MBUNGE PROF. NDALICHAKO AMWAGA MADAWATI KASULU


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kasulu mjini kupitia Mfuko wa jimbo la Kasulu Mjini mkoani Kigoma amekabidhi madawati 730 kwa halmashauri ya Kasulu Mjini ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini.

Akikabidhi madawati hayo Mbunge wa jimbo hilo Prof.Joyce Ndalichako amefafanua kuwa madawati hayo yamegharimu shilingi milioni 59, ambapo amempogeza rais Dkt.Samia Suluh Hassan kwa kuonesha njia katika sekta ya Elimu.

Prof. Ndalichako pia amesisitiza kuendelea kutumia fedha ya jimbo kwa maendeleo ya wananchi.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali.Isack Mwakisu amemshukuru mbunge hiyo kwa msaada huo na kueleza kuwa uwepo wake kwenye jimbo hilo umesaidia pakubwa wilaya hiyo kupiga hatua.

Naye mwenyekiti wa halmashauri ya Kasulu Mji Noel Hanura amemshukuru Prof. Ndalichako kwa kuwa mbunge Kiongozi ambaye pamoja na majukumu makubwa ya serikali aliyonayo amekuwa na utamaduni mzuri wa kukutana na wananchi na kutatua kero zao.

Mapema akitoa taarifa kwa Mbunge huyo Mkurugenzi wa halmashauri ya Kasulu Dollar Kusenge amesema msaada huo utasaidia kupunguza changamoto ya Madawati ambapo mpaka sasa halmashauri hiyo inaupungufu wa madawati, 22,500.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post