Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 31,2023 katika Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam
**************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) imepanga kushirikiana na halmashauri pamoja na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) katika kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa wenye mabasi na magari ya mizigo katika utunzaji wa mazingira kutokana na uwepo wa tabia kusimamia porini kwa lengo la kujisaidia (kuchimba dawa).
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka amesema moja ya jambo ambalo limekuwa likifanyika mara kwa mara kama mazoea ni mabasi ya abiria, malori na magari yanayofanya safari ndefu kuwa na kawaida ya kusimama porini kwa lengo la kujisaidia (kuchimba dawa).
Amesema tabia hiyo imechangia kuchafua mazingira na kuwa kero kwenye jamii, kwani hali hiyo imekuwa ikifanyika hata katika vyanzo vya maji na hivyo wakati wa mvua uchafu unasambaa na kuharibu mazingira.
“Mbali na hapo inadharirisha hasa kwa wenye jinsi ya kile, kwani mara nyingi maeneo wanayofanya hivyo si rafiki kwa binadamu kunaweza kuwa na wadudu au Wanyama wakali.
“Hivyo ni muhimu kushirikiana na Halmashauri mbalimbali kuhakikisha vyoo vinajengwa kila baada ya mwendo fulani kwenye maeneo ambapo Barabara Kuu zinapita, pia nipongeze baadhi ya mabasi ambayo yana vyoo ndani.
“Kuna watu wengi wanapitia wakati mgumu katika kujizuia wanapokuwa njiani wakati wa safari, wapo wanaoogopa kunywa maji kwa kuwa wanajua inaweza kumsumbua anapobanwa haja.”
Ameongeza kuwa elimu itolewe kwa abiria wanaotupa takataka mbalimbali barabarani wakati wa safari.
Kuanzia Wiki ijayo NEMC itatoa elimu kwa muda wa mwezi mmoja, baada ya hapo basi litakalokamatwa, litapigwa faini ya Tsh. Milioni tano.
Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 31,2023 katika Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 31,2023 katika Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 31,2023 katika Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam