Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WAKULIMA


Na Dotto Kwilasa, DODOMA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema serikali imeweka mazingira wezeshi kwa wakulima Ili kuzalisha mazao kwa wingi  kwani ndiyo uti wa mgongo.

Senyamule ameseyasema Agosti 8,2023  Jiji la  Dodoma  wakati akihitimisha maenesho  ya siku ya wakulima na wafugaji (Nane nane).

Amesema  Kila halmashauri nchini itapata visima 150 na hivyo kwa upande wao kama mkoa wako tayari kupokea visima hivyo ili kuweza kuwanufaisha wakulima.alisem Senyamule"

"Dodoma tumedhamiria kukifanya kilimo kweli kuwa uti wa mgongo kama Dkt. Samia alivyo ifanya Tanzania kuwa  hadhi ya chakula," amesem Senyamule.

 Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe. Peter Selukamba amesema kuwa pato la mkoa huo linategemea kilimo kwa asilimia kumbwa.

Aidha ameongeza kuwa mategemeo yao nikwamba wakulima elimu waliyoipata itaenda kuwaongezea tija na hivyo kama mikoa miwili ya Singida na Dodoma inayolima alizeti kama zao la mkakati wanategemea kupata faida kubwa na  kuwakaribisha wawekezaje kuja kuwekeza katika mikoa hiyo.

"Ni vyema Wizara ya mambo ya ndani itanganze haya maadhimisho kimaifa ili wakulima kuweza kupa fursa za kupata masoko zaidi nje ya nchi,"amesema Selukamba.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com