ambapo KC hiyo iliweza kuomba kuingia kwenye vikao vya Kamati ya Maendeleo ya kata na kuingia kwao ndo ilikuwa sehemu sahihi ya kutoa mapendekezo yaliyoleta mafanikio hayo. alisema Anna Massawe


Naye Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule, Zahara Mzee amesema kazi kubwa wanaibua changamoto zilizopo kwenye Kata hiyo na kuzichanganua ikiwa nikutafuta vipaumbele ambapo wanaweza kuiwasilisha sehemu husika ili kuweza kutatua changamoto hiyo kwenye Kata ya Kivule.


Amesema Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule kinashirikiana na wadau mbalimbali kupitia Afya wanashirikiana na Madaktari, kwenye elimu wanashirikiana na Walimu, Uongozi wa Kata pamoja na Polisi kwasababu kazi hizi wanaibua changamoto tofauti tofauti zikiwepo changamoto za kata husika pamoja na masuala ya ukatili wa kijinsia.


Naye mwanafunzi aliyepitia changamoto ya kupata mimba wakati akiwa kidato cha tatu (jina limehifadhiwa) amesema baada ya kupata ujauzito hakuweza kuendelea na shule na ikampelekea kukaa mwaka mmoja nyumbani lakini kutokana na Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule kupata taarifa hiyo waliweza kuwasiana naye na kuweza kumtafutia nafasi ya kuendelea na Shule kupitia mradi wa Mama Samia kupitia Rais wa Awamu ya Sita Dkt. Samia Suluhu Hassan aliweza kupata nafasi ya kuendelea na masomo na mwaka kesho atakuwa anahitimu kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Kitunda
Afisa Maendeleo kata ya Kivule Anna Massawe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule kwa kutoa mchango mkubwa sana katika kuibua changamoto hasa zinazotokana na ukatiliunaohusisha watoto, wanawake katika sehemu mbalimbali za Kata hiyo wakati wa kueleza mafanikio yaliyojitokeza kutokana na harakati za nguvu ya pamoja na wakishirikiana na Viongozi kwenye kata pamoja na Wananchi walipotembelea na kukagua ufanisi wa miradi hiyo ikiwa na rengo la kuwafikishia wananchi karibu hudama za muhimu.
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule, Zahara Mzee akizungumza kuhusu kazi zilizofanywa na kituo hicho wakati wa kueleza mafanikio yaliyojitokeza kutokana na harakati za nguvu ya pamoja na wakishirikiana na Viongozi kwenye kata pamoja na Wananchi walipotembelea na kukagua ufanisi wa miradi hiyo ikiwa na rengo la kuwafikishia wananchi karibu hudama za muhimu.
Afisa Ustawi wa Jamii Hospitali ya Wilaya ya Kivule, Irene Shembilu akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule kinavyosaidia kuibua changamoto zilizopo kwenye jamii na kwasababu wao ni wanajii na wanatokea kwenye jamii hivyo inakuwa ni rahisi kutambua changamoto ambapo aliweza kupokea kesi ya Fabian aliyeletwa hospitalini hapo na kumpatia huduma za kimatibabu kuokana na changamoto alizokuwa nazo na kesi yake iliripotiwa polisi na mwajiliwa wake aliweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu na pia weweza kupata kesi nyingi za ukatili wa kijinsia kupitia KC ya Kivule.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Abuuy Jumaa, Froida Mkya akizungumza na waandishi kuhusu changamoto ya Madarasa na matundu ya Vyoo yaliyokuwepo katika shule hiyo kupitia Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule kupasa sauti na kwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ni msikivu pale wananchi wanapoibua changamoto mama anasiki kwa kushirikiana na Serikali yake na anatatua changamoto hiyo hivyo mwaka jana wameweza kujengewa matundu 14 ya Vyoo, madarasa manne yamejengwa na kuweza kupata madawati kwenye vyumba hivyo vine hii itasaidia wanafunzi kuwa na mazingira sahihi ya kujifunza na hakika ufahuru utapanda.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Abuuy Jumaa, Froida Mkya akionesha vyoo vilivojengwa naSerikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan

Muonekano wa madarasa mapya manne na Vyoo ya Shule ya Sekondari ya Abuuy Jumaa
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule, Zahara Mzee akionesha kitolea ufafanuzi baadhi ya majengo ya shule mpya ya Magole inayotarajiwa kuanza hivi karibuni
Mwenyekiti wa Mtaa wa Magole , Abubakary Kindagule akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu mchango wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule kwenye kuhamasisha ujenzi wa Shule ya Msingi ya Magole ambapo wanafunzi walikuwa wanatembea kilometa saba hadi 10 kutafuta shule ambapo mpaka sasa mwanga umeonekana na Shule imejengwa tunasubilia sasa kuanza rasmi ili kupunguza mzigo kwa wanafunzi waliokuwa wanasoma umbali mrefu na mazingira ya Mtaa wa Magole kipindi cha mvua madaraja hayapitiki hivyo inapelekea mtoto kukosa masomo.
Mjumbe wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule Hamedi Katolela amesema kwenye kituo kunaibuliwa mambo mengi sana katika jamii hasa watoto wa kike kufanyiwa ukatili ambapo Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule kwa kushirikiana na jamii wanapopata taarifa zinafanyiwa kazi kwa kutoa taarifa kwenye Serikali ya Mtaa husika, mabalozi kwani watoto wengi wa kike na kiume kulawitiwa na kubakwa kwani wengi wao wanasoma shule ziliopo mbali hivyo wanavyokuwa wanakwenda shule au kurudi nyumbani njiani ufanyiwa vitendo vibaya hivyo kumalizika kwa shule ya msingi ya Magole itaweza kupunguza matukio hayo ambapo ameishauri jamii kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuweza kumaliza kabisa ukatili wa kijinisia katika kata ya Kivule.
Muonekano wa Shule mpya ya Msingi ya Magole iliyopo katika kata ya Kivule
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kivule, Amos Hangaya akizungumza kuhusu kupokea Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule wanachofanya kazi nacho kwa karibu ambacho kinapokea taarifa kutoka kwenye jamii zikiwemo za ukatili ambapo mpaka sasa kituo hicho kimeweza kushiriki kwenye kamati za maendeleo na pia kushiriki kwenye Bunge la Jamii ambapo waliweza kuibua changamoto zinazopatikana kwenye jamii inayowazunguka na kutoa mapendekezo yao kama wanajamii na yameweza kusaidia jamii kiujumla kujitambua na hata pia kwa Serikali ya mtaa kutambua vipaumbele vya jamii ili kuvitafutia ufumbuzi.
Mwalimu wa Shule ya Msingi Kivule Annex, Joyce Kwambela akizungumza na waandishi wa habari kuhusu vyumba kujistili vya mabiti wa kike wanapokuwa shule vilivyohamasishwa na Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule ambapo katika shule hiyo kwa sasa wanafunzi wa kikewanaweza kusoma bila tatizo lolote.
Mwalimu wa Shule ya Msingi Kivule Annex, Joyce Kwambela akiwaonesha waandishi wa habari sehemu ya kujistili mabiti wa kike wanapokuwa shule vilivyohamasishwa na Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule ambapo katika shule hiyo kwa sasa wanafunzi wa kikewanaweza kusoma bila tatizo lolote.
Mkazi wa Kivule, John Mbamba akitoa shukrani kwa Serikali pamoja na Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kivule kwa kuweza kuhamasisha ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami pamoja na changalawe ambapo wakazi wa Kivule sasa wajivunia na barabara hiyo.
Muonekano wa Barabara ya lami na vumbi iliyopo katika kata ya Kivule

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com