***************
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Ndg. Sophia Mjema amewakumbusha wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kufanya siasa safi na kistaarbu na kujiepusha na matusi.
Ndugu Mjema ametoa wito huo Agosti 12, 2023 wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa hadhara wa Jimbo la Kigamboni ambapo mbunge aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Mjema amesema ‘‘Ndg zangu tuendelee kuwa na siasa za kistaarabu tusiingie katika mtego wa matusi na kelele, wakiongea maneno jibuni kwa kazi alizozifanya mama Samia."
Aidha, Ndugu Mjema amewaasa wanachama wa CCM kukisemea vizuri chama na Mwenyekiti, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
’Kila mwana CCM lazima aongelee sioni sababu uone haya au kigugumizi, lazima useme ili kuendelea kutawala, lakini kuyasema mazuri ya Mama na CCM’’
Social Plugin