RC TELACK ATEMBELEA BANDA LA TBS KWENYE MAONESHO NANENANE MKOANI LINDI


**************

MKUU wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Zainab Telack ametembelea banda la Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na kuipongeza kwa jitihada wanazozifanya katika kuwafikia wajasiriamali kwa wingi katika Mkoa huo kwenye Maonesho Maonesho ya Nane Nane yanayoendeleo kwenye viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.

Akizungumza wakati alipotembelea banda la TBS, leo Augosti 8,2023, Mhe.Zainab amesema Mkoa wake utaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Shirika hilo ili wafanyabiashara wadogo wadogo, wa kati na wakubwa waweze kufikiwa kwa urahisi na kuweza kusajili biashara zao ili ziweze kutambulika.

Nae Meneja wa Kanda ya Kusini, Mhandisi Saidi Mkwawa amesema kumekuwa na uingizaji wa bidhaa nchini ambavyo havina viwango, hivyo kupitia maonesho hayo wanatumia kuelimisha wananchi kuhusu masuala ya viwango.

Aidha amewataka wazalishaji wa bidhaa kufika kwenye banda la TBS lililopo kwenye Maonesho hayo ili waweze kupatiwa elimu ya namna bora ya uzalishaji pamoja na kufanya usajili wa majengo ya chakula na vipodozi.

Amesema kupitia Maonesho hayo imekuwa ni rahisi kuwafikia wajasiriamali mbalimbali wanaotembelea maonesho hayo kuwapatia elimu kuhusu masuala ya viwango wakati wanapozalisha na kuuza bidhaa zao.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post