Kwa mujibu wa kifungu cha 39 (1) cha Kanuni ya Adhabu (Penal Code), mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au popote, atakuwa ametenda kosa la uhaini iwapo ataamua:
* Kujaribu kumuua Rais
* Kuanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kwa mujibu wa kifungu cha 39 (2) cha Kanuni ya Adhabu (Penal Code), mtu yeyote akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, ambaye anajenga nia kusababisha au kuwezesha kusababishwa, au anajenga nia ya kuchochea, anashawishi, shauri au kuusia mtu yeyote au kikundi cha watu kusababisha au kuwezesha kusababishwa yoyote kati ya matendo au malengo yafuatayo, atakuwa ametenda kosa la uhaini:
* Kusababisha kifo, kumlemaza au kumjeruhi, au kufungwa au kumzuia Rais
* Kumwondoa Rais madarakani isivyo halali kutoka katika wadhifa wake wa Urais au kumwondolea ufahari, heshima na jina la Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Muungano
* Kupindua kwa njia zisizo halali, Serikali ya Jamhuri ya Muungano; au
* Kutishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Bunge na Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kubainisha nia hiyo kwa kuchapisha maandishi au machapisho au kwa kitendo chochote cha siri kinachojionyesha cha hali yoyote
Kwa mujibu wa kifungu cha 39 (3) cha Kanuni ya Adhabu (Penal Code), mtu yeyote ambaye, yumo katika utii wa Jamhuri ya Muungano, atakuwa ametenda kosa la uhaini kwa:
* Kuwa na mshikamno na maadui wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au anawapa msaada au hifadhi ndani ya Jamhuri ya Muungano au kwingineko
* Anachochea, aidha ndani ya Jamhuri ya Muungano au kwingineko, mtu yeyote aivamie Jamhuri ya Muungano kwa kutumia jeshi; au
* Anabeba silaha ndani ya Jamhuri ya Muungano kwa amri, kwa nia ya kutumia nguvu ya kuizuia, kuilazimisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano kubadilisha vigezo au ushawishi wake, au kwa nia ya kulazimisha au kuzuia au kutishia, Serikali ya Jamhuri ya Muungano
Kwa mujibu wa kifungu cha 39 (4) cha Kanuni ya Adhabu (Penal Code), mtu yeyote ambaye, yumo katika utii wa Jamhuri ya Muungano, akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, atakuwa ametenda kosa la uhaini kwa kuonesha nia ya kumsaidia adui wa Jamhuri ya Muungano kwa kufanya kitendo chochote kinacholenga au kinachoweza kutoa msaada kwa adui huyo, au kuingilia kwa maelekezo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano, au kuzuia operesheni ya Majeshi ya Ulinzi au Jeshi la Polisi, au kuhatarisha maisha, ana hatia ya kosa la uhaini.
⚠️ Adhabu ya kosa la uhaini ni kifo
✒️ Kanuni hii ya adhabu ni kwa mujibu wa Sheria ya Uhaini Namba 2 ya mwaka 1970
Social Plugin