Mkurugenzi wa Vigimark Hotel Mjini Shinyanga, Antelope Hotel iliyoko Mwanza na Kampuni ya Mabasi ya Victoria Express , Abel Majige amefariki dunia Agosti 24,2023 usiku wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan Nairobi nchini Kenya.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika familia, kesho jioni mwili utawasili uwanja wa ndege Mwanza na kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Kanda Bugando, Jumatatu mwili utafuatwa Bugando na kulala nyumbani Lubaga Shinyanga. Jumanne Ibada katika kanisa la A.I.C.T na mwili kusafirishwa kwenda Salawe kwa ajili ya mazishi siku ya Jumatano
Social Plugin