Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA Dkt. Stella Bitanyi akitoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Mpemba iliyopo Wilaya ya Tunduma mkoa wa Songwe waliotembelea banda la TVLA kujifunza kazi mbalimbali za kimaabara zinazofanywa na TVLA hususani katika utoaji wa huduma za kiuchunguzi wa Magonjwa ya Wanyama, utafiti wa magonjwa ya Wanyama pamoja na Uzalishaji wa Chanjo za wanyama kwenye maonesho ya Kimataifa ya Nanenane yanayoendelea katika uwanja wa John kwenye Mwakangale Mkoa wa Mbeya Agosti 5, 2023.
Meneja wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA kituo cha Sumbawanga Dkt. Rajabu Mlekwa akitoa elimu kwa wadau wa Mifugo waliotembelea banda la TVLA kujifunza matumizi sahihi ya chanjo dhidi ya Homa ya Mapafu ya Ng’ombe (BOVIVAC-CBPP) inayozalishwa na TVLA kwenye maonesho ya Kimataifa ya Nanenane yanayoendelea katika uwanja wa John kwenye Mwakangale Mkoa wa Mbeya Agosti 5, 2023.
Afisa Mifugo Mtafiti mwandamizi wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA Dkt. Ronald Benju akifanya uchunguzi kupitia upasuaji wa Mzoga wa kuku ulioletwa na Mfugaji ili kutambua Magonjwa yaliyo sababisha vifo vya kuku wake alipotembelea banda la TVLA lililopo kwenye maonesho Nanenane yanayoendelea katika uwanja wa Nyamhongolo uliopo Mkoa wa Mwanza Agosti 5, 2023.
Fundi Sanifu Maabara Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA bwana Ally Fussah akitoa elimu kwa wadau wa mifugo waliotembelea banda la TVLA kujifunza namna ya kuwadhibiti wadudu aina ya Mbung'o wanaobeba vimelea vinavyosababisha ugonjwa wa Nagana Kwa mifugo na malale kwa binadamu kwa kutumia vitambaa vyenye dawa kwenye maonesho ya Kimataifa ya Nanenane yanayoendelea katika uwanja wa John kwenye Mwakangale Mkoa wa Mbeya Agosti 5, 2023.
Social Plugin