Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo akizungumza wakati alipozindua zoezi la wanachama,wapenzi na mashabiki wa timu ya Simba kuchangia damu katika Zahanati ya Kisosora Jijini Tanga kulia ni Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Mkoa wa Tanga Edgar Mdime |
Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Tanga Edgar Mdime akizungumza kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo |
MKUU wa Idara ya Maabara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo Sinde Mtobu akieleza umuhimu wa uchangiaji damu |
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kulia ni Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Mkoa wa Tanga Edgar Mdime |
Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Mkoa wa Tanga Edgar Mdime akichangia damu
Na Oscar Assenga, TANGA.
MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Tanga Japhet Simeo leo amezindua zoezi la wanachama,wapenzi na mashabiki wa timu ya Simba kuchangia damu katika Zahanati ya Kisosora Jijini Tanga huku akieleza kwamba michezo ni moja ya nguzo muhimu katika utulivu na usalama kwenye nchi.
Simeo ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba kwenye uzinduzi huo alisema kwamba michezo ina tija sana katika maisha ya binadamu ikiwemo kuwaunganisha jamii na kutengeneza undugu.
Alisema kwamba uchangiaji wa damu ni muhimu ili kuokoa maisha ya wagojwa wahitaji wa damu wakiwemo waluopata ajali, wakina mama wajawazito na watoto waliopo katika hospital mbalimbali mkoani Tanga.
Mganga Mkuu huyo aliwapongeza wanachama hao kwa utayari wao wa kuona umuhimu wa kuchangia damu ambayo itakwenda kusaidia jamii yenye uhitaji huku akizitaka Taasisi, Vikundi na watu binafsi kuendelea kuwa na utamaduni huo ili kuweza kuokoa maisha ya watu wanaofika hospital kupata huduma hiyo.
"Nawapongeza mashabiki wa timu ya Simba SC kwa utayari wenu kuja kuchangia damu mimi nawaambia hii ni sadaka na thawabu kubwa sana mliyoitoa kwa wenzenu wenye uhitaji wa damu " Alisema Simeo.
Awali akizungumza Mwenyekiti wa Matawi ya Klabu ya Simba SC Edgar Mdime alisema kwamba zoezi la uchangiaji wa damu imekuwa ni utaratibu waliojiwekea kila mwaka lengo likiwa kuhakikisha wanakuwa sehemu ya kuokoa maisha ya wahitaji.
Alisema bado wanasukumwa kuchangia damu katika hospitali wakitambua kuwa uhitaji wa damu ni mkubwa kwa wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu hivyo licha ya kushiriki siku hiyo adhimu kwao bado wanaendelea kuhamasishana kujitoa kwa pamoja katika zoezi hilo.
Aidha alisema walianza na zoezi la usafi kubwa zaidi ilikuwa ni kuchangia damu na hamasa kubwa sana ambayo imetokea kwa mkoa huo kwa wana Simba na matawi yote wameungana kwa pamoja kwa ajili ya zoezi hili la kuchangia damu
Hata hivyo alisema kwamba wanajua damu ni muhimu sana kwa kila mmoja hasa ukizingatia wapo wakina mama wanaojifungua katika hospitali ikiwemo ajali zinatokea watu wanahitaji kuwekewa damu kwa hiyo wao wamehamasika kama wanajamii ukiachana na suala la michezo.
Tambo
Mwenyekiti huyo alisema kwamba dhamira yao kubwa msimu huu lazima timu yao ichukue Ubingwa kutokana na uwepo wa kikosi kipana kulingana na usajili mkubwa uliofanyika wakiamini lazima timu hiyo ifanye makubwa katika mashindano ya ndani na hata kimataifa pia.
Katika hatua nyengine, Mdime alituma salamu kwa watani zao timu ya wananchi Yanga kuelekea mechi za Ngao ya jamii zitakazo chezwa Mkwakwani Tanga ambapo ametamba kwa kusema kuwa hawatakuwa tayari ngao hiyo aichukue tena mtani mbele yao.
Mchezo huo unatarajiwa kucheza Agosti 9 mwaka huu katika uwanja wa CCM Mkwakwani Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ngao ya jamii watakutana na matajiri wa Chamanzi Azam FC huku Simba SC wao wakiminyana na Singida Fountain Gate katika hatua ya nusu fainali timu zote zikitafuta nafasi ya kuanza vyema msimu 2023/2024 .
Katika hatua nyengine, Mdime alituma salamu kwa watani zao timu ya wananchi Yanga kuelekea mechi za Ngao ya jamii zitakazo chezwa Mkwakwani Tanga ambapo ametamba kwa kusema kuwa hawatakuwa tayari ngao hiyo aichukue tena mtani mbele yao.
Mchezo huo unatarajiwa kucheza Agosti 9 mwaka huu katika uwanja wa CCM Mkwakwani Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ngao ya jamii watakutana na matajiri wa Chamanzi Azam FC huku Simba SC wao wakiminyana na Singida Fountain Gate katika hatua ya nusu fainali timu zote zikitafuta nafasi ya kuanza vyema msimu 2023/2024 .