Na Elizabeth Kilindi,Njombe.
Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Pindi Chana amesema watanzania wanapaswa kurudi kwenye utamaduni halisi na sio kukumbatia tamaduni za kigeni ambazo hazikubaliki.
Ameyasema hayo wakati akizindua tamasha la kitaifa la Utamaduni lililofanyika viwanja vya stendi ya zamani mjini Njombe lenye kauli mbio isemayo utamaduni ni msingi wa maadili,tuulinde na kuuendeleza.
"Kauli mbiu inatutaka sote kwa umoja wetu tukemee vitendo vyote vinavyokizana na utamaduni wetu,hivyo niwaombe sana tukemee,tulinde utamaduni,tudumishe utamaduni wetu,utamaduni wetu ndio utambulisho wetu",amesema.
Awali Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Saidi Yakubu, amesema Rais aliagiza wizara kuratibu tamasha la utamaduni kila mwaka Tanzania bara na Zanzibar na kuyakutanisha makabila yote ili yaweze kutangaza tamaduni zao.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka,mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amesema tamasha hilo limetoa fursa kwa wananchi wa Njombe kwa kukuza uchumi wao.
Social Plugin