Imeelezwa kuwa maboresho ya ujenzi wa choo, .madarasa pamoja na uboredhaji miundombinu ya elimu katika kata ya Mabwepande vimepelekea ongezeko la ufaulu pamoja na kupungua changamoto ya utoro kwa wanafunzi wa shue ya sekondari Mabwepande.
Hayo yameelezwa leo wakati wa utoaji taarifa ya Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Mabwepande kilicho chini ya Mtandao wa Jinsia nchini TGNP ambapo akizungumza Katibu wa diwani kata ya Mabwepande Bw. Mawazo Malugu amesema Kituo cha Taarifa na Maarifa Mabwepande wametoa mchango mkubwa katika uboreshaji miundombinu ya afya, maji, elimu na barabara na hivyo kupelekea ongezeko la wanafunzi shuleni pamoja na ufaulu kwa zaidi ya asilimia 80.
Amesema kwenye jamii kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na Vituo vya Taarifa na Maarifa ili kuhakikisha jamii inapata ufumbuzi wa masuala yao kiurahisi na kuondoka na changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara kwenye jamii.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Mabwepande Bi.Fatma Nungu katika utendaji kazi wa kituo hicho imeweza kutatua chabgamoto zinazowakabili wananchi zaidi ya elfu 60 wanaoishi kata hiyo hususani katika barabara elimu.pamoja na afya kwa kutoa hamasa kwa wananchi kujitolea na kuihamasisha serikali ujenzi wa Zahanati na huduma ya maji na elimu.
Nao baadhi ya wananchi katika kata ya Mabwepande licha ya kukiri maendeleo yalioletwa kutokana na kituo cha taarifa na maarifa bado wameiomba serikali kuharakisha ujenzi wa shule ya msingi Bunju B ili kupunguza mwendo wa kufuata elimu kwa watoto ambao hulazimika kuvuka barabara ya Bagamoyo hali inayopelekwa baadhi yao kugongwa na magari.