Na Dotto Kwilasa, DODOMA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema serikali imeweka mazingira wezeshi kwa wakulima Ili kuzalisha mazao kwa wingi kwani ndiyo uti wa mgongo.
Senyamule ameseyasema Agosti 8,2023 Jiji la Dodoma wakati akihitimisha maenesho ya siku ya wakulima na wafugaji (Nane nane).
Amesema Kila halmashauri nchini itapata visima 150 na hivyo kwa upande wao kama mkoa wako tayari kupokea visima hivyo ili kuweza kuwanufaisha wakulima.alisem Senyamule"
"Dodoma tumedhamiria kukifanya kilimo kweli kuwa uti wa mgongo kama Dkt. Samia alivyo ifanya Tanzania kuwa hadhi ya chakula," amesem Senyamule.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe. Peter Selukamba amesema kuwa pato la mkoa huo linategemea kilimo kwa asilimia kumbwa.
Aidha ameongeza kuwa mategemeo yao nikwamba wakulima elimu waliyoipata itaenda kuwaongezea tija na hivyo kama mikoa miwili ya Singida na Dodoma inayolima alizeti kama zao la mkakati wanategemea kupata faida kubwa na kuwakaribisha wawekezaje kuja kuwekeza katika mikoa hiyo.
"Ni vyema Wizara ya mambo ya ndani itanganze haya maadhimisho kimaifa ili wakulima kuweza kupa fursa za kupata masoko zaidi nje ya nchi,"amesema Selukamba.