WAZIRI KIJAJI:ATAKAYEUZA SUKARI ZAIDI YA 3200 ACHUKULIWE HATUA




Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) awataka Maafisa Biashara wote nchini kukagua bei ya Sukari duka kwa duka na atakae kutwa na bei zaidi ya shilingi 3,200 achukuliwe hatua za kisheria.

Waziri Kijaji ameyasema hayo alipotembelea Kiwanda cha kuzalisha Sukari cha TPC Mkoani Kilimanjaro kujionea shughuli za uzalishaji na kisikiliza changamoto walizonazo.

Dkt. Kijaji amesema ni jukumu la Maafisa Biashara kutambua mfanyabiashara yeyote atakayeuza sukari juu ya bei kati ya 2800 na 3200 kumchukulia hatua.

Dkt. Kijaji amesisitiza kiwa ni jukumu la Serikali kulinda bidhaa yoyote inayotengenezwa nchini na kufanya Juhudi za kila namna ili kuweza kuwasaidia wawekezaji na wafanyabiashara kuwa na mazingira bora na wezeshi ili kukuza biashara zao na kiwa na tija.

Aidha, amesema bidhaa zinazotengenezwa nchinj zinatakiwa kuwanufaisha wawekezaji na wafanyabiashara wa ndani na biashara yoyotee inayofanyika nje ya nchi inatakiwa kuwa rasmi.

Vilevile amekipongeza Kiwanda cha kuzalisha Sukari cha TPC kwa kutoa ajira zaidi ya elfu 3200 na jinsi kinavojihusisha na utoaji wa huduma kwa jamii inayokizunguka

Naye Kaimu Afisa Mtendaji Utawala wa Kiwanda cha TPC, David Shiltu amesihi watanzania kuwa na Amani kwa kuwa sukari ipo sokoni ya kutosha na hakuna uhaba na uzalishaji unaendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post