Na Oscar Assenga, TANGA
ZAIDI ya Trilioni 7.81 zimetolewa na Benki ya CRDB nchini kwa ajili ya kuwezesha shughuli mbalimbali za kimaendeleo nchini hadi kufikia mwezi Agosti mwaka huu
Hayo yalisemwa na Meneja Mwandamizi wa Benki ya CRDB nchini Samson Keenja wakati wa uzinduzi wa kambi ya kupima afya bure maarufu Afya Check inayofanyika Jijini Tanga
Kambi hiyo ni juhudi za Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya kuhakikisha anawasogezea huduma za afya karibu wananchi wake.
Alisema uwekezaji huo mkubwa ni sawa na asilimia 26 ya fedha zote zinazotolewa katika mfumo wa kifedha Tanzania ukilinganisha na mabenki yote 60 nchini.
“Benki ya CRDB ndio inaongoza kwa upande wa huduma za kifedha na mpaka Agosto 13 mwezi huu tulikuwa tumeshatoa fedha za kuwezesha shughuli za maendeleo nchini Trilioni 7.81 na hata afya Benki imetoa mikopo mingi ya kuwezesha ujengaji wa vituo vya afya na uwendeshwaji vituo na kununua vifaa na vitu nyengine”Alisema
Aidha alisema kipekee kwa kipindi cha miaka minne kuanzia 2020 CRDB wamekuwa wakifanya matembezi ya kimataifa ya CRDB lengo kubwa ni kukusanya pesa zinazokwenda kwenye sekta ya afya na mwaka jana walikusanya milioni 470 na fedha hizo zilikwenda kwenye Sekta ya Afya JKCIA kwa ajili ya kusaidia upuasuaji wa magonjwa ya moyo pia CCBRT zilikwenda kusaidia wakina mama wanaopata mimba hatarishi.
Meneja huyo alisema kwa mwaka 2023 zimekusanywa sh. Bilioni 1 zinazokwenda kwenye sekta ya Afya kiasi kitakwenda kwenye huduma ya mama na mtoto Visiwani Zanzibar na kiasi kitakwenda kwenye CCBRT tena na kiasi kitakwenda JKCI.
“Sisi tumejisikia farahi kubwa sana kuwa sehemu ya kampeni hii ya Afya Chek na tunashiriki kama wafadhili kwa sababu kuu tatu kwamba wakitambua umuhimu mkubwa wa watanzania kupima afya zao mara kwa mara kama inavyoshauriwa ili kujua hali zao za kiafya ili kuweza kupata matibabu”Alisema
Hata hivyo alisema wao kama benki wanasema kampeni hiyo ni ya kipekee ndio maana wanaiunga mkono kwa sababu wanatambua watamzania wapo tofauti tofauti na ni muhimu kupima afya zao mara kwa mara .
“Sababu ya pili ya kuunga kwenye kampeni hiyo tunatambua moja hao watanzania ndio wateja wa CRDB Milioni 4 lakini ndio wale 11000 wanaomiliki benki hiyo na wana tofautiana kipato kuna wengine wana uwezo wanaweza kumudu gharama za kupima na wengine hawawezi”Alisema
Alisema ndio sababu ya kuunga mkono ubunifu huo wa kizalendo wa kupima afya bure kwa watanzania ili waweze kujua afya zao
Hata hivyo lengine liliwapelekea kuungano mkono ni Serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia imefanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya afya.
“Mimi ni shahidi wa uwekezaji kwenye miundo mbinu ya uwekezaji kwenye vifaa vya tiba ,uwekezaji kwenye watoa huduma madaktari,nesi nk katika Tanzania umefanyika kwa kiwango kikubwa sana hivyo inatupa moyo kama benki kuungana na serikali yao kuunga mkono jitihadaa hizo hivyo tuendelee akumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu”Alisema
Meneja Mwandamizi wa Benki ya CRDB nchini Samson Keenja akizungumza wakati wa uzinduzi wa kambi ya kupima afya bure maarufu Afya Check inayofanyika Jijini Tanga kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga na kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Tanga Januari
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kulia akisisitiza jambo wakati alipotembelea Banda la Benki ya NMB wakati alipozindua kambi ya kupima afya bure maarufu Afya Check inayofanyika Jijini Tanga
Social Plugin