Na Dotto Kwilasa, DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan amezindua jengo la kitega uchumi la Kanisa la Angikana Central Dodoma (DCT) lililopewa jina la Safina House huku akiweka msimamo wake Katika kuimarisha amani na utulivu nchini.
Amesema Kutokana na utulivu uliopo,kamwe Taifa halitayumbishwa dhidi ya watu wasio itakia mema Tanzania na kutumia nafasi hiyo kuwaomba viongozi wa Dini kuendelea kuhubiri amani, umoja na mshikamano.
Akizindua jengo hilo la kitegauchumi Leo Agosti 15,2023 jijini hapa, DK.Samia amesema,"Niwasihi viongozi wote wa dini nchini kuendelea kuliweka Taifa letu katika mikono salama ya mwenyezi mungu ili lidumu katika umoja, amani na mshikamano. Kamwe tusikubali kuyumbishwa na mtu yoyote yule asiyelitakia Taifa mema,”anasisitiza
Amesema serikali inatambua mchango wa taasisi za kidini nchini ambapo zimekuwa zikisaidia katika kutoa huduma za kijamii kwa wananchi ikiwemo elimu, kilimo na Afya.
Amefafanua kuwa Kabisa Angrikani ni kanisa kongwe zaidi duniani,na kwamba tangu kuingia kwake nchini limekuwa likitoa huduma kwa wananchi kwani shule nyingi zilijengwa ikiwemo shule ya msingi Mvumi,Mazengo na shule ya sekondari ya Msalato.
“Nimefurahi kusikia kuwa mnajihusisha na na kutoa mafunzo ya kilimo hasa Dodoma ambapo kuna ukame lengo ni kuhakikisha watu wanakuwa na chakula cha kutosha na salama kama ilvyonukuliwa katika kitabu cha zaburi ya 15;16,”
Aliongeza kuwa :“Suala la kilimo ni jukumu mlilobeba na ndio nguzo kuu ya serikali ndio maana tunatekeleza mradi wa Jenga Kesho Iliyobora (BBT) lengo ni kuhamasisha vijana kuingia katika kilimo, uvuvi na ufugaji.”
Katika hatua nyingine Dk.Samia alieleza kuwa serikali itaendelea kuenzi mchango wa kanisa la Anglikana pamoja na kudumisha umoja na mshikamano na kuifikisha Tanzania pale inapotakiwa.
“Muendelee kuwaimiza watanzania kufanya kazi kwa bidii na kuchangamkia fursa zilizopo Dodoma kwa ninyi ni mashaidi mtaona jiji hili linavyobadilika siku hadi siku na mwakani tutaitana wana pamoja kuelezana yote yaliyofanyika,”alifafanua
Kwa upande wake Askofu wa Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) Dk.Dickson Chilongani alimpogeza Rais Dk.Samia kwa kushiriki tukio hilo kwani ujio wake unaonyesha kuwa yeye ni kiongozi wa Dini zote.
Alisema hiyo sio mara ya kwanza kushiriki Rais Dk.Samia kushiriki katika matukio kama hayo.
“Sisi tunaendelea kukupongeza Rais Dk.Samia kwa uongozi wako mahili wako na kazi unazoendelea kuzifanya kwa maendeleo ya wananchi.Tangu umepokea kijiti hujayumba wala kuteteleka kwani miradi yote ya kimkakati iaendelea ikiwemo ujenzi wa bwawa la mwalimu nyeerere.
Ameongeza kuwa :”Miradi mingine ambayo inaendelea kutekelezwa ni ujenzi wa reli ya kisasa, barabara ya mzunguko, kukamilika kwa mji wa serikali, ujezi wa ikulu chamwio a ujenzi wa vituo vya afya a shule katika kila koa ya Tanzania hivyo uchumi kuendelea kukua.Tuamuomba mungu akujalie ili utuvushe hapa tulipo utupeleka katika Tanzania mpya.
Dk.Chilongani amesema DCT inaundwa na wilaya tatu za Dodoma ikiwemo Chamwino, Bahi na Mpwapwa ambapo kwa sasa ina jumla ya waumini 700,000 na wachungaji 300 ambapo kati ya wachungaji hao 65 ni wanawake ambao wamehitimu ngazi mbalimbali za elimu.
“Naishukuru serikali yako kwa kuendelea kutoa vifaa mbalimbali ikiwemo vitabu, walimu na chakula ambapo Hadi sasa DCT imefanikiwa kusomesha vijaa 7,000 wa shule za msigi a sekodari amapo wapo katika hatua mbalimbali za maendeleo.
Akizungumzia kuhusu jengo hilo Dk.Chilonga amesema ujenzi wake ulianza mwaka 2017 ambapo hadi kukamilika kwa jengo hilo wametumia sh.bilioni nane ambapo kati ya hizo sh.bilioni mbili ni msaada kutoka kwa rafiki kutoka Newyork.
Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa la Angrikana Tanzania Dk.Maimbo Mndolwa alisema kanisa hilo limekuwa likifanya kazi kwa kushirikiana na serikali.
“Leo umechukua nafasi ya kipekee kuungana nasi.kanisa linafanya kazi za kimaendeleo na kijamii na tunafanya kazi na makundi mbalimbali ya watu wenye changamoto.”
Ameongeza kuwa :”Kanisa linaendelea kuiombea serikali kwasababu hata Rais Dk.Samia anapigwa maneno mengi lakini watu hao ndio wa kwanza kula matunda ambayo yanatokana na uongozi wa serikali yake.
Social Plugin