Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita amezindua Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’ iliyopo Mjini Kahama katika eneo la Phantom nyuma ya maegesho ya Malori inayomilikiwa na Taasisi ya Charity Vision Tanzania (CVT).
Akizungumza leo Jumatatu Agosti 21,2023 Mkuu wa Wilaya Mboni Mhita ameishukuru na kuipongeza Taasisi ya CVT kwa kuanzisha Hospitali ya huduma za macho wilayani Kahama.
“Charity Vision Tanzania niwapongeze sana kwa kuwekeza kwenye changamoto za jamii, asanteni sana kwa kuleta huduma hii hapa Kahama. Nimeshuhudia vitendea kazi na mashine zilizopo hapa ni za kisasa, huduma zinatolewa kwa teknolojia ya hali ya juu”,amesema Mkuu huyo wa Wilaya.
“Niwashukuru CVT na wadau wetu Local Potential Enhancing kutoka Canada na Africa Relief & Community Development kwa kutuletea huduma za viwango vikubwa katika kutatua changamoto za macho. Wameleta vifaa, tunaamini kabisa watalaamu tulio nao watavuna ujuzi kutoka wa wadau wetu hawa wa kweli”,ameongeza Mboni.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (katikati) akipata huduma ya uchunguzi wa macho katika Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho CVT Specialised Eye Clinic Kahama.
Amesema serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kuboresha sekta ya afya kwani serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefungua milango na kuruhusu sekta binafsi kushirikiana na serikali kuboresha sekta ya afya.
“Wananchi wa Kahama hawataki maneno maneno, hawataki mbambamba wakisikia huduma inatolewa wanachangamkia ndiyo maana wamejitokeza kwa wingi kupata huduma za matibabu ya macho. Huduma nyingi za macho hupatikana kwenye Hospitali za Rufaa, hazitolewi kwenye zanahati na vituo vya afya hivyo kupitia Kliniki hii wananchi watatumia fursa hii kwa huduma bora kwa gharama nafuu.
Kahama ni kubwa, nashukuru mmekubali ombi langu la kuwafikishia huduma za macho wananchi wanaoishi pembezoni katika halmashauri za Ushetu na Msalala, wazee wetu wapate huduma”,amesema Mhe. Mboni.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (katikati) akikata utepe wakati wa uzinduzi wa CVT Specialised Eye Clinic Kahama.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama Dkt. Deogratius Nyaga ambaye ni Daktari Bingwa wa Macho akimwakilisha Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, amesema Kliniki hiyo ya CVT ina kila kitu, vifaa vingi vya kisasa hivyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kufikia malengo ya nchi katika utoaji wa huduma bora za macho kwa wananchi.
Kwa upande wao, wadau wanaoshirikiana na CVT kutoa huduma za kibingwa za macho Dkt. Mohamed Habsah kutoka Shirika la Local Potential Enhancing Canada na Mkurugenzi wa Miradi kutoka Africa Relief & Community Development UK, Mohannad Jaber wamesema lengo la kuanzisha Kliniki ya Macho/Hospitali ya macho ni kutatua changamoto za macho kwa wakazi wa Kahama kwani furaha yao ni kuona wananchi wanapata huduma bora za macho kwa gharama nafuu.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Charity Vision Tanzania (CVT), Yohana Baptist amesema wamekuwa wakishirikiana na wadau mbalimbali kutoa huduma za macho nchi nzima ambapo tangu waanze kutoa huduma za macho ndani ya miaka saba wamefanikiwa kutoa huduma za upasuaji wa macho kwa wateja zaidi ya 50,000 na tangu waanze kutoa huduma Wilayani Kahama Agosti 7,2023 mpaka wametoa huduma kwa wananchi zaidi ya 100 na mwitikio ni mkubwa.
Mkurugenzi wa CVT, Yohana Baptist akizungumza wakati wa uzinduzi wa CVT Specialised Eye Clinic Kahama.
“Tunahudumia pia hospitali za serikali na zisizo za serikali na tunashirikiana na madaktari bingwa binafsi. Tunatoa huduma za kutoa mtoto wa jicho kwa gharama nafuu kabisa kati ya shilingi 100,000/= hadi 150,000/=. Tumesogeza huduma za macho tukitumia madakari bingwa wa macho.
Tunawakaribisha wakazi wa Kahama na maeneo jirani kuja kupata huduma za macho. Tunaamini kabisa tutakuwa msaada mkubwa kwa serikali kwa kuhakikisha tunayafikia maeneo ambayo hayafikiki”,amesema Yohana.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Mhe. Underson Msumba ambaye ni mmoja wa wanufaika wa huduma zinazotolewa CVT amewasihi wananchi kuchangamkia fursa ili kutatua changamoto za macho zinazowakabili.
Nao baadhi ya wananchi waliopata huduma ya matibabu ya macho akiwemo Masanja Kimbulu, Maria Juma na Julius Machagi wameishukuru CVT kwa kuwasogezea huduma za matibabu ya macho wakieleza kuwa huduma zinazotolewa ni bora na viwango vya juu na kuahidi kuwa mabalozi katika jamii kutangaza huduma za kibingwa zinazotolewa kwa kutumia vifaa vya kisasa.
Meneja Msaidizi wa CVT) Sophia Mshanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa CVT Specialised Eye Clinic Kahama
HUDUMA ZINAZOTOLEWA CVT SPECIALISED EYE CLINIC KAHAMA
Huduma zinatolewa katika Hospitali maalumu ya Macho CVT Specialised Eye Clinic Kahama ni pamoja na Kuonana na Daktari Bingwa wa macho kwa ushauri na elimu juu ya magonjwa ya macho (Consultation/Ophthalmologist), Uchunguzi wa kina wa macho kwa vifaa vya kisasa (Comprehensive Eye Examination), Kipimo cha uoni wa pembeni kwa wagonjwa wa presha ya macho (Visual Field Analysis), Uchunguzi wa kina wa macho kwa wagonjwa wa kisukari (Diabetic Retinopathy), Usafishaji wa mtoto wa jicho kwa njia ya kawaida (Small Incision Cataract Surgery), Usafishaji wa mtoto wa jicho kwa njia ya teknolojia ya kisasa ( Phacoemulsification Cataract Surgery) na Huduma za mionzi ( Yag Laser Capsulotomy & Trabeculoplasty).
Huduma zote hizo zinatolewa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 2: 30 usiku.
Kwa Mawasiliano zaidi +255 624 959 639
CVT Specialised Eye Clinic Kahama ipo Phantom nyuma ya maegesho ya Malori Mjini Kahama.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (katikati) akikata utepe leo Jumatatu Agosti 21,2023 wakati wa uzinduzi wa Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’ iliyopo Mjini Kahama katika eneo la Phantom nyuma ya maegesho ya Malori. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (katikati) na wadau wakikata keki wakati wa uzinduzi wa Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’ iliyopo Mjini Kahama katika eneo la Phantom nyuma ya maegesho ya Malori.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati wa uzinduzi wa Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati wa uzinduzi wa Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’
Dkt. Mohamed Habsah kutoka Local Potential Enhancing Canada na Mkurugenzi wa Miradi kutoka Africa Relief & Community Development UK, Mohannad Jaber (kulia0 wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza na wadau wanaoshirikiana na CVT kutoa huduma za kibingwa za macho Dkt. Mohamed Habsah kutoka Local Potential Enhancing Canada na Mkurugenzi wa Miradi kutoka Africa Relief & Community Development UK, Mohannad Jaber (katikati) ambapo walimuahidi kupeleka pia huduma za matibabu ya macho katika Halmashauri ya Ushetu na Msalala badala la Manispaa ya Kahama pekee
Mkurugenzi wa Miradi kutoka Africa Relief & Community Development UK, Mohannad Jaber (katikati) akimuahidi Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita kupeleka pia huduma za matibabu ya macho katika Halmashauri ya Ushetu na Msalala badala la Manispaa ya Kahama pekee
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akiwashukuru wadau wanaoshirikiana na CVT kutoa huduma za kibingwa za macho Dkt. Mohamed Habsah kutoka Local Potential Enhancing Canada na Mkurugenzi wa Miradi kutoka Africa Relief & Community Development UK, Mohannad Jaber (katikati) kwa kukubali kupeleka pia huduma za matibabu ya macho katika Halmashauri ya Ushetu na Msalala badala la Manispaa ya Kahama pekee
Mkurugenzi wa Taasisi ya Charity Vision Tanzania (CVT), Yohana Baptist akizungumza wakati wa uzinduzi wa Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’ iliyopo Mjini Kahama

Dkt. Mohamed Habsah kutoka Local Potential Enhancing Canada akizungumza wakati wa uzinduzi wa Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’
Dkt. Mohamed Habsah kutoka Local Potential Enhancing Canada akizungumza wakati wa uzinduzi wa Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’
Mkurugenzi wa Miradi kutoka Africa Relief & Community Development UK, Mohannad Jaber akizungumza wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’
Mkurugenzi wa Miradi kutoka Africa Relief & Community Development UK, Mohannad Jaber akizungumza wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’
Julius Machagi akitoa ushuhuda namna alivyopata huduma za macho kupitia madakari bingwa kwenye Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’
Meneja Msaidizi wa Taasisi ya Charity Vision Tanzania (CVT), Sophia Mshanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’ iliyopo Mjini Kahama
Mratibu wa Taasisi ya Charity Vision Tanzania (CVT), Mariam Mbijima akizungumza wakati wa uzinduzi wa Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’ iliyopo Mjini Kahama
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama Dkt. Deogratius Nyaga ambaye ni Daktari Bingwa wa Macho akizungumza wakati wa uzinduzi wa Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’ iliyopo Mjini Kahama
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Underson Msumba akizungumza wakati wa uzinduzi wa Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’ iliyopo Mjini Kahama
Wadau wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic
Meneja Msaidizi wa Taasisi ya Charity Vision Tanzania (CVT), Sophia Mshanga akimwelezea Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (kushoto) kuhusu huduma zinazotolewa katika Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’ iliyopo Mjini Kahama

Daktari Bingwa wa Macho Dkt. Japhet Boniphace akimwelezea Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (kulia) namna wanavyotoa huduma za kibingwa kwa kutumia vifaa vya kisasa katika Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’ iliyopo Mjini Kahama
Daktari Bingwa wa Macho Dkt. Japhet Boniphace kutoka Dodoma RRH akimwelezea Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (kushoto) namna wanavyotoa huduma za kibingwa kwa kutumia vifaa vya kisasa katika Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’ iliyopo Mjini Kahama

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (kulia) akipata maelezo juu ya huduma za kibingwa kwa kutumia vifaa vya kisasa zinazotolewa katika Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’ iliyopo Mjini Kahama

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (katikati) akisalimiama na wananchi waliopata huduma ya macho katika Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’ iliyopo Mjini Kahama
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (kushoto) akipata maelezo juu ya huduma za kibingwa kwa kutumia vifaa vya kisasa zinazotolewa katika Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’ iliyopo Mjini Kahama

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (kushoto) akiuliza swali juu ya huduma za kibingwa kwa kutumia vifaa vya kisasa zinazotolewa katika Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’ iliyopo Mjini Kahama
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (kulia) akipata maelezo juu ya huduma za kibingwa kwa kutumia vifaa vya kisasa zinazotolewa katika Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’ iliyopo Mjini Kahama
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (kulia) akipata maelezo juu ya huduma za kibingwa kwa kutumia vifaa vya kisasa zinazotolewa katika Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’ iliyopo Mjini Kahama
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (katikati) akipata maelezo juu ya huduma za kibingwa kwa kutumia vifaa vya kisasa zinazotolewa katika Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’ iliyopo Mjini Kahama
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (katikati) akiangalia miwani katika Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’ iliyopo Mjini Kahama
Wadau mbalimbali wakiwa katika Hospitali Maalumu ya Huduma za Macho ‘CVT Specialised Eye Clinic’ iliyopo Mjini Kahama
Zoezi la kula keki likiendelea wakati wa uzinduzi wa CVT Specialised Eye Clinic Kahama

Muonekano wa sehemu ya jengo la CVT Specialised Eye Clinic Kahama
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin