TGNP WAENDESHA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA KISHAPU


Wawakilishi wa vituo vya taarifa Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga wakiendelea na mafunzo kutoka kwa watoa elimu yaliyofanyika Agosti 12,2023 Wilayani humo.

Na Halima Khoya _ Malunde 1 blog

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) limetoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa vituo vya taarifa na maarifa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga ili kuwawezesha wanaharakati kuweza kujitegemea katika shughuli zao hali itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo endelevu.

Akieleza malengo ya mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) leo Agosti,12,2023 Mtaalamu kutoka Idara ya mafunzo,Ester William amesema TGNP imelenga kuleta mabadiliko makubwa kwa wanavituo vyaa taaarifa na maarifa Kishapu kwa kutoa mafunzo ya ujasiriamali ambayo ambayo yamelenga kuongeza thamani kwenye shughuli zao na harakati kwa ujumla .

Ameongeza kuwa kuwepo kwa wanaharakati wenye ujuzi wa ujasiriamali kuwa naa uchumi wenye nguvu na ambao utawasaidia kufanya harakati zenye tija. 

“Miongoni mwa mafunzo waliyoyapata ni namnaa yaa kufugaa kuku wa kisasa,ufugaji wa mbuzi,utengenezaji wa mafuta na batiki aina zote”,amesema Ester.

Kwa upande wake Mwezeshaji kutoka SIDO,Adam Samwel Hamis amesema mafunzo haya yatawasaidia kuinuka kiuchumi,kuendeshamiradi kwa weledi pamoja naa kusambaza elimu hii kwa watu wengine. 

Vile vile miongoni mwa washiriki wa mafunzo haya,Robert John na Zainab Issa kutoka vituo vyaa taarifa na maarifa Kata ya Maganzo naa Kiloleni walishukuru na kukiri kupata mafunzo haya na kubainisha kuwa kabla ya mafunzo walikuwa wanapata changamoto za kuendesha miradi endelevu. 
Wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga wakiendelea na mafunzo kutoka kwa watoa elimu yaliyofanyika Agosti 12,2023 Wilayani humo.
Wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga wakiendelea na mafunzo kutoka kwa watoa elimu yaliyofanyika Agosti 12,2023 Wilayani humo.

Wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga wakiendelea na mafunzo kutoka kwa watoa elimu yaliyofanyika Agosti 12,2023 Wilayani humo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post