Na Dotto Kwilasa, Dodoma
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bahi na Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM- Taifa Donard Megitii amewataka Wafugaji wa kuku nchini kuongeza uzalishaji wenye tija Kwa kujifunza mbinu mpya kupitia Maonesho ya wakulima yanayoendelea .
Megitii ameeleza hayo Jijini Dodoma kwenye maonesho ya Nanenane na kueleza kuwa Sekta ya kuku ina nafasi kubwa katika kukuza uchumi wa Taifa na kuongeza kipato na fursa za ajira.
Amesema, Sekta hiyo husaidia Kwa kiasi kikubwa huhifadhi rasilimali za asili na kwamba vizazi vijavyo vitaendelea kufurahia urithi huo.
Sambamba na hayo ameeleza tathmini ya Sekta ya kuku Kwa ukanda wa kati kuwa,kwa mwaka 2022 Sekta hiyo ilikua kwa asilimia 5 ikilinganishwa na asilimia 4.2 kwa mwaka 2020 na kueleza kuwa lengo ni kufikia asilimia 9 kila mwaka.
"Ufugaji wa kuku Kwa ukanda wa kati upo Katika mfumo wa asili na kibiashara,mfumo wa asili huchangia zaidi ya asilimia 70 ya kuku wote wanaofugwa na hutoa nyama na mayai,ni jambo la jujivunia zaidi iwapo tutaongeza kasi zaidi,"amesisitiza
Pia ametumia nafasi hiyo kuwataka Maafisa ugani kwenda vijijini kutoa elimu juu ya ufugaji bora wenye tija kwa ajili ya manufaa ya mtu mmoja mmoja hata Taifa kwa ujumla.
Megitii amesema wafugaji wa vijijini bado wana shida ya wataalam na hivyo baadhi Yao kushindwa kufuga kwa tija na kuendelea kufuga kwa mazoea na kueleza kuwa huu ndo wakati mzuri wa kuwaelimisha wafugaji.
Social Plugin