Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAMISHNA WA KAMISHENI YA USHIRIKISHWAJI JAMII CP SHILOGILE AKUTANA NA WANANCHI, MACHIFU ,SUNGUSUNGU, VIONGOZI WA DINI NA WAZEE WA KIMILA SHINYANGA

Kamishna wa jeshi la Polisi Kamisheni ya Polisi Jamii CP Faustine Shilogile akizungumza kwenye kikao hicho ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Polisi jamii fitness center mjini Shinyanga.
Kamishna wa jeshi la Polisi Kamisheni ya Polisi Jamii CP Faustine Shilogile akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Ukenyenge Kishapu.

Na Amo Blog Shinyanga.

Kamishana wa Kamisheni ya Ushirikishwaji Jamii CP Faustine Shilogile amefanya ziara ya siku moja ya kukagua miradi ya Polisi jamii mkoani Shinyanga ikiwa na lengo la kuimarisha mahusiano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi ili kuweza kushirikiana katika kuzuia na kutokomeza uhalifu mkoani Shinyanga.


Akizungumza wakati wa ziara hiyo ilifanyika Agosti 5,2023 Kamishina Shilogile ametumia ziara hiyo kuwakumbusha Polisi jamii katika Mkoa wa Shinyanga kuendelea kushirikiana na viongozi mbalimbali wa serikali, chama, Dini, viongozi wa kimila, wadau pamoja na wananchi katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao.

Aidha Kamishna Shilogile ametumia nafasi hiyo kumpongeza Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi kwa kuzuia na kupunguza uhalifu ikiwemo kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia pamoja na Rushwa zinazosababisha migogoro mbalimbali yenye uvunjifu wa amani.

Katika ziara hiyo, Kamishna Shilogile ameambatana na mratibu wa dawati la jinsia na watoto ACP- Faidha Suleiman ambaye kwa upande wake amewaomba viongozi hao kukemea mmomonyoko wa maadili ikiwemo kupinga vitendo vya ukatili vinavyoendelea kufanyika katika jamii.

Acp Faidha amesisitiza kutumia Askari wenye weledi katika madawati ya Jinsia kwani idara hiyo inahitaji umakini mkubwa katika kutatua changamoto za wahanga.

Naye Kamishna mstaafu wa Jeshi la Polisi Rt Sacp Englibert Kiondo pamoja na mambo mengine amewataka Askari wa kila kata kufuata mila na desturi za jamii husika ikiwa ni pamoja na kuhudhuria kwenye nyumba za ibada.

Akihitimisha ziara hiyo ndani ya wilaya ya Shinyanga, na Kishapu Kamishna Shilogile amepata wasaa wa kuongea na viongozi mbalimbali wa Serikali za mitaa ,Wananchi ,Jeshila jadi (Sungusungu) na madiwani pamoja na vikundi mbalimbali vya ulinzi shirikishi.

Kwa upande wake kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amemshukuru Kamishna Shilogile kwa ujio wakemkoani Shinyanga huku akiahidi kutekeleza maagizo yote yaliyo tolewa na kamishna huyo katika kuhakikisha wanaboresha utendaji kazi wa jeshi hilo na kuzuia uhalifu kwa kushirikisha jamii mkoanihumo.
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza kwenye kikao hicho ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Polisi jamii fitness center mjini Shinyanga.
Kamishna mstaafu wa Jeshi la Polisi Rt Sacp Englibert Kiondo akizungumza kwenye kikao hicho ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Polisi jamii fitness center mjini Shinyanga.
Kikao cha kuwajengea uwezo wa pamoja katika jukumu la ulinzi na usalama viongozi na polisi jamii kikiendelea katika ukumbi wa Polisi jamii fitness center mjini Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com