Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MADA ZILIZOJADILIWA SAMBAMBA NA UZINDUZI WA AGRF 2023


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika kwa Mwaka 2023(AGRF) katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es salaam. Tarehe 05 Septemba 2023
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizindua ripoti ya hali ya kilimo Barani Afrika ya Mwaka 2023 wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika kwa Mwaka 2023(AGRF) katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es salaam. Tarehe 05 Septemba 2023.


MADA ZILIZOJADILIWA SAMBAMBA NA UZINDUZI WA AGRF 2023 KATIKA UKUMBI WA JULIUS NYERERE, DAR ES SALAAM, TAREHE 5 SEPTEMBA 2023

 

Mambo ni mazuri, mkutano umeitikiwa na watu zaidi ya 3000 kutoka nchi mbalimbali. Wameitikia kuja kuzungumzia usalama wa uhai wetu. Mada ni nyingi zinajadiliwa. Washiriki si Waafrika tu, watu kutoka mabara mengine nao wapo. Mpenzi msomaji fatana nami upate dondoo za kongamano hilo.

 

Mada ya 1 ni kuhusu Sekta za Mifugo na Uvuvi kwa kifupi.: Muelekeo na Vipaumbele.

 

Mada hii iliunganisha wadau wakubwa kwenye sekta. Ilijadili sekta kwa ujumla na kuainisha muelekeo na vipaumbele.

 

Wazungumzaji walikuwa ni kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, SAGCOT na Heifer International.

 

Mada ya 2 ni Good Morning AGRF.

 

Mada hii ni ya kila siku asubuhi wakati wa kuanza vikao. Huonesha kwa kifupi yaliyojiri siku iliyotangulia na yatakayojiri siku hiyo.

 

Waandaaji walikuwa ni Ms. Jolenta Joseph wa Tanzania, Bwana John Agboola kutoka Nigeria na Ms. Wangari Kuria kutoka Kenya.

 

Mzungumzaji alikuwa ni kutoka Africa Food Systems Forum (AGRF)

 

Uzinduzi wa Kilele cha Mkutano

 

Mada ya 3 ilihusu Recover, Regenerate, Act: Africa’s Solutions to Food Systems Transformation.

 

Mada hii ilijadiliwa kwa umakini mkubwa kulingana na  wazungumzaji wake walivyo jiandaa. Lengo la mada ni kuweka msingi wa AGRF 2023, kuunganisha wadau mbalimbali wenye malengo na uzoefu tofauti. Katika kikao cha kujadili mada, uzinduzi wa Africa Agricultural Report ulifanyika.

Mada ndogo ndogo zilizojadiliwa ni The Africa Agriculture Status Report na The Food Systems Stocktaking: Critical parameters for Food Systems transformation.

 

Wazungumzaji walikuwa ni pamoja na Mhe. Philip Isdor Mpango (Makamu wa Rais, Tanzania), Mhe. Abdallah Ulega (Waziri wa Mifugo na Uvuvi-Tanzania), World Business Council for Sustainable Development, Eastern on Development (IGAD), Ofisi ya Rais wa Niger.

 

Mada ya 4 ilihusu Uzinduzi Wa Jukwaa Dogo la Kujadili Suala Mahsusi la Ufadhili wa Kilimo

 

Wadau wakuu kuhusu upatikanji wa fedha na jamii ya wafanya biashara walikutana na kubadilishana mawazo kuhusu uwekezaji katika kilimo.

 

Wazungumzaji walikuwa ni Mhe. Dr. Ashatu Kijaji (Naibu Waziri wa Fedha Tanzania), IFC, Janngo Capital & led Financial Business Award Winner CEO Forum 2023, Pearl Capital Partners Ltd, MyGrowthFund Venture Partners, Benki Kuu Tanzania, mwakilishi kutoka Serikali ya Kenya, IFAD, Rwanda Development Board, AFEX na USAID.

 

Mada ya 5 ilihusu Sera: Nguvu za Takwimu, Taarifa na Tafiti kwa ajili ya Mifumo Endelevu ya Usalama wa Chakula.

 

Mada hii ililenga kujadili kuhusu Nguvu za Takwimu, Taarifa na Tafiti na changamoto zake kwa ajili ya Mifumo Endelevu ya Usalama wa Chakula, na namna bora ya kuboresha mifumo mbalimbali ikijumisha watoa maamuzi na wadau wengine.

 

Wazungumzaji walikuwa ni pamoja na Waziri wa Kilimo Uganda (Mhe. Frank Tumwebaze), na kutoka McKinsey & Company, Jounalist and Entrepreneur Haiti, 2020 Pitch Agrihack Winner, FarmLifeline Technologies, House of Harvest, Country Manager Kenya OCP, Zambia Apollo Agriculture, Microsoft Tech for Social Impact, Civil Society, SDG Advocate, AU (East Africa Director), WWF, Association for the Promotion of African Studies, FARA, Regions and Partnership (CGIAR), African Agricultural Technology Foundation (AATF), United Arab Emirates na International Centre for Innovation and Transfer of Agriculture, Livestock and Environmental Technology.

 

Mada ya 6 ilihusu Bunge na Jukwa la Watunga Sera: Kuwezesha Biashara Kufanyika Katika Mazingira Rafiki.

 

Mada hii ililenga kujadili masuala yanayozunguka mazingira rafiki katika mifumo ya uzalishaji wa chakula. Aidha, ililenga kujadili sera, sheria na kanuni ambazo zinavutia wakulima wadogo na wa kati kuwekeza katika kilimo. Changamoto mbalimbali pia zilijadiliwa.

 

Wazungumzaji walikuwa ni Spika wa Bunge la Tanzania (Mhe. Tulia Ackson), Waziri wa Chakula na Kilimo Ghana (Mhe. Bryan Acheampong), Waziri wa Uwekezaji Togo (Mhe. Rose Kayi Mivedor), Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini China (Mhe. Renjian Tang), Mhe. Hisham Al-Husari, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo na Umwagiliaji Misri, Kamati ya Bunge ya Kilimo, Ardhi na Maendeleo Vijijini Afrika ya Kusini, International Development Research Centre (IDRC), na kutoka Equity Bank, Rural Economy and Agriculture, Pan-African Parliament (PAP) na Young Professionals for Agricultural Development.

 

Mada ya 7 ilihusu Mashindano ya Vijana Kuonesha Ubunifu wa Wajasiriamali katika Biashara za Kilimo Barani Afrika.

 

Katika mada hii, viongozi wa vijana kutoka sehemu mbalimbali walionesha mifano ya ubunifu wao na mawazo yao katika ujasiriamali kwenye biashara ya kilimo. Kulikuwa na waamuzi waliosikiliza vijana hao ili kuamua washindi. Lengo lilikuwa ni kupata ufumbuzi wa mifumo bora ya kilimo na kuhamasisha vijana kuwekeza katika kilimo.

 

Wazungumzaji walikuwa ni kutoka Sahel Consulting, Yara International, Youth Ambassador, Generation Africa (Ms. Ada Osakwe), Syngenta Foundation, Heifer International na General Counsel of Agricultral Development Morocco.

 

Mada ya 8 ilihusu Maono ya Afrika kuhusu Mbolea na Afya ya Udongo.

 

Mada hii ilijadili maendeleo ya kilimo katika bara la Afrika kwa kuzingatia kuwa kidunia hali ni tete kutokana na masuala mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vita kati ya Urusi na Ukraine. Vita inayoendelea inazuia upatikanaji wa mbolea ya kilimo, hivyo ni fursa ya Afrika kutafakari upya hali ilivyo ili kujenga viwanda vya mbolea barani Afrika.

 

Lengo la mada lilikuwa ni kuchambua kwa kina umuhimu wa mbolea na kubaini mikakati inayoweza kuwezesha upatikanaji wa mbolea bora.

 

Wazungumzaji walikuwa ni Waziri wa Uchumi na Fedha Msumbiji (Mhe. Ernesto Max Elias Tonela), Waziri wa Kilimo na Mifugo Rwanda (Mhe. Dr. Ildephonse Musafiri), Waziri wa Kilimo na Mifugo Burkina Faso (Mhe. Dr. Ismael Sombie), Waziri wa Kilimo na Mifugo Brazil (Mhe. Carlos Henrique Baqueto Favaro). Wengine ni kutoka Bill and Melinda Gates Foundation, OCP Morocco, Yara International, International Fertiliser Development Centre, Economic Community of West African States (ECOWAS), Jumuiya ya Afrika Mashariki (Dr. Peter Mutuku), Wizara ya Ushirikiano wa Kichumi na Maendeleo ya Ujerumani (Dirk Meyer), na Agricultural Livelihoods-IKEA Foundation.

 

 

Mada ya 9 ni kuhusu Improving BDS Delivery to African Agri-SMEs.

 

Waandaaji ni SAFIN na AMEA.

 

Lengo la mada ni kushirikishana matokeo ya utafiti kuhusu tija katika uendelezaji wa biashara katika Afrika Mashariki. Lengo mahsusi ni kubaini ufumbuzi mbalimbali kwa ajili ya kuendeleza utafiti uliofanyika na kuonesha hatua za kuchukuwa katika utekelezaji.

 

Wazungumzaji walikuwa ni SAFIN, AMEA, Pearl Capital Partners ya Uganda na Food Systems Summit (IFAD).

 

 

Mada ya 10 ni kuhusu Ubunifu na Teknolojia.

 

Lengo la mada ni kuainisha maeneo ambayo ujasiriamali wa kilimo unaweza kufanyika barani Afrika kwa kutumia ubunifu na teknolojia kuongeza uzalishaji, uendelevu na ushindani katika kilimo.

 

Wazungumzaji walikuwa ni kutoka Vodacom, Syngeta, Angola Cables ya Angola na Robocare ya Tunisia.

 

Mada ya 11 ni kuhusu Upatikanaji wa Fedha

 

Lengo la mada lilikuwa ni kubainisha ubunifu katika upatikanaji wa fedha. Mijadala ilijikita katika kuchambua maeneo mbalimbali ya kuweza kupata fedha kwa kuzingatia aina ya wajasiriamali wa kilimo katika bara la Afrika. Lengo la mjadalapia ni kuangalia namna ya kusaidia vijana katika kilimo.

 

Wazungumzaji walikuwa ni kutoka ORABANK Group, NMB Tanzania, Zima Health Group ya Rwanda, Smiley’z Kitchen ya Nigeria, Lillies Innovations ya Malawi na Grow for Me ya Ghana.

 

Mada ya 12 ilikuwa ya Majadiliano Mepesi ya Watu Binafsi Kufahamiana kwa Karibu.

 

Mada hii ilikuwa ya watu binafsi kufahamiana kwa karibu (social networking) pamoja na kuburudika kwa vinywaji laini na mziki mwororo kumalizia siku.

 

Taarifa hii imetokana na ratiba ya AGRF kwa sehemu kubwa.

 

Imeandaliwa na Nyabaganga Taraba.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com