Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Damas Mfugale akiwa kwenye kikao na mabalozi ambao wamepangiwa vituo vyao hivi karibuni ikiwemo Ufaransa,Austria, Omani na Namibia ambapo wamkutana leo Agosti 24,2023 katika Ofisi za TTB Jijini Dar es Salaam
**************
EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
BODI ya Utalii nchini (TTB), imekutana na kuzungumza na Mabalozi wanne ambao wamepangiwa vituo vya hivi karibu ambapo wamejadili mipango ya kuhakikisha wanaleta watalii na wawekezaji w akutosha nchini.
Mabalozi hao wamepangiwa vituo vya Ufaransa, Austria, Omani na Namibia ambao hivi karibu watakwenda kwenye vituo vyao.
Akizungumza leo Agosti 24,2023 Jijini Dar es Salaam, mara baada ya kufanya kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Damas Mfugale amesema wamekutana na mabalozi hao kupeana uzoefu ambapo wameshauriwa kuboresha maeneo mbalimbali katika kutangaza Utalii.
"Mabalozi hawa wametupa uzoefu wao, wametushauri vitu vya msingi ambavyo vinaweza kusaidia Tanzania iweze kukua katika sekta ya Utalii". Amesema Bw. Mfugale.
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Austria, Balozi Naimi Aziz amesema wamepokea yale yote ambayo wameshauriwa kuyafanya katika kuhakikisha wanatangaza utalii na kuvutia wawekezaji kutoka maeneo mbalimbali.
Amesema wamekubaliana kushirikiana kwa pamoja wanapokwenda kwenye vituo vyao kuangalia ni jinsi gani wanaweza kuongeza idadi ya watalii ambao wataweza kutembelea nchi yetu.
Nae Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Balozi Ali Mwadini amesema wamejifunza mikakati ya kuwawezesha wawekezaji kuwekeza kwenye maeneo mengi ikiwemo vitalu, kuboresha utalii wa bahatini, utalii wa fukwe, utalii wa milima, utalii wa mito na maporomoko.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Damas Mfugale akiwa kwenye kikao na mabalozi ambao wamepangiwa vituo vyao hivi karibuni ikiwemo Ufaransa,Austria, Omani na Namibia ambapo wamkutana leo Agosti 24,2023 katika Ofisi za TTB Jijini Dar es Salaam
Social Plugin