MKURUGENZI wa Elimu Maalum Wizara ya Elimu Sayansi na Tekonolojia, Dk. Magreth Matonya akizungumza na washiriki wa kikao cha tathimni ya utekelezaji wa mradi wa uboreshji maisha ya watu wenye ulemavu kwenye sekta ya elimu unaotekelezwa na shirika la Foundation For Disabilities Hope (FDH) kwa ufadhiri wa The Faundation for Civil Society, juzi wilayani Mpwapwa, kulia ni mwenyekiti wa shirika hilo Michael Salali.PICHA PAUL MABEJA
Na Paul Mabeja, MPWAPWA
MKURUGENZI wa Elimu Maalum Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk. Magreth Matonya imemwagiza Ofisa Elimu maalum wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kuhakikisha kuwa anabainisha vikwazo vyote vinavyokwamisha watoto wenye ulemavu kupata elimu ili vipatiwe suluhu.
Dk. Matonya alisema hayo juzi wilayani hapa alipokuwa akizungumza kwenye kikao cha tathimni ya utekelezaji wa mradi wa uboreshji maisha ya watu wenye ulemavu kwenye sekta ya elimu unaotekelezwa na shirika la Foundation For Disabilities Hope (FDH) kwa ufadhiri wa The Faundation for Civil Society.
Alisema idara ya elimu maalum wilaya ya Mpwapwa inatakiwa kubainisha vikwazo mbalimbali ambavyo vinakwamisha jitihada za serikali pamoja na wadau wengine kusaidia watu wenye ulemavu kupata elimu.
“Watu wanawachukulia wenye ulemavu kama siyo watu nataka nipate changamoto zinazokwamisha walemavu kupata elimu ili waliopo nyumbani waweze kwenda darsani”alisema Dk.Matonya
Alisema baadhi ya vikwazo vilivyo hivi sasa ni pamoja na miundombinu isiyo rafiki katika shule mbalimbali ambazo zinakwamisha wenye ulemavu kupata elimu.
“Zipo chanGamoto nyingi kwa walemavu ikiwemo miundombinu ya vyoo isiyo rafiki, madarasa yenye ngazi badala ya mseleleko,umbali wa shule lakini pia ukosefu wa viti mwendu kwa wenye ulemavu wa viungo ambavyo kama wilaya mtashikamana kwa kutushirikisha sisi haiwezi kuwa tatizo tena”alisema
Aidha, alisema bado lipo tatizo la wazazi kufungia watoto wenye ulemavu ndani na kuwanyima haki yao ya kupata elimu kama ilivyo kwa wengine hivyo jamii inapaswa kubadili mtizamo huo ili kuwasaidia.
Pia, alisema shule nyingi nchini bado hazia walimu wenye taaluma rasmi inayohusu elimu maalum hivyo kushindwa kuwahudumia watoto wengi wenye mahitaji maalum.
“Walimu wengi wenye taaluma hii ya elimu maalum wengine wamesoma hadi ‘masters’ lakini hawapo katika shule zenye mahitaji maalum hivyo bainisheni changamoto hizo ili tuweze kuona ni namna gani walimu hawa wanakuja katika shule zenye uhitaji”alisisitiza Dk. Matonya
Kadhalika, aliwataka wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalum kushikamana ili kuwasaidia kupata haki zao za msingi kwani imekuwepo tabia ya baadhi yao kukimbia majukumu yao.
“Watoto wengi wenye ulemavu wamelelewa na mazazi mmoja kwani ipo tabia ya baadhi ya wazazi anapotokea mtoto mwenye ulemavu katika familia wanamkimbia lakini pia wapo wengine wanafikia hadi kuwafanyia vitu vya unyama”alisema
Ofisa Maendeleo ya Jamii Bruno Mwakibibi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walema alisema wameandaa Mwongozo utakao tumika kuwabaini watoto wenye mahitaji maalum utakaosambazwa katika maeneo mbalimbali.
Mwenyekiti wa Shirika FDH, Michael Salali alisema mradi huo unatekelezwa katika Kata mbili ambapo tayari wamewafikia walimu 250 na kuwapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo kuwahudumia watoto wenye mahitaji maalam.
“Mradi wetu unalenga kuwezesha watoto wenye ulemavu kupata elimu na kuondoa tabia kwa jamii kuwaficha ndani na hadi sasa tayari tumeibua watoto 72 lakini pia tumetoa elimu kwa makundi mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini,waganga wa jadi,kamati za shule, viomgozi wa kisiasa hali ambayo imesaidia vikao vya vijiji kufanya elimu maalum kuwa ajenda yao ya kudumu kwenye mikutano”alisema
Social Plugin