Na Nyabaganga Daudi Taraba
Mada zilizowasilishwa ni kama ifutavyo:
Mada ya 1 ni AIM for Climate, lengo ni kuhusu tabianchi: Kuwekeza katika ubunifu kwenye masuala ya mabadiliko ya tabianchi, yakilenga zaidi kuongozwa na wanawake.
Muandaaji wa mada ni USAID.
Mada inasisitiza juu ya uvumbuzi katika masuala ya tabianchi, mabadiliko ya tabianchi na ukosefu wa chakula kimataifa, kuunganisha washiriki katika kuongeza uwekezaji katika utafiti na uendelezaji katika kilimo janja na ubunifu katika mifumo ya usalama wa chakula. Aidha, imelenga kuelimisha washiriki kuhusu namna wanavyoweza kushirikiana ili kuongeza uwekezaji utakaowanufaisha wakulima wadogo hususan mwanamke.
Wazungumzaji katika mada hiyo walikuwa ni kutoka USAID, CGIAR na wengine ni CAN/CGIAR, Bill & Melinda Gates Foundation, Corteva Agriscience na Mkulima.
Mada ya 2 ni Uzinduzi wa agenda ya mabadiliko katika mfumo wa kilimo Tanzania.
Mada hii imejikita katika kueleza hali halisi ya sekta ya kilimo na kwa namna gani mabadiliko ya mfumo yalivyoinua juhudi za serikali katika sekta ya kilimo.
Kutoa hamasa kwa washiriki kuhusu juhudi za Tanzania katika kufanya mabadiliko ya kuimarisha taasisi zake na kuhusisha sekta binafsi katika sekta ya kilimo.
Kuboresha mfumo wa kupata elimu kuhusiana na sekta ya kilimo, changamoto na njia za kupambana na mabadiliko ya tabianchi katika kilimo, pia elimu imetolewa kuhusu umuhimu wa kuunganisha mambo ya mabadiliko ya tabianchi na njia za kutatua changamoto hiyo.
Wazungumzaji walikuwa ni Mhe. Hussein Bashe (Waziri wa Kilimo-Tanzania) na Safia Boly (Mkurugenzi wa African Agricultural Transformation Initiative). Ukumbi uliotumika ni wa Serena Hotel.
Mada ya 3 ni Uzinduzi wa CALA Leadership Forum III, Integrating Youth in Africa’s Food Systems Transformation CALA AGRA.
Mada ya 4 ni Kuongeza upatikanaji wa rasilimali ndani ya nchi.
Tukio lilizungumzia programu ya G4G ya nchini Ghana na programu ya Farmfit TA ya nchini Tanzania, kama sehemu ya ukuaji endelevu barani Afrika (GSA), ikiwa ni mifano jinsi ya kuunganisha mifumo mbalimbali na wanunuaji, watoa huduma, wajasiriamali wadogo na wakubwa na wadau wengine, katika kuhuisha mnyororo wa upatikanaji wa nafaka na kuinua biashara za kilimo nchini Ghana na Tanzania.
Mada imetolewa na wawakilishi kutoka Ghana (IDH) na Tanzania
Mada ya 5 ni Kuyapa mazao jamii ya mikunde/maharage umuhimu katika lishe bora na mazao vumilivu kuyajumuisha katika mifumo ya usalama wa chakula.
Mada imeongozwa na WorldVeg, yenye uzoefu wa miaka 50 ya utafiti na uendelezaji.
Kamati ya wataalam washiriki kwenye mjadala wameulizwa maswali na kutoa ufafanuzi. Wameainisha umuhimu wa mboga za majani na maharage kwa wanawake na vijana, na wamependekeza hatua madhubuti za kipaumbele za kuchukuwa dhidi ya suala hili.
Wazungumzaji ni kutoka WorldVeg na CGIAR.
Madaya 6 ni Mifumo ya Kilimo kwa Vijana: Fursa na Changamoto
Imeandaliwa na FAO, CGIAR GENDER IMPACT PLATFORM, SACAU, AGRA.
Yaliyojili katika mada hii ni: kuimarisha juhudi za vijana zenye tija barani Afrika, zinazozingatia mabadiliko ya tabianchi, jinsia na ujasiriamali endelevu, pamoja na kuandaa programu muhimu zinazowezesha vijana wa Afrika kuongoza mabadiliko katika kilimo barani Afrika. Pamoja na kutafiti nguvu ya vijana na wanawake kuweka mitandao ya kuweza kusogeza mbele hatima na ndoto za vijana na wanawake katika kilimo.
Mada ya 7 ni kuwekeza kwa wanawake-juhudi za mpango wa AECF kuunga mkono mabadiliko ya wanawake katika kilimo.
Imeandaliwa na AECF.
Katika muda wa miaka minne, AECF imewekeza katika mpango mahsusi unaolenga wanawake kwenye kilimo janja, kwa kutoa fedha kwa wakulima wadogo na vikundi vingine vya kiuchumi vya wanawake.
Mada ilibainisha uwekezaji kwa wanawake, na kubaini sababu za kutoa msaada kwa wanawake, na sababu za wanaume kuunga mkono juhudi za kutoa misaada kwa wanawake.
Wazungumzaji wakuu walikua ni kutoka AECT na mwakilishi mmoja wa wanawake .
Mada ya 8 ni Kufadhili Kampuni za Mbegu.
Mada iliandaliwa na CESSA.
Mad ya 9 ni Kufadhili Vikundi vya Wakulima kwa ajili ya uhimulivu wa chakula.
Waandaaji ni IFAD, SAFIN, AFEX.
Tukio lililenga kujadili changamoto wanazopata vikundi vya wakulima (FOs) barani Afrika katika kupata misaada ya kifedha kwa ajili ya kilimo, kwa kuzingatia changamoto za UKIMWI, vita ya Ukraine na mabadiliko ya tabianchi. Tukio lilijikita katika kutafiti namna mpya za ushirikiano baina ya sekta binafsi kutoa fedha kwa FOs. Lengo kuu likiwa ni kuja na fursa thabiti zinazovutia wafadhili kutoa fedha kwa FOs, hivyo kuwezesha uhimilivu katika kilimo katikati ya changamoto zilizopo.
Wazungumzaji walikuwa ni kutoka AFEX, IFAD, AAACO, Equity Bank na TAHA Group.
Mada ya 10 ni vipaumbele katika Sera na mnyororo wa thamani katika ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi. Waandaji ni RENAPRI.
PPVC ni progamu ambayo inazingatia soko na imepangwa kwa awamu. Imesisitiza kuwa serikali ziwe na viipaumbele katika sera za kilimo, zinazozingatia ubora wa bidhaa na minyororo ya thamani.
Wazungumzaji walikuwa ni kutoka SUA, Tegemeo Institute of Agricultural Policy and Development, Egerton University, Kenya, Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA), Sunflower Value Chain, Qstek Farm Limited – Tanzania, Institute of Statistical, Social and Economic Research, University of Ghana, Bill & Melinda Gates Foundation na ReNAPARI
Mada ya 11ni Kutoka shambani hadi kwa mtumiaji: namna ya kuwezesha ajira kwa vijana na fursa za ujasiriamali ndani ya mifumo ya usalama wa chakula barani Afrika.
Waandaaji ni Mastercard Foundation.
Mada hii ilisimamiwa na kundi la vijana wenye fani na kutoka jamii mbalimbali, wanaoangalia mifumo ya sasa na ile ijayo kuhusu kilimo. Viongozi wa vijana watashirikishana kuhusu uzoefu waliopata kupitia mbinu mbalimbali.
Mapendekezo yaliyowasilishwa yalipatikana kutoka kwenye mitazamo shirikishi. Lengo la mada ni kuunganisha elimu kati ya vijana na viongozi wanaotoa maamuzi.
Walioongoza majadiliano ni kuoka Ghana society for the Physically Disabled (GSPD) and Ghana Federation for Disabled (GFD), West Gonja Municipal; Advocacy and Capacity Development Consultant, YPARD ya Mali na Novelle Generation limited.
Madaya 12 ni Jukumu la Sayansi katika kuharakisha Biashara Kilimo kwa kuzingatia mabadiliko ya tabianchi kwa kilimo, uhimilivu, jinsia na uhusishaji wa jamii yote kwa ujumla.
Waandaaji ni kutoka CIAT, AECF, 2SCALE na Women Investment Club (WIC).
Mada ilihusu jukumu la msingi la sayansi na tafiti katika kuharakisha uwekezaji katika kilimo janja na mabadiliko ya tabianchi (CSA) na jinsi ya kutoa msaada wa kiufundi kwa kuzingatia utayari katika uwekezaji. Uzoefu wa vijana na wanawake kutoka nchi za Senegal, Zambia na Kenya ulijadiliwa.
Wazungumzaji walikuwa ni kutoka Venture building & Investment Specialist, Alliance Bioversity International & CIAT, CGIAR’s Ukama Ustawi Regional Integrated Initiative for East and Southern Africa, AICCRA Zambia Cluster Lead, South Africa Representative, International Water Management Institute (IMWI), AECF, East and Southern Africa, 2SCALE, Women’s Investment Club, Senegal, Afri-Farmers Market and GIE Diallo Tiama.
Mada ya 13 ni Kuwezesha mitaji kwa vijana.
Waandaji ni Heifer International.
Afrika inaongoza kwa kuwa na vijana wengi duniani, ambapo zaidi ya 80% ya watu wana umri chini ya miaka 35. Ifikapo 2055, idadi ya vijana itakuwa mara dufu. Pamoja na fursa zilizopo kwenye kilimo, ushiriki wa vijana bado ni mdogo. Aidha mada hiyo imeongelea uwezeshaji na upatikanaji wa mtaji kwa vijana, hususan fedha, unavyoweza kutoa fursa kwenye kilimo kwa wakulima wadogo.
Wazungumzaji ni kutoka Soupah Farm-En-Market, Ltd, Heifer International, Sub Saharan Africa, Mastercard, AfDB, Mhe. Abdallah Ulega (Mb), Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Tanzania, Thrive Agric (AYuTe Regional Winner 2022 West Africa).
Mada ya 14 ni Mabadiliko katika Mifumo ya usalama wa chakula: Kusaidia uongozi wa serikali katika njia za utekelezaji.
Waandaddji ni GAIN, ACT4Food na Akademiya2063.
Ni uzoefu kutoka UNFSS ili kuona jinsi ya kutoa misaada kwa serikali kwa ajili ya kuharakisha utekelezaji wa mipango ya nchi mbalimbali.
Wazungumzaji ni kutoka Food Systems Coordination, IFAD, GAIN, GAIN Tanzania, National Convenor, United Republic of Tanzania, TBC kutoka Nigeria/Kenya, Policy and Advocacy, AGRA, USAID, GBRI Ltd na Akademiya 2063.
Mada ya 15 ni Azimio la Malabo kuhusu Kilimo barani Afrika: Kuunganisha nguvu kati ya watoa maamuzi na wadau ili kuharakisha utekelezaji.
Waandaaji ni Chuo cha Mali Asili, Chuo Kikuu cha Greenwich, United Kingdom, AGRA.
Wakuu wa nnchi na Serikali waliafikiana na azimio la Malabo la 2014, la kuwezesha kuwa na ukuaji endelevu, ambao unaboresha maisha ya watu, na lishe, usalama wa chakula na uhimilivu. Hiyo ilijengeka kutoka kwenye Programu ya Afrika kuhusu kilimo kabambe ambayo imeweka malengo mahsusi. Japokuwa baadhi ya nchi zimepata maendeleo kiasi kwenye malengo ya azimio la Malabo, bado kunahitajika juhudi kubwa ili kuharakisha utekelezaji wake. Lengo kuu la mada ni kujadili ili kufikia namna bora ya kufanya mabadiliko katika mifumo ya usalama wa chakula katika kilimo Kiafrika.
Wazungumzaji ni kutoka University of Greenwich, Umoja wa Afrika, Mhe. (Dr) Godfred Jasaw, Mbunge na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Bunge la Ghana, MVIWATA na Policy and State Capability.
Mada ya 16 ni Ukuaji wa Maendeleo Vijijini katika hali tete.
Muandaaji ni IFAD.
Mada iliongelea ushirikiano kwenye biashara binafsi ili kuboresha uhimilivu kwenye kilimo katika mazingira tete, na kujifunza uzoefu kutoka AfDB mazingira tete na jinsi ya kuyatumia katika mazingira halisi ya kila nchi.
Wazungumzaji walikuwa ni kutoka Sekta binafsi ya Somalia, Sudan ya Kusini, WCA na IFAD.
Mada ya 17 ni Ajira: Changamoto na fursa kwenye maisha ya vijijini katika mifumo ya usalama wa chakula.
Waandaaji ni EAT Foundation, IKEA Foundation, Just Rural Transition na Food Systems Economics Commission.
Maisha ya takriban watu bilioni moja yanategemea kilimo barani Afrika, japo mara nyingi wakulima wanakutana na tatizo la ukosefu wa chakula na mazingira magumu ya kilimo. Mada hii imejadili kwa kina hali iliyopo na kubaini tafiti zilizofanyika kutokana na uzinduzi wa Food System Economics Commission’s Policy Brief on Africa, ikiangazia upatikanaji wa ajira. Washiriki wamejadi pia kuhusu sera na mifano bora ya utekelezaji.
Wazungumzaji ni kutoka Food Program at the World Resources Institute (WRI) na Global Alliance for Improved Nutrition (GAIN).
Mada ya 18 ni Sera zenye mitazamo ya Kijinsia: AWARD, African Food Changemakers
Ripoti mpya ya FAO (2023) inayotoa picha kamili kuhusu hali ya kuhusika kwa wanawake katika kilimo imeonesha kuwa japo kuna maendeleo kidogo, kwa kiwango kikubwa hakuna usawa katika mifumo ya kilimo katika mtazamo wa kijinsia na majukumu ya mifumo ya kijinsia kuhusiana na kilimo, na kupendekeza kuhusu maboresho.
Wazungumzaji walikuwa ni kutoka CGIAR GENDER Impact Platform, AWARD, FAO, AGRA, USAID PolicyLink Program, Sahel Consulting: Agriculture & Nutrition Ltd, National Nutritional Consultant, Buttercup Farmhouse, For Food’s Sake Eat na The Atije Experience.
Mada ya 19 ni Kubaini Mbolea kutoka Afrika na Maono kuhusu Afya ya Udongo.
Waandaaji ni kutok AAP, CIFOR/ICRAF, CGIAR, AGRA, AFAP, IITA na GiZ.
Mada ilihusu mapendekezo ya nini kifanyike kuhusu afya ya udongo barani Afrika na mahitaji ya mbolea. Kuzorota kwa afya ya udongo ni changamoto barani Afrika na ikiwa ni pamoja na uwepo wa tija.
Wazungumzaji ni kutoka AFAP, Waziri wa Kilimo wa Tanzania (Mhe. Hussein Bashe), TARI, Climate and Soil Fertility, AGRA, International Institute of Tropical Agriculture (IITA), CIMMYT, SafiOrganics Ltd, SAGCOT (Tanzania), AFAP na Mkulima.
Mada ya 20 ni kuhusu Bajet Janja kuhusu Mabadiliko katika mifumo ya Kilimo.
Waandaaji wa mada ni USDA na FAO.
Tukio hili lilihusisha uzinduzi wa ushirikiano mpya kati ya AIM na FAO, kwenye ufuatiliaji na uchambuzi wa Programu ya sera za chakula na kilimo, inayoweka mkazo kwenye sera bora zinazozingatia utatuzi wa changamoto za tabianchi na upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kilimo.
Wazungumzaji walikuwa ni kutoka FAO, USDA, Bill & Melinda Gates Foundation, Serikali za Morocco, Ghana na Msumbiji.
Mada ya 21 ni kuhusu utoaji wa misaada kwa wakulima wadogo kwa ajili ya kilimo chenye tija na himilivu, kupitia uwekezaji, habari na ubunifu.
Waandaaji ni kutoka AAAP, CABI Virginia Tech.
Kulingana na uchambuzi wa wadau mbalimbali, ukuaji wa tija katika kilimo unashuka katika nchi zilizo chini ya jangwa la Sahara, ambayo ni changamoto kubwa katika kilimo.
Lengo la mada hii ni kuweka hatua za uwekezaji, biashara kilimo na muelekeo wa serikali katika kuongeza tija kwenye kilimo.
Wazungumzaji walikuwa ni kutoka Strategic Partnerships, Africa, CABI, Global Agricultural Productivity Report, Virginia Tech, Food Security & Rural Wellbeing, Global Center on Adaptation na AgriTech Analytics.
Mada ya 23 inahusu Gharama Halisi ya Usalama wa Chakula.
Muandaji wa mada ni AFEX.
Lengo la mada ni kuchambua changamoto kuhusu masuala yanayozingira usalama wa chakula, ikiwa ni pamoja na mnyororo wa thamani ili kuwezesha upatikanaji wa ubunifu na ufumbuzi endelevu.
Wazungumzaji ni kutoka Program Innovation and Delivery, AGRA, IFAD na AFEX.
Mada ya 24 ni Mabadiliko katika mifumo ya usalama wa chakula ya Kiafrika: Ushirikiano, Kuaminiana na Upatikanaji wa Takwimu na Taarifa za Kilimo kwa Wakati.
Waandaji wa mada ni USDA, AKADEMIYA2063 na AGRA.
Mifumo ya usalama wa chakula ya Kiafrika ni muhimu katika uchumi wa kitaifa, maisha na lishe. Mada ilihusu mabadiliko katika mifumo mbalimbali ili kuhakikisha chakula bora, ukuaji wa uchumi na usalama wa mazingira.
Wazungumzaji ni kutoka USDA, Marketing, Trade and Regulatory Programs, AU, AKADEMIYA2063 na AGRA.
Mada ya 25 ilihusu uendelezaji wa ujumuishi wa jamii katika usalama wa chakula, je ni picha halisi ?
Waandaaji ni kutoka FOLU, AGRA, WRI, GAIN Practical Action (PA), Micro Enterprise Support Program Trust (MESPT) na Tanager.
Lengo la mada ni kujua endapo vijana wako tayari kuongoza mabadiliko katika mifumo ya usalama wa chakula na kama wadau wengine wako tayari kushiriki kwenye midahalo na mijadala kuhusu mabadiliko hayo.
Wazungumzaji ni kutoka GAIN, Sahel Consulting, FOLU na mkulima.
Pamoja na mada hizi, pia kuna mada za ufugaji zimejadiliwa.
Ndugu msomaji na mfuatiliaji wa mkutano huu, nikwambie kwamba Dar es Salaam kumenoga na mambo ni bambam, maonesho nayo yanaendelea kwa uzuri kabisa. Nitaendelea kukujuza yatakayojili katika mkutano huo nawe utakuwa kama ulikuwepo maana kila tukio tutakujuza. Usikose kutembelea tovuti ya Wizara ya Kilimo www.kilimo@go.tz
Social Plugin