Leo tarehe 26/08/2023 Kiongozi Mkuu wa Makampuni ya Vanilla International Na Mvumbuzi wa miradi mikubwa ya kilimo cha Vanilla kwa jina la Vanilla Village Dodoma, Vanilla Village Zanzibar , Vanilla Village Arusha , Vanilla Village Dubai, Vanilla Village Comoro na Vanilla Village Mwanza, Simon Mnkondya amefanya mashindano mbalimbali ya kimichezo, sanaa na burudani kwa ajili ya kujenga mahusiano madhubuti kati ya kampuni na Mradi wa Vanilla Village Dodoma na Wananchi wa Dodoma hususani wanakijiji cha Zamahero Mayamaya.
Wananchi zaidi ya mia mbili wameshiriki michezo mbali mbali ikiwemo unywaji wa soda bila kuvuta futo (kuguda), kucheza michezo ya kurusha chupa, mpira wa miguu danadana , unywaji wa wines za vanilla na uimbaji wa muziki wa Utamu wa Vanilla na bila kusahau maswali ya matumizi ya vanilla.
Wananchi wa Dodoma wameufurahia mradi wa vanilla Dodoma na kuahidi kutoa ushirikiano wa kiulinzi na ufanyaji wa kazi kwa sababu mradi umeonekana kuwa chachu ya Ajira kwa Kanda ya Kati Dodoma hususani kwa vijana wa vijiji vinavyouzunguka mradi wa vanilla village Dodoma.
Mwenyekiti wa kijiji wa Zamahero, Wilson amekiri kuridhishwa na uhusiano uliopo kati ya mwekezaji huyo na wanakijiji wake.
Kwa niaba ya washiriki kijana Lupakisyo Yeremia amesema ni mwekezaji wa kuigwa kwa ushirikiano na wananchi hapa Dodoma.
Kwa upande wa Mwekezaji huyo , Simon Mnkondya amewaasa vijana na wananchi kwa ujumla kuchangamkia fursa ya uwekezaji wa vanilla kwani za kilimo mkombozi wa uchumi Tanzania na hususani kwa Dodoma.
Aidha amesema ameitisha burudani hiyo kwa sababu vanilla inahitaji ulinzi na bila mahusiano mazuri na wananchi mradi wa vanilla na vanilla zitadokolewa au kuibwa kama ilivyo Uganda na Kagera ambapo vanilla ni zao linaloongoza kwa kuibwa duniani kutokana na ukubwa wa bei ya vanilla inayofikia mpaka milioni moja licha ya kipindi kifupi cha kushuka kwa bei kutokana na ugonjwa wa Corona.
Amewashauri wananchi wawe na namba zake ili kupata mafunzo namba hizo ni 0769300200 au 0629300200 au 0624300200.
Social Plugin