Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YATENGA BILIONI 50 KUBORESHA KILIMO CHA ZAO KOROSHO NCHINI-NAIBU WAZIRI MAVUNDE

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Wadau wa Korosho nchini kilichofanyika Jijini Tanga ambapo alisema uboreshaji huo unakwenda sambamba na kuongeza bajeti kwenye sekta ya Kilimo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, ya Viwanda,. Biashara, Kilimo na Mifugo Mariam Ditopile akziungumza wakati wa mkutano huo
Mwenyekiti wa Bodi ya korosho Tanzania, Jenerali Mstaafu Aloyce Mwanjile akizungumza wakati wa mkutano
MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza wakati wa mkutano huo
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Pesa Angelica Pesha akizungumza akielezea namna wakulima watakavyonufaika kupokea malipo yao kupitia line zao za simu kwenye akaunti ya Tigo Pesa wakati wa mkutano huo
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Pesa Angelica Pesha akizungumza akielezea namna wakulima watakavyonufaika kupokea malipo yao kupitia line zao za simu kwenye akaunti ya Tigo Pesa wakati wa mkutano huo
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Pesa Angelica Pesha kushoto akiwa na washiriki wengine wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye mkutano wa wadau wa Korosho Jijini Tanga
Sehemu ya Wakuu wa Mikoa wakifuatilia mkutano huo
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) Saady Kambona katikati akiwa kwenye kikao hicho


Na Oscar Assenga, TANGA

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde amesema Serikali imetenga bajeti ya Sh.Bilioni 50 kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 kwa ajili ya kuboresha kilimo cha zao la korosho nchini.

Mavunde aliyasema hayo leo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Wadau wa Korosho nchini kilichofanyika Jijini Tanga ambapo alisema uboreshaji huo unakwenda sambamba na kuongeza bajeti kwenye sekta ya Kilimo.

Alisema hiyo itakuwa kwa ajili ya kulipia pembejeo zinazotolewa kwa wakulima ikiwemo pamoja na kugawa miche bora ya mikorosho kwa wakulima ikiwemo kuhuisha kanzidata ya wakulima wa Korosho.

Aidha alisema kanzidata hiyo ya wakulima wa korosho kwa kupima mashamba ikiwemo kuchukua GPS Codines kuhesabu idadi ya mikorosho kwa kutumia mfumo wa satellite, kupiga picha wakulima na kuchukua namba za vidole.

“Lakini pia kumpatia mkulima namba maalumu ya utambulisho ambayo ataitumia kupata pembejeo na kuuza korosh zake katika msimu unaokuja watahakikisha ile namba maaliumu ya mkulima ambayo anaitumia kama utambulishio wa kupata pembenejo ndio itakayotumika kuuzia korosho zake”Alisema

Mavunde alisema hiyo itawasaidia kupata takwimu sahahi za wakulima huku akiiagiza kwenye bodi ya Korosho nao wasimamizi wa usajili wa wakulima katika ngazi ya wilaya lazima sasa maelekezo washuke mpaka ngazi ya kata ili zoezi hilo liende kwa haraka zaidi ili waweze kuwasajili wakulima.

Hata hivyo alisema bado wanafikiria mpango wa kuongeza idadi ya wasimamizi kupitia usajili huo ambao utawasaidia kupata nafasi kujua aina ya wakulima walionao na ukubwa wa mashamba yao ikiwemo pembejeo wanazopokea na miche walionao.
“Hii itawasaidia sana kwenye takwimu zao kama serikali katika kuwahudumia wakulima lakini la tatu tutaendelea kuvutia na kuhamasisha uwekezaji mkubwa kwenye ubanguaji na usindikaji wa korosho “Alisema

Hata hivyo alisema tayari wamekwisha kutenga eneo la kutosha kwa ajili hiyo katika kijiji cha Maranje Kata ya Mtiniko Halmashauri ya Mji wa Nanyamba Mkoani Mtwara lenye ukubwa wa Ekari 1375 zimetengwa na zitatumika kujenga kongani ya viwanda

Katika hatua nyengine, Naibu Waziri Mavunde alisema kwa kulifanya zao hilo liendelee kuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi wa Taifa.

“Ukiangalia takwimu za dunia biashara ya kirosho kwa msimu uliopita ni Trilioni 17.8 duniani na inadiriwa ilifanyika na ifikapo mwaka 2028 biashara ya korosho itakuwa ni zaidi ya Trilioni 21.8 duniani hivyo inawaambie kwamba mfanye uwekezaji mzuri kuanza kwenye tafiti na kuwawezesha wakulima kulima kwa tija ipo fursa kubwa dunia kwa zao hilo”Alisema Naibu Waziri Mavunde

Awali akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya korosho Tanzania, Jenerali Mstaafu Aloyce Mwanjile amesema kuwa katika msimu wa mwaka 2022/23 jumla ya korosho ghafi zaidi ya tani laki moja 176.6 ziliweza kukusanywa na kuingiza zaidi ya Sh bilioni 328.

Alisema kati ya hizo tani zaidi ya laki 168 zilisafirishwa nje ya nchi na zilizobaki ziliendelea kubanguliwa ndani ya nchi na kwa msimu wa 2023/2024 bodi imepanda kuendelea kushirikiana na wadau wa korosho nchini kutekeleza mipango mbalimbali ya kuongeza uzalishaji,ubanguaji na ufanisi wa masoko nchini.

Aidha alisema kwamba bodi kwa kushirikiana na wizara wameendelea kufanya mazungumzo na wawekezaji ambao watafungulia Industry Park Maranja wilaya ya Nanyamba Mkoani Mtwara eneo ambapo kikifanikiwa watakwenda kuwa na ubanguaji wa tani zaidi ya laki mbili nchini jambo ambalo kwao wanaliona kama sahihi kwenye kuongeza thamani kwenye mnyororo wa zao la Korosho.

Naye kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akitoa salamu za mkoa kwenye mkutano huo alisema mkoa huo unatekeleza ilani ya CCM ya Mwaka 2020 ili kuweza kuongeza uzalishaji wa Korosho kufikia tani 700,000 itakapofika mwaka 2025/2026.

Alisema mkoa umepanga kuzalisha tani 10,000 ili kuweza kuchangia kwenye tani laki saba zilizopangwa kitaifa na wamejiwekea mipango mbalimbali ikiwemo ufufuaji wa mashamba pori ambapo mashamba pori 3382 yaliibuliwa na jumla ya ekari 328 zimekwisha kufufuliwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com