WATU WAWILI WAJERUHIWA KWENYE AJALI YA BASI KAHAMA
Monday, August 21, 2023
Gari la abiria lenye namba T192 DBZ aina ya Scania Kampuni ya AM Safari linalofanya safari zake kutoka Kahama kuelekea Dodoma, limepata ajali eneo la Mizani mjini Kahama mkoani Shinyanga, huku chanzo ajali hiyo kikielezwa kuwa ni Mwendokasi ambapo dereva alishindwa kumudu kona ya kuingia eneo la Mizani.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa shinyanga ACP Janeth Magomi ameiambia MALUNDE 1 BLOG kuwa watu wawili wamejeruhiwa katika ajali hiyo na kukimbizwa katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama kwa ajili ya Matibabu zaidi.
Hata hivyo, Kamanda Magomi amesema licha ya uzembe wa Dereva lakini pia gari hilo ni bovu na limezuiliwa kuendelea kutoa huduma, huku akiwataka Wamiliki na Wasafirishaji kuzingatia Sheria za Usalama barabarani ikiwemo kuhakiki Magari yao kabla ya kuanza safari.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin