WAZIRI KIJAJI ATAKA VIWANDA VYOTE NCHINI KUTENGENEZA BIDHAA ZENYE UBORA


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb) ametaka viwanda vyote nchini kutengeneza bidhaa zenye ubora kwa gharama nafuu ili ziweze kuingia katika soko Eneo huru la biashara Afrika (AfCFTA).

Waziri Kijaji ameyasema hayo alipotembea Kiwanda cha kuzalisha Maziwa cha Tanga Fresh kilichopo jijini Tanga kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji wa maziwa na kusikiliza na kutatua changamoto walizonazo.

Aidha amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inafanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha wafanyabiashara na wawekezaji wanakuwa na mazingira bora na wezeshi ili kufanya biashara kwa tija na kukuza uchumi wa Taifa.

Vilevile amesema Serikali ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Tanzania nikuona wafugaji wanabadilika kutoka katika ufugaji wa kienyeji kwenda katika uwekezaji wa kisasa ili kukidhi mahitaji ya soko.

Aidha amepongeza kiwanda hicho kwa ajira walizotoa hapa nchini na ametaka ajira zisizo za moja kwa moja ziongezeke.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post