MADA ZA AGRF 2023 ZILIZOJADILIWA SEPTEMBA 6

 

MADA ZA AGRF 2023 ZILIZOJADILIWA KATIKA KUMBI MBALIMBALI ZA JULIUS NYERERE, DAR ES SALAAM, TAREHE 6 SEPTEMBA 2023

 

Mada tofauti ziliendelea kujadiliwa katika kumbi mbalimbali zilizopo kwenye maeneo ya ukumbi mkubwa wa Kimataifa ya Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

Mada ya 1 ilikuwa ya Kushawishi Washirika wa Maendeleo Kuchangia Katika Mpango wa Tanzania wa BBT

Programu ya Tanzania ya Jenga Kesho Bora (Build Better Tomorrow-BBT) kuhusu mifumo ya uzalishaji chakula ni programu yenye ubora wa hali ya juu, ambayo inauzika. Lengo mahsusi la mada hii lilikuwa ni kujadili programu zilizofanikiwa za mfano, kupitia BBT. Aidha mada ililenga kuhamasisha washirika wa maendeleo kuunga mkono serikali ya Tanzania katika programu hiyo na kuchangia fedha ili itekelezwe na kutengeneza fursa ya ajira kwa vijana katika mifumo ya uzalishaji wa chakula.

Wazungumzaji walikuwa ni pamoja na Waziri wa Kilimo Tanzania (Mhe. Hussein Mohamed Bashe), Waziri wa Mifugo na Uvuvi Tanzania (Mhe. Abdallah Ulega), Mwenyekiti Mwenza wa President’s Agricultural Committee (Hailemariam Dessalegn).

Wazungumzaji wengine walikuwa ni pamoja na Waziri wa Fedha wa Tanzania (Mhe. Mwigulu Nchemba), Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania (Mhe. Ashatu Kijaji), Head of MDBs, UN agencies, IFAD, Bilateral & Multilateral organizations (World Bank, AfDB, IsDB, USAID, NORAD, BMZ, FCDO, BMGF), wakilishi wa sekta binafsi, wawekezaji (Mohammed Industries, Vodacom, NMB, SouthBridge Investment, ETG, Brewers and Bottling Companies, Seed Companies, Millers including Bakhresa etc.) na Dr. Victoria Kwakwa, Makamu wa Rais wa Afrika Mshariki na Kusini wa Benki ya Dunia.

Wengine ni kutoka Youth & Women Civil Society and Farmer Organisations Representatives, na Dr. Abou Bamba, mshauri katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Abdijan Legacy Program, Cote dIvoire.

 

Mada ya 2 ni Good Morning AGRF.

 

Mada hii ni ya kila siku asubuhi wakati wa kuanza vikao. Huonesha kwa kifupi yaliyojiri siku iliyotangulia na yatakayojiri siku hiyo.

 

Waandaaji  ni Ms. Jolenta Joseph wa Tanzania, Bwana John Agboola kutoka Nigeria na Ms. Wangari Kuria kutoka Kenya.

 

Wazungumzaji walikuwa ni Lenzie Mills na AfDB.

 

Mada ya 3 ilihusu Mageuzi Katika Mifumo ya Uzalishaji Chakula Barani Afrika kwa Manufaa ya Lishe Bora.

 

Mada hii ilijadili masuala tete kuhusu mifumo ya uzalishaji chakula, lishe bora, afya ya binadamu, mazao himilivu, uzalishaji wa chakula ulio endelevu, yote yakilenga kufanya mageuzi katika mifumo ya uzalishaji chakula iliyopo. Aidha, ilijadili kuhusu hali (status) ya wanawake katika uzalishaji wa chakula, hali ya lishe bora na milo endelevu.

 

Wazungumzaji walikuwa ni Waziri wa Afya wa Ethiopia (Mhe. Dr. Lia Tadesse), Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Canada (Mhe. Mélanie Joly), Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway (Mhe. Anne Beathe Tvinnereim) na Waziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Sudan ya Kusini (Josephine Joseph Lagu).

Wengine ni Mhe. Mariam Mwinyi, Mke wa Rais Wa Zanzibar, na wake wa marais wengine mbalimbali.

Aidha, wazungumzaji wengine walikuwa ni kutoka FAO, Msanii, Mwanasiasa na mkulima kutoka Ghana (John Dumelo), Heifer International, Kwanza Tukule, Policy and Advocacy Officer; Regional Coordinator, Africa, CARE International, Rockefeller Foundation, na Ethiopia International Livestock Institute,

 

Mada ya 4 ilihusu Fedha za Kilimo kwa Hali ya Hewa Kuanzia Mpango Hadi Tathmini ya Utekelezaji.

 

Waandaji ni SAFI na UNEP

 

Mada hii ililenga zaidi wawekezaji, wasimamizi wa fedha zinazotolewa kwa ajili ya kilimo, taasisi za fedha na wadau wengine wanaojihusisha na kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia mabadiliko ya tabianchi yanavyoathiri kilimo.

Mada ilijadili mipango, usimamizi na tathmini ya juhudi zinazofanywa na taasisi zilizojikita kwenye kutoa fedha kwa ajili ya mabadiliko ya tabianhi kwenye kilimo.

Wazungumzaji walikuwa ni kutoka SAFIN, IFAD na UNEP.

 

Mada ya 5 ni kuhusu Pitch AgriHack.

Mada hii ina lengo la kuhamasisha vijana barani Afrika kufanya mageuzi katika kilimo kwa kutumia Teknolojia ya Habari (ICT).

 

Mashindano hutumika kama njia ya kuhamasisha na kuharakisha matumizi ya ICT katika kilimo. Mashindano yatabainisha na kukuza juhudi zinazotumiwa na vijana katika kilimo, ikiwa ni pamoja na ubunifu na digital agriculture.

 

Wazungumzaji walikuwa ni kutoka MasterCard Foundation, Feronia, Telus Agriculture & Consumer Goods (Muddy Boots), Heifer International, Policy Research Institutes (ReNAPRI), AL for Agribusiness Network, African Leadership Academy, Climate Smart Agriculture (World Bank), Mastercard Foundation na Digital Agriculture.

 

Mada ya 6 ilikuwa kuhusu Gharama ya Chakula Bora.

 

Mada hii ilijadili gharama ya chakula bora. Mjadala ulijkita kwenye kuangalia uhusiano kati ya bei ya vyakula, uchaguzi wa vyakula na matokeo kwenye afya ya watu. Mada ilijadili pia kuhusu changamoto zinazozingira ulaji wa chakula bora na kutoa mapendekezo.

 

Wazungumzaji walikuwa ni pamoja na Waziri wa Kilimo wa Zambia na Waziri wa Afya wa Tanzania (Mhe. Ummy Mwaalimu).

Wengine walikuwa ni kutoka Agricultural Development, Bill & Melinda Gates Foundation (BMGF), Pure and Just Co ya Ghana, Policy and Advocacy One Thousand Days, Center for Development Research, Bonn University, Southern African Confederation of Agricultural Unions, AKM Glitters Company ya Tanzania, Family Health and Sun, Syngeta Foundation, WHO na Umoja wa Mataifa.

 

Mada ya 7 ilihusu Biashara na Uwekezaji.

 

Mada hii ilijadili masuala ya biashara na uwekezaji. Viongozi wa ngazi za juu wa serikali mbalimbali walijadili kuhusu mahitaji ya mabadiliko katika sera na misaada hitajika ili kuwa na mazingira rafiki katika mabadiliko katika mifumo ya uzalishaji chakula, ikiwa ni pamoja na mabadiliko katika sera za uwekezaji.

Wazungumzaji walikuwa ni Waziri wa Biashara wa Niger, Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania (Mhe. Ashatu Kijaji), Waziri wa Uwekezaji wa Togo (Mhe. Rose Kayi Mivedor), Waziri wa Biashara wa Benin (Mhe. Shadiya Alimatou Assouman).

Wengine walikuwa ni kutoka East African Breweries, Kenya, Africa Improved Foods, Rwanda, WARC, Ghana, Syngenta Foundation, United States Agency for International Development (USAID), Makamu wa Rais wa Millennium Challenge (Ms. Aysha House) na Regional Food Trade & Resilience - Policy & State Capability.

 

Mada ya 8 ilikuwa ni African Women Leaders Forum and WAYA Awards.

 

Mada hii ilijikita kwenye kuhamasisha na kuendeleza uongozi wa wanawake katika mifumo ya uzalishaji chakula barani Afrika. Ilijadili namna African Women Leaders Forum ni jukwaa la kuhimiza na kuendeleza wanawake kuwa katika uongozi wa masuala ya kilimo.

 

Wazungumzaji walikuwa ni Waziri wa Maendeleo Jamii, Jinsia, Wanawake, na Makundi Maalum wa Tanzania (Mhe. Dr. Dorothy Gwajima), na kutoka Africa Growth Initiative, Brookings Institution, Ayavuna Women’s Investments, Global Agriculture Practice, World Bank, East and Southern Africa Division, International Fund for Agricultural Development (IFAD), Sahel Consulting.

 

Mada ya 9 ni kuhusu Usalama wa Chakula na Usimamizi Baada ya Uvunaji.

 

Lengo la mada hii lilikuwa ni kujadili chakula baada ya mavuno. Tabia za usimamizi wa chakula baada ya mavuno ni muhimu sana kutokana na upungufu wa chakula mara kwa mara katika nchi mbalimbali. Mada ilijadili changamoto zilizopo na kushirikishana uzoefu kutoka nchi mbalimbali.

Wazungumzaji walikuwa ni kutoka FAO, COMESA, Agriculture and Rural Development AUC, Partners in Food Solutions, Codex Alimentarius Commission, Uganda National Bureau of Standards, NAMPAK, WTO, East African Community, PACA, United States Department of Agriculture (USDA), WB, Wizara ya Biashara, Uwekezaji na Viwanda Kenya, Eastern Africa Grains Council, World Vegetable Centre, Global Farmer Network na Green Climate Fund (GCF).

 

Mada ya 10 ni Mifumo ya Uzalishaji Chakula wakati wa Hali tete: Wahamiaji Vijana na Waliohamishwa kama moja ya Ufumbuzi.

 

Lengo la mada lilikuwa ni kujadili uzoefu kuhusu uhusika wa vijana wahamiaji katika mifumo ya uzalishaji chakula katika nchi mbalimbali.

Wazungumzaji walikuwa ni Waziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Sudan ya Kusini (Mhe. Josephine Joseph Lagu) na kutoka Akademiya 2063, International Committee for Red Cross na World Food Programme (WFP).

Wengine ni kutoka Resilience and Food Security (RFS) at USAID, Feed the Future Deputy Coordinator for Development, Youth Ambassador, Generation Africa, International Union for Conservation of Nature (IUCN), UN Environment Programme (UNEP), IFAD, CODIG na UNDP.

 

Mada ya 11 ilihusu Matokeo ya Kilimo katika Jamii (Soial Impact)

Mada hii ilijadili nguvu ya kilimo katika kuleta mabadiliko katika jamii na kutatua changamoto zinazowakabili. Mada ililenga kuhamasisha jamii na wajasiriamali wa kilimo kuwa wabunifu katika kilimobiashara.

Wazungumzaji walikuwa ni pamoja na kutoka Africa Enterprise Challenge Fund, Heifer International, MAYA ya Mali na Women in Africa ya Cameroon.

 

Mada ya 12 ilikuwa ni Program & Innovatiion: Regenerative Agriculture and Resilient Food Systems

 

Lengo la mada lilikuwa ni kubaini mifumo ya uzalishaji chakula ambayo inaweza kuhimili mabadiliko ya tabianchi na mazingira. Hii ni pamoja na kuzingatia uzoefu kutoka nchi mbalimbali.

 

Wazungumzaji walikuwa ni kutoka Rural Development, Food Security, Nutrition, European Commission’s department for International Partnerships, Governor of Embu County, Kenya, East Africa Farmers Federation (EAFF), National University of Sciences, Technologies, Engineering and Mathematics (UNSTIM), Benin, East Africa Business Lead, D-Olivette Enterprise, Nigeria, Rockland Farms, Ghana, SVP Technologies and Crops, Netafim, Israel, Rockland Farms ya Ghana, SNV, Rockefeller Foundation, Agri Innovation Hub, Keny na Land O’Lakes USA.

 

Mada ya 13 ilikuwa ya Majadiliano Mepesi ya Watu Binafsi Kufahamiana kwa Karibu.

 

Mada hii ilikuwa ya watu binafsi kufahamiana kwa karibu (social networking) pamoja na kuburudika kwa vinywaji laini na mziki mwororo kumalizia siku.

 

 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post