Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TEMDO YAANZISHA KARAKANA YA KISASA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO YA VIFAA TIBA NCHINI


Mtalamu wa kutengeneza mashine kutoka Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) Mosses Chalamila akiwaelezea Wakulima waliohudhuria katika maonesho ya Nane nane Kanda ya Kaskazini yanayofanyika katika viwanja vya Themi njiro mkoani Arusha namna mashine ya kukamua mafuta ya mawese iliyobuniwa na taasisi hiyo inavyofanya kazi (Picha na Woinde Shizza).

Na Woinde Shizza, ARUSHA

KATIKA kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa vifaa tiba nchini, Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) imeanzisha karakana yakisasa kuzalisha vifaa tiba kwa ajili ya hospitali pamoja vituo vya afya hapa nchini.

Hayo yamekuja baada ya kipindi cha mwaka 2021/2022 ambapo taasisi hiyo iliamua kuwekeza zaidi ya Shilingi bilioni tatu kwa ajili karakana ya kisasa ya kutengeneza vifaa tiba aina 17
mpaka sasa baadhi ya vifaa tiba vimeshazalishwa.


Hayo yamebainishwa na Afisa mawasiliano na masoko wa TEMDO Dkt. Sigisbert Mmasi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika Maonesho ya Wakulima Nanenane yanayofanyika katika Viwanja vya Themi- Njiro, jijini Arusha ambapo alisema kuwa taasisi hiyo ina malengo makuu matatu ikiwemo kufanya tafiti zitakazotoa suluhu ya matatizo yaliyopo katika jamii.


Aidha alisema pia wanatoa mafunzo ya kihandisi kwa watu ambao wanafanya kazi ndani ya viwanda kwa ajili ya uendeshaji, usalama viwandani pamoja mambo mbalimbali yanayohusiana na uzalishaji tija viwanda.

Alisema kuwa TEMDO inatengeneza vifaa tiba kwa ajili hospitali, zahanati, vituo vya afya nchini lengo likiwa ni kupunguza uingizwaji wa vifaa kutoka nje ya nchi pamoja na kupunguza matumizi ya fedha za kigeni.

“Katika maonesho haya tumekuja kuonesha vifaa tiba ambayo vinatengenezwa TEMDO pamoja na kutoa elimu kwa Wakulima na wananchi waliohudhuria maonesho haya ya nane nane tunaamini kwamba watakuwa mabalozi wetu waziri wa kututangaza TEMDO na kuja kununua bidhaa zetu,"alisema.


Alibainisha kuwa tayari taasisi hiyo imeweka mikakati mbalimbali kuhakikisha kuwa inazalisha vifaa vya kutosha.

Alitaja baadhi ya vifaa hivyo wanavyovitenga kuwa ni pamoja na vitanda vya wodi ya wajawazito, stendi za kuwekea dripu,vitanda vya wagonjwa kufanyiwa uchunguzi pamoja na vitanda vya wagonjwa wanaolazwa ,jokofu la kuhifadhia maiti pamoja na kiteketeza uchafu wa hospitali ,ambapo alibainisha kuwa karakana hiyo kwa sasa ina uwezo wa kutengeneza vitanda zaidi ya 500 vya wajawazito na vitanda na vya wagonjwa wanaolazwa hospitalini.


“Taasisi yetu pia inazalisha majokofu yakuhifadhia maiti, pia tunatengeneza viteketezataka za mahospitali, hivyo tunakaribisha wadau wa afya na wamiliki wa hospitali binafsi za Serikali , zahanati na vituo vya afya kununua vifaa tiba katika taasisı yetu",alisema Dkt. Mmasi.


"Watanzania wenzangu ikiwemo wizara ya afya ,zahanati , hospitali za serikali pamoja na binafsi niwatake tu kutumia vifaa tiba vinavyoendana na uhalisia wa kitanzania vinavyotengenezwa na taasisi ya ubunifu na usanifu mitambo (TEMDO) kwani vinadumu muda mrefu na kwa kutumia vifaa vinavyotengenezwa ndani ya nchi vinasaidia kutokutumia fedha za kigeni kwa ajili ya kuagiza nje ya nchi ambayo ni gharama kubwa",alisema Dr Mmasi.


Aidha alisema kuwa mbali na vifaa tiba pia TEMDO wametengeneza mashine za aina mbalimbali za kilimo, viwandani pamoja na kutoa elimu kwa wahandisi na mafundi uchundo nchini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com