Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Wakati Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI - The U.S. President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR) ukitimiza miaka 20 tangu uanzishwe mnamo mwaka 2003, mafanikio makubwa yameelezwa kufikiwa nchini Tanzania ikiwemo watoto wengi kuzaliwa bila Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI lakini pia maambukizi kupungua kufuatia wanaume kupata huduma ya tohara kinga.
Akizungumza Jumatatu Agosti 14,2023 na Waandishi wa Habari wanaofanya ziara Mkoani Mara kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 20 ya PEPFAR, Mratibu wa PEPFAR nchini Tanzania Bi. Jessica Greene amesema mapambano dhidi ya UKIMWI yamekuwa na matokeo chanya kwa kupunguza maambukizi hususani kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
“Tunapotimiza miaka 20 ya PEPFAR nchini Tanzania tunajivunia kuwa na matokeo chanya kwa watoto. Wakati tunaanza mpango wa PEPFAR ,kwa watoto wengi walikuwa wanaambukizwa Virusi vya UKIMWI kupitia mama zao wenye maambukizi ya VVU, na sasa hii ni dunia tofauti maana kuna watoto wengi wanaozaliwa bila kuwa na maambukizi kutokana na huduma ambazo mama zao wanazipata kipindi cha ujauzito na baada ya kujifungua”,amesema Greene.
Mratibu wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) nchini Tanzania Bi. Jessica Greene
“Sasa hivi watoto wengi wanaishi maisha wakiwa wenye afya njema na tunaelekea kwenye kizazi kisichokuwa na maambukizi ya UKIMWI ,haya ni mafanikio makubwa sana tuliyofikia tangu Serikali ya Marekani na Serikali ya Tanzania ilianzisha Mpango wa PEPFAR mnamo mwaka 2003 baada ya Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush kutangaza Mpango wa Dharura wa Kukabiliana na UKIMWI”,ameeleza Bi. Greene.
Amefafanua kuwa PEPFAR kupitia Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (The U.S. Center for Disease Control -CDC) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na wadau mbalimbali wakiwemo Amref Health Africa Tanzania wamekuwa wakitekeleza afua mbalimbali za afya kama vile kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto lakini pia kutoa bure huduma ya tohara ya kitabibu kwa wanaume.
“Serikali ya Marekani ndiyo mfadhili mkubwa zaidi wa misaada ya VVU/UKIMWI nchini Tanzania, ikiwa imewekeza zaidi ya dola bilioni 6.6 kumaliza janga la VVU. Tuna ubia na makampuni ya madawa na wabia wenye wigo mkubwa wa usambazaji ili kukuza upatikanaji wa ARV. PEPFAR inafadhiliwa moja kwa moja kutoka serikali ya Marekani kisha ufadhili huo unapelekwa kwa mashirika watendaji manne nchini Tanzania ambavyo ni USAID, Kituo cha Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa CDC, Walter Reed, Idara ya Ulinzi na Peace Corp.Tumejitahidi kutanua kazi zetu kwenye vituo vya afya”,ameongeza Bi. Greene.
“PEPFAR ilipoanza kazi nchini Tanzania, kulikuwa na watu wasiozidi 1,000 waliokuwa kwenye matibabu. Leo PEPFAR inasaidia zaidi ya watu milioni 1.6 kwenye matibabu ya ARV ya kuokoa maisha. Mwisho wa VVU/UKIMWI kama tishio la afya ya umma ifikapo 2030 ni lengo kubwa linaloweza kufikiwa”,amesema Bi. Greene.
Amesema Serikali ya Marekani inajivunia kushirikiana na Serikali ya Tanzania kufikia malengo ya shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Kupambana na Ukimwi Duniani (UNAIDS) 95/95/95 (95% ya watu wanaoishi na VVU wanajua hali zao, 95% ya waliogundulika wako kwenye matibabu, 95% ya wanaopata matibabu virusi vitakuwa vimefubazwa ifikapo 2025.
Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (CDC) nchini Tanzania Bw. Mahesh Swamination.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (The U.S. Center for Disease Control -CDC) nchini Tanzania Bw. Mahesh Swamination amesema huduma za tohara kinga wanazozitoa bure kwa wavulana na wanaume Mkoani Mara ili kuzuia maambukizi ya VVU kwa asilimia 60 zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza maambukizi ya VVU kwenye migodi na makambi ya Wavuvi.
“Tumekuwa tukitoa huduma za tohara kinga bure kwa wanaume kwenye vituo vya afya lakini kwa kuwafuata wananchi kwenye maeneo yao kupitia huduma ya Mkoba ambapo huwa tunapeleka huduma ya tohara katika jamii mfano kwenye migodi na makambi ya wavuvi. Huduma ya tohara inafanya vizuri Mara licha ya changamoto ya mila”,ameeleza bw. Swamination.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha afya Murangi kilichopo katika halmashauri ya Musoma, Dkt. Anceth Elias amesema kituo hicho kimekuwa kikitoa huduma za tohara kwa wanaume ikiwemo kupeleka huduma za tohara kwa wavuvi na wachimbaji wa madini ambapo mwitikio ni mzuri kwani tangu walipoanzisha huduma ya tohara kinga bure mwaka 2018 wanaume 35,539 wamepatiwa huduma ya tohara na wameendelea kujitokeza kupata huduma
Muuguzi na Mtoa huduma za tohara katika kituo cha afya Murangi halmashauri ya Musoma, Bi. Fasines Mwashitete.
“Mafanikio haya makubwa yanatokana na msaada mkubwa kutoka PEPFAR, tumekuwa tukitoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa tohara na mwitikio ni mzuri, wanaume watu wazima ambao hawakupata tohara wanajitokeza kwa wingi, tunawapa huduma ya tohara salama kabis tofauti na ile ya kimila ambayo ina madhara mengi ikiwemo kuvuja damu nyingi, maumivu makali na hatari ya kupata maambukizi ya VVU kwa sababu vifaa vinavyotumika kwenye tohara ya kimila siyo salama”,ameongeza Bi. Fasines Mwashitete na Musa Makele ambao ni wauguzi na watoa huduma za tohara katika kituo cha afya Murangi.
Naye Stephano Maphuru ambaye ni mnufaika wa huduma ya tohara anayetoa elimu ya umuhimu wa tohara amewaomba wanaume ambao hawajafanyiwa tohara kujitokeza kupata huduma hiyo ili kujikinga na maambukizi ya VVU kwa asilimia 60.
Mkuu wa Afua za UKIMWI kutoka CDC Tanzania, Dkt. Edward Machage na Mratibu wa Huduma za afya ya uzazi na mtoto Halmashauri ya wilaya ya Musoma Lameck Andrea Magori wamesema Maambukizi ya VVU kwa mjamzito na mama anayenyonyesha yanaweza kutokea wakati wowote (mtoto anapokuwa tumboni, wakati wa kujifungua au unyonyeshaji) hivyo ni muhimu kufanya vipimo vya marudio ili kujua hali yake na kumkinga mtoto asipate maambukizi.
Muuguzi Msaidizi wa Zahanati ya Chitare iliyopo kata ya Makojo Halmashauri ya Musoma, Neema Mshama na Muuguzi Mkunga wa zahanati hiyo, Hamis Zuberi wameishukuru PEPFAR kwa kuwapatia mafunzo kuhusu vipimo vya marudio kwa kwa akina mama ambapo kwa kipindi cha mwaka 2005- 2023 wamefanikiwa kuokoa watoto wawili wasipate maambukizi ya VVU baada ya kufanya vipimo vya marudio na kubaini mama zao wamepata maambukizi.
Mmoja wa akina mama walionufaika na huduma za PEPFAR Mariam Wambura (jina siyo halisi) mkazi wa kata ya Makojo Halmashauri ya wilaya ya Musoma ameishukuru PEPFAR kwa huduma inazotoa hali iliyochangia aendelee kuwa na afya njema licha ya kuwa na maambukizi ya VVU lakini pia kujifungua mtoto ambaye hana maambukizi ya VVU.
Mratibu wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI - The U.S. President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR) nchini Tanzania Bi. Jessica Greene akielezea mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa PEPFAR Agosti 14,2023 katika kituo cha Afya Murangi Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Mkoani Mara. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mratibu wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) nchini Tanzania Bi. Jessica Greene akielezea mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa PEPFAR
Mratibu wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) nchini Tanzania Bi. Jessica Greene akielezea mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa PEPFAR
Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (CDC) nchini Tanzania Bw. Mahesh Swamination akielezea mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa PEPFAR
Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (CDC) nchini Tanzania Bw. Mahesh Swamination akielezea mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa PEPFAR
Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (CDC) nchini Tanzania Bw. Mahesh Swamination akielezea mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa PEPFAR
Mkuu wa Afua za UKIMWI kutoka CDC Tanzania, Dkt. Edward Machage akielezea umuhimu wa vipimo vya marudio kwa akina mama katika Hudhurio la kwanza la kliniki (atakapogundua tu ni mjamzito), Ujauzito ukiwa na wiki 32 hadi 36 (miezi 8 hadi 9 ya ujauzito), Miezi 3 baada ya kujifungua, wakati wa kunyonyesha na Miezi 6 baada ya kujifungua, wakati wa kunyonyesha.
Waandishi wa habari wakiwa katika kituo cha afya Murangi Halmashauri ya Wilaya ya Musoma
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha afya Murangi kilichopo katika halmashauri ya Musoma, Dkt. Anceth Elias akielezea huduma wanazotoa ili kukabiliana na maambukizi ya VVU
Muuguzi na Mtoa huduma za tohara katika kituo cha afya Murangi halmashauri ya Musoma, Musa Makele akielezea huduma za tohara kinga kwa wanaume
Muuguzi na Mtoa huduma za tohara katika kituo cha afya Murangi halmashauri ya Musoma, Bi. Fasines Mwashitete akielezea huduma za tohara kinga kwa wanaume
Mnufaika wa huduma ya tohara Stephano Maphuru akihamashisha wanaume kupata huduma ya tohara kinga
Gari maalumu lenye huduma zote za Tohara Kinga kwa wanaume likiwa katika uwanja wa shule ya Msingi Kigera kata ya Kigera Manispaa ya Musoma ambapo huduma za tohara zinatolewa bure kupitia Mradi wa Afya Kamilifu unaokelezwa na Shirika la Amref Health Africa Tanzania kupitia CDC kwa ufadhili wa PEPFAR
Gari maalumu lenye huduma zote za Tohara Kinga kwa wanaume likiwa katika uwanja wa shule ya Msingi Kigera kata ya Kigera Manispaa ya Musoma ambapo huduma za tohara zinatolewa bure kupitia Mradi wa Afya Kamilifu unaokelezwa na Shirika la Amref Health Africa Tanzania kupitia CDC kwa ufadhili wa PEPFAR
Huduma za Upimaji VVU na tohara zikiendelea katika uwanja wa shule ya Msingi Kigera kata ya Kigera Manispaa ya Musoma
Vijana wa kiume wakipata elimu ya Tohara kinga katika uwanja wa shule ya Msingi Kigera kata ya Kigera Manispaa ya Musoma ambapo huduma za tohara zinatolewa bure kupitia Mradi wa Afya Kamilifu unaokelezwa na Shirika la Amref Health Africa Tanzania kupitia CDC kwa ufadhili wa PEPFAR
Mratibu wa Huduma za afya ya uzazi na mtoto Halmashauri ya wilaya ya Musoma Lameck Andrea Magori akielezea juhudi mbalimbali zinazofanyika kukabiliana na maambukizi ya VVU ndani ya miaka 20 ya PEPFAR
Mratibu wa Huduma za afya ya uzazi na mtoto Halmashauri ya wilaya ya Musoma Lameck Andrea Magori akielezea juhudi mbalimbali zinazofanyika kukabiliana na maambukizi ya VVU ndani ya miaka 20 ya PEPFAR
Muuguzi Msaidizi wa Zahanati ya Chitare iliyopo kata ya Makojo Halmashauri ya Musoma, Neema Mshama akielezea huduma zinazotolewa na PEPFAR ikiwemo vipimo vya marudio kwa mjamzito na mama anayenyonyesha
Mmoja wa akina mama walionufaika na huduma za PEPFAR Mariam Wambura (jina siyo halisi) mkazi wa kata ya Makojo Halmashauri ya wilaya ya Musoma akielezea jinsi alimwepusha mtoto wake kupata maambukizi ya VVU kupitia huduma za PEPFAR
Muuguzi Msaidizi wa Zahanati ya Chitare iliyopo kata ya Makojo Halmashauri ya Musoma, Hamis Zuberi akielezea huduma zinazotolewa na PEPFAR.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin