Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DIWANI AWAKUMBUSHIA WALIMU UTUMISHI BORA

Diwani wa kata ya Bwilingu halmashauri ya Chalinze Mh. Nassar Karama(suti nyeusi) akizungumza na walimu


NA. ELISANTE KINDULU, CHALINZE

DIWANI wa kata ya Bwilingu ,katika halmashauri ya Chalinze mkoa wa Pwani, Mh. Nassar Karama amesisitiza walimu kufanya kazi kwa bidii na kufuata kanuni za Utumishi wa umma ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Mh. Nassar ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na walimu  wa shule ya msingi Kibiki katika kata ya Bwilingu, alipowatembelea leo shuleni hapo.

Mh. Nassar amesema Jambo pekee linalomjengea mwalimu heshima ni pamoja uadilifu na ufanisi katika kazi yake ya ualimu vitakavyomfanya kuepuka migogoro na mwajiri wake.

Aidha Mh.Nassar amesema kuwa kata yake bado inauhitaji mkubwa wa shule shikizi kutokana na wanafunzi wengi kusafiri umbali mrefu kufuata shule Kongwe mahali  zilipo.

" Mfano maeneo ya Kibiki Maziwa  na  Kitoho Kuna wimbi kubwa la wanafunzi kutembea umbali mrefu kuja kusoma hapa. Lazima tuone namna ya kuanzisha miradi ya Ujenzi wa shule kwenye maeneo yenye changamoto", alisema Diwani huyo.

 Mh. Diwani aliuelekeza uongozi wa shule hiyo kuitisha vikao vya wazazi na wadau wa maendeleo ya elimu kwa ajili ya  uhamasishaji wa kuwapatia watoto chakula shuleni, kuhimiza maadili pamoja na masuala ya kitaaluma.

Katika ziara hiyo walimu walitoa changamoto mbalimbali za kikazi zinazowakabili ikiwamo uhaba wa nyumba za walimu, uzio na kuwepo barabara inayopita pembezoni mwa  eneo la shule ambayo jamii itakuwa ikiitumia badala ya barabara ya Sasa ambayo inapita katikati ya viwanja vya shule hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com