Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CDC, AMREF HEALTH AFRICA TANZANIA WAKABIDHI VIFAA VYA UTAMBUZI WA VIDOLE 'BIOMETRIC FINGERPRINT' MIKOA YA MARA & SIMIYU



Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (The U.S. Center for Disease Control -CDC) kupitia Shirika la Amref Health Africa Tanzania kwa ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) kimetoa msaada wa vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) katika mkoa wa Mara na Simiyu kwa  ajili ya utunzaji sahihi wa takwimu kwa kuondoa makosa na urudiaji wa usajili wa mteja pamoja na kutatua changamoto ya utambuzi wa kawaida wa wateja wapya na wa zamani wanaopata huduma katika vituo vya tiba na matunzo. 

Hafla fupi ya Makabidhiano ya vifaa vya utambuzi wa vidole ambayo pia imehudhuriwa na Mratibu wa PEPFAR Tanzania bi. Jessica Greene, Mkurugenzi Mkazi wa Kituo Cha Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (CDC) Tanzania Dk. Mahesh Swaminathan, Mkurugenzi Msaidizi wa CDC Tanzania
Dkt. George Mgomella, Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk. Florence Temu imefanyika leo Agosti 15,2023 katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara ambapo Mgeni rasmi alikuwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bw. Dominicus Lusasi.

Awali akizungumza, Mkurugezi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk. Florence Temu amesema vifaa hivyo vimenunuliwa kupitia Mradi wa Afya Kamilifu unaotekelezwa na Amref Health Africa Tanzania kwa ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI - The U.S. President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR) kupitia Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (The U.S. Center for Disease Control -CDC)


“Kwa muongozo wa Wizara ya Afya (NACP), Amref Tanzania imenunua vifaa vya utambuzi wa vidole ( Biometric fingerprint) 155 vyenye thamani ya shilingi Milioni 25 kwa mkoa wa Mara ikiwa ni sehemu ya vifaa vya utambuzi 398 tulivyotoa kwa ajili ya Mikoa mitatu ya Tanga (vifaa vya utambuzi 108) na Simiyu (vifaa vya utambuzi 135)  ambapo vifaa vyote vya utambuzi 398 vina thamani ya dola za Marekani 20,000.7.

Pia tumetoa mafunzo kwa vitendo kwa viongozi wa Afya wa Mkoa na wilaya na wahudumu wa Afya kwa halmashauri zote juu ya matumizi ya utambuzi wa vidole kupitia mfadhili PEPFAR”,ameongeza Dk. Florence.
 Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk. Florence Temu.

“Hadi sasa hapa Mkoani Mara tangu tuanzishe huduma hii ya kutumia vifaa vya utambuzi wa vidole kwa watu wanaoishi na maambukizi ya VVU wanaopata huduma katika vituo vya tiba na matunzo tumeweza kusajili wateja  takribani 3000  kwa utambuzi wa vidole kati ya wateja 63,000 (6%) walio kwenye dawa . Kwa kipindi cha wiki mbili na wateja wote wanaendela na kutumia mfumo huu wa kisasa wa utambuzi wa vidole. Kwa mantiki hii, kupitia vifaa hivi vya kisasa kuna ufanisi mkubwa katika utambuzi wa wateja, utunzaji sahihi wa takwimu za wateja wa VVU katika kitengo cha Utunzaji na Matibabu ya Virusi Vya Ukimwi (Care and Treatment centre)”, ameongeza Dkt. Frolence.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bw. Dominicus Lusasi, ameipongeza Serikali ya Tanzania na mfadhili PEPFAR kupitia CDC Tanzania na mdau Amref Health Africa Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele katika kuboresha sekta ya afya kupitia miradi mbalimbali ya afya hapa nchini.


“Hivi karibuni tu PEPFAR ilikuwa inaadhimisha Miaka 20 ya uwepo na utekelezaji wa mfuko huko tangu kuanzishwa kwake na Tanzania ikiwa moja wa nchi inayonufaika na mfuko huo. Binafsi nawapongeza sana Kwa kujali maendeleo ya sekta ya afya kwa Manufaa ya wanajamii wote. Chini ya Ufadhili wa PEPFAR kupitia CDC Tanzania, Amref Tanzania imekuwa ikitekelza huduma za afya mkoani Mara”,amesema .
Mkurugenzi Mkazi wa Kituo Cha Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (CDC) Tanzania Dk. Mahesh Swaminathan (kushoto) akikabidhi vifaa vya utambuzi wa vidole kwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bw. Dominicus Lusasi 


Lusasi ameishukuru Amref Health Africa Tanzania kuendelea kuboresha mifumo ya takwimu na taarifa katika vituo vinavyopewa ufadhili wa PEPFAR kupitia CDC mfano Chini ya ufadhili wa PEPFAR, kupitia CDC Mradi umekuwa ukitoa msaada katika mkoa huo kama utunzaji wa takwimu (Data Management), Uchambuzi wa takwimu (Analysis,) na Utoaji wa Taarifa sahihi ( Reporting).

“Misaada mingine wanayotoa ni kuwajengea uwezo wataalamu wetu wa takwimu kupitia mafunzo ya darasani na vitendo katika maeneo ya kazi. (on Job training and Mentorship), Mradi unatoa usimamizi wa kuunga mkono (Supportive supervision) katika shughuli za tathmini na ufuatiliaji (M&E) ili kuboresha ubora wa takwimu. Pia Mradi unatoa mafunzo ya kazini (on Job training) kwa watumishi wa takwimu na watumishi wengine wa afya katika vituo vyetu na Mradi huu umetoa ajira kwa Data Clerks wapatao 110 kwa mkoa wa Mara”,amesema Kaimu Katibu Tawala.

Lusasi ametumia fursa hiyo kuwataka watumishi wa afya na watu wote watakaotumia vifaa hivyo wawe waaminifu na waadilifu wahakikishe wanavitunza na yeyote atakayeleta uzembe na kusababisha uharibifu au upotevu hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

 Mratibu wa PEPFAR Tanzania bi. Jessica Greene akikabidhi vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bw. Dominicus Lusasi (kulia) na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Boniphace Marwa  (kushoto)


Naye Mratibu wa PEPFAR Tanzania bi. Jessica Greene amesema Amref Tanzania inatoa huduma jumuishi za kina katika vituo na jamii kupitia CDC kwa ufadhili wa PEPFAR ili kuunga mkono malengo ya kimataifa juu ya mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI yaani UNAIDS 95-95-95 na imekuwa ikishirikiana na Wizara ya Afya na uongozi wa afya ngazi ya mkoa katika kuboresha shughuli za Tathmini na Ufatiliaji (M&E).

Mkurugenzi Mkazi wa Kituo Cha Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (CDC) Tanzania Dk. Mahesh Swaminathan amesema matumizi ya Biometric fingerprint yatasaidia sana kukabiliana na changamoto ya wateja kupotea katika huduma na kwamba ili kuhakikisha mfumo huo unafanikiwa watumishi wa afya wamepatiwa mafunzo ya namna ya kutumia mfumo huo vizuri.
Maboksi yenye vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint)

Mkurugenzi Msaidizi wa CDC Tanzania Dkt. George Mgomella amesema matumizi ya vifaa vya utambuzi wa vidole yatasaidia sana kuongeza usiri kwa wateja kwani sasa hawatatembea na kadi za utambuzi na wataweza kutumia huduma popote, na itarahisisha kujua idadi halisi ya wateja na kuondoa changamoto ya kwamba wateja wanapotea katika huduma endapo wataondoka kwenye kituo kimoja kwenda kituo kingine.


Amesema mfumo huo wa kisasa unalenga kuboresha mifumo ya upatikanaji wa taarifa katika vituo vya afya ili kuweza kusaidia katika kufanya maamuzi kwa hatua ya kituo hadi mkoani (Improved data ownership) Chini ya Ufadhili wa PEPFAR kupitia CDC Tanzania.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt. Zabron Masatu na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Boniphace Marwa ambaye pia mkoa wake umekabidhiwa vifaa vya utambuzi wa vidole ( Biometric fingerprint) wameishukuru Amref Tanzania kupitia CDC kwa ufadhili wa PEPFAR kwa kuwapatia vifaa hivyo kwani vitasaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa takwimu sahihi kwa ajili ya matokeo sahihi ili kuboresha huduma za afya.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi Mkazi wa Kituo Cha Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (CDC) Tanzania Dk. Mahesh Swaminathan (kushoto) akikabidhi vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bw. Dominicus Lusasi leo Jumanne Agosti 15,2023 katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mkazi wa Kituo Cha Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (CDC) Tanzania Dk. Mahesh Swaminathan (kushoto) akikabidhi vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bw. Dominicus Lusasi 
Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk. Florence Temu akikabidhi vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bw. Dominicus Lusasi (kulia).
Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk. Florence Temu akikabidhi vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bw. Dominicus Lusasi (kulia).
Mratibu wa PEPFAR Tanzania bi. Jessica Greene akikabidhi vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bw. Dominicus Lusasi (kulia) na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Boniphace Marwa  (kushoto)
Mkurugenzi Mkazi wa Kituo Cha Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (CDC) Tanzania Dk. Mahesh Swaminathan (kushoto) akikabidhi vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Boniphace Marwa ambaye pia mkoa wake umekabidhiwa vifaa vya utambuzi wa vidole.
Mkurugenzi Mkazi wa Kituo Cha Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (CDC) Tanzania Dk. Mahesh Swaminathan (kushoto) akikabidhi vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Boniphace Marwa ambaye pia mkoa wake umekabidhiwa vifaa vya utambuzi wa vidole.
Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk. Florence Temu akikabidhi vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Boniphace Marwa ambaye pia mkoa wake umekabidhiwa vifaa vya utambuzi wa vidole.
Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk. Florence Temu akikabidhi vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Boniphace Marwa ambaye pia mkoa wake umekabidhiwa vifaa vya utambuzi wa vidole.
Viongozi mbalimbali wakipata maelezo kuhusu matumizi ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kutoka kwa Afisa TEHAMA wa Amref Health Africa Tanzania Kawedi Mchomvu
Viongozi mbalimbali wakipata maelezo kuhusu matumizi ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kutoka kwa Afisa TEHAMA wa Amref Health Africa Tanzania Kawedi Mchomvu
 Afisa TEHAMA wa Amref Health Africa Tanzania Kawedi Mchomvu akionesha namna vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) vinavyofanya kazi
Viongozi mbalimbali wakipata maelezo kuhusu matumizi ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kutoka kwa Afisa TEHAMA wa Amref Health Africa Tanzania Kawedi Mchomvu
 Mkurugenzi Mkazi wa Kituo Cha Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (CDC) Tanzania Dk. Mahesh Swaminathan akielezea kuhusu vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint)
Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk. Florence Temu akielezea kuhusu vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint)
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bw. Dominicus Lusasi  akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kwa ajili ya mkoa wa Mara na Simiyu
Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk. Florence Temu akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kwa ajili ya mkoa wa Mara na Simiyu
Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk. Florence Temu akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kwa ajili ya mkoa wa Mara na Simiyu
 Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk. Florence Temu akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kwa ajili ya mkoa wa Mara na Simiyu
Mratibu wa PEPFAR Tanzania bi. Jessica Greene akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kwa ajili ya mkoa wa Mara na Simiyu
Mkurugenzi Mkazi wa Kituo Cha Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (CDC) Tanzania Dk. Mahesh Swaminathan akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kwa ajili ya mkoa wa Mara na Simiyu
 Mkurugenzi Msaidizi wa CDC Tanzania
Dkt. George Mgomella akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kwa ajili ya mkoa wa Mara na Simiyu
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Boniphace Marwa akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kwa ajili ya mkoa wa Mara na Simiyu
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt. Zabron Masatu akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kwa ajili ya mkoa wa Mara na Simiyu
Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk. Florence Temu, Mkurugenzi Mkazi wa Kituo Cha Kudhibiti Magonjwa Nchini Marekani (CDC) Tanzania Dk. Mahesh Swaminathan na Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk. Florence Temu  wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa vya utambuzi wa vidole (Biometric fingerprint) kwa ajili ya mkoa wa Mara na Simiyu
Picha za pamoja.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com