MADA ZA AGRF 2023 ZILIZOJADILIWA SEPTEMBA 7



 MADA ZA AGRF 2023 ZILIZOJADILIWA KATIKA KUMBI MBALIMBALI ZA JULIUS NYERERE, DAR ES SALAAM, TAREHE 7 SEPTEMBA 2023

 

Imeandaliwa na Nyabanga Daudi Taraba

Mpenzi msomaji kwa siku ya leo kongamano hali joto linazidi kupanda, utulivu na shauku ya washiriki wa mkutano vinaonekana waziwazi, wakipishana kila mmoja akisaka tukio linalomhusu.

Mada tofauti ziliendelea kujadiliwa katika kumbi mbalimbali zilizopo kwenye maeneo ya ukumbi mkubwa wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

Mada ya 1 ni Good Morning AGRF.

 

Mada hii ni ya kila siku asubuhi wakati wa kuanza vikao. Huonesha kwa kifupi yaliyojiri siku iliyotangulia na yatakayojiri siku hiyo.

 

Waandaaji walikuwa ni Ms. Jolenta Joseph wa Tanzania, Bwana John Agboola kutoka Nigeria na Ms. Wangari Kuria kutoka Kenya.

 

Wazungumzaji walikuwa ni Assistant DG, Regional Representative for Africa, FAO (Dr. Abebe Haile Gabriel), VP Policy & StateCapablity AGRA (Dr. Apollos Nwafor) na Director, West Africa Centre for Crop Improvement, Africa Food Prize 2022 Winner (Prof. Eric Danguah)

 

Mada ya 2 ilihusu Hoja za Vijana kuhusu Mifumo ya Maendeleo.

Katika mada hii, Kitengo cha Wanawake wa AGRF na Generation Africa Platform, kilijadili masuala mbalimbali. Lengo ni vijana kuelezea hoja zao kwa viongozi wanasiasa, ili zizingatiwe kwenye sera za jumla za mifumo ya maendeleo.

Majadiliano ya mada yalifunguliwa kwa hotuba iliyotolewa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania.

Wazungumzaji walikuwa ni Mheshimiwa Samia suluhu Rais wa Jamhuri ya Muungano, Waziri wa Kilimo wa Tanzania (Mhe. Hussen Bashe), na wengine kutoka IFAD, Youth Envoy, AU, Swiss Agency for Development & Cooperation, Tanzania, UN Sustainable Development Solutions Network, Bolivia.

 

Mada ya 3 ni kuhusu Mageuzi Katika Mifumo ya Uzalishaji Chakula Afrika ili Kuendana na Mabadiliko ya Tabianchi.

Lengo la mada lilikuwa ni kujadili masuala mbalimbali yanayochagiza kilimo barani Afrika. Hii ni pamoja na mabadiliko ya tabianchi, teknolojia, uhimilivu, sera, tafiti na mengineyo. Changamoto pia zilibainishwa na mapendekezo kutolewa kuhusu nini kifanyike katika mifumo ya uzalishaji chakula ili kuwa salama.

 

Wazungumzaji walikuwa ni Waziri wa Kilimo na Chakula wa Burkina Faso, Waziri wa Kilimo wa Ethiopia, Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji wa Somali, Waziri wa Kilimo na Mitambo ya Maendeleo Vijijini wa Senegal.

Wengine walikuwa ni kutoka CGIAR, Bill & Melinda Gates Foundation (BMGF), Seed Systems Development, AGRA, International Maize and Wheat Improvement Center (CIMMYT), Global Development, Cornell University, Leading Light Initiative, UNEP na USAID.

 

Mada ya 4 ni kuhusu Ubunifu Katika Upatikanaji wa Fedha.

Katika mada hii, masuala mbalimbali ya kifedha yalijadiliwa. Lengo lilikuwa ni kubaini mbinu mbalimbali za kupata fedha kwa ajili ya kilimo. Hii ni pamoja na ushirikishji wa sekta binafsi kupitia ubia kati ya serikali na sekta binafsi, yaani Public-Private Partnership (PPP).

 

Wazungumzaji walikuwa ni pamoja na Waziri wa Sea, Inlands Waters and Fisheries wa Msumbiji (Lidia de Fatima da Graca Cardoso) na 2022 Africa Food Prize Winner (Dr. Birama Sidibe).

Wengine walikuwa ni kutoka Eastern and Southern Africa, World Bank, Equity Bank, Stanbic Bank Kenya, Bamboo Capital Partners, ORABANK Group, Sahel Consulting, AGRA, NMB Bank Tanzania, Qatar Fund for Development (QFFD) na OPEC Fund for International Development (OFID).

 

Mada ya 5 ni kuhusu Ununuzi Ndani ya Nchi Kuchochea Mageuzi Katika Mifumo ya Uzalishaji Chakula.

Mada hii ilihusu masuala ya ununuzi kufanyika ndani ya nchi. Lengo ni kuchochea mageuzi katika mifumo ya uzalishaji chakula, kwani upatikanaji wa fedha za ndani huongezeka, uzalishaji huongezeka, hivyo kuimarisha uchumi wa nchi na usalama wa chakula.

Wazungumzaji walikuwa ni Waziri wa Kilimo na Mifugo wa Brazil (Mhe. Carlos Henrique Baqueta Favaro), Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Uganda (Mhe. Frank Tumwebaze), Waziri wa Kilimo na Mifugo wa Kenya (Mhe. Mithuka Linturi), Waziri wa Afya wa Rwanda (Mhe. Dr. Sabin Nsanzimana).

Wengine walikuwa ni kutoka WFP, Rockefeller Foundation, WWF, Natural Resources Institute, University of Greenwich, UK, Ethiopian Agricultural Transformation Agency na Secretary General of East African Community.

 

Mada ya 6 ni kuhusu Miundombinu Katika Mageuzi ya Mifumo ya Uzalishaji Chakula

Lengo la mada lilikuwa ni kubaini aina mbalimbali ya miundombinu inayotumika katika kilimo. Aidha, mada ilijadili teknolojia zenye tija katika kilimo. Lengo mahsusi ni kupata na kushirikiana uzoefu ili kuwezesha uwepo wa kilimo endelevu.

Wazungumzaji walikuwa ni Waziri wa Ardhi, Kilimo, Maji na Makazi Vijijini wa Zimbabwe (Mhe. Anxious Masuka) na Waziri wa Kilimo wa Cameroon (Mhe. Gabriel Mbairobe).

Wengine walikuwa ni kutoka IMF, Tree Group Authority ya Ghana, UAE, Millennium Challenge Corporation, Green Deal and Digital Agenda na European Commission, Department for Sustainable Development, Ministry of Foreign Affairs, Norway.

 

Mada ya 7 ilihusu Usimamizi wa Mageuzi Katika Uzalishaji na Usalama Bora wa Chakula.

 

Mada ililenga kujadili mifumo, sera na mikakati mbalimbali inayosimamia uzalishji wa chakula. Aidha, iljadili changamoto zilizopo na kutoa mapendekezo kuhusu hatua za kuchukuwa.

Wazungumzaji walikuwa ni pamoja na Waziri wa Kilimo na Masuala ya Vijijini wa China (Mhe. Renjian Tang), Waziri wa Kilimo, Tabianchi na Mazingira wa Seychelles (Mhe. Flavien P. Joubert) na Waizri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Nigeria (Dr. Mohammad Mohamood Abubakar).

Wengine ni Assistant Director General, Regional Representative for Africa, FAO, OIC, African Capacity Building Foundation, Bill & Melinda Gates Foundation.

 

Mada ya 8 ni kuhusu Jukwaa la Wakulima.

Lengo la mada lilikuwa ni kujadili changamoto wanazopitia wakulima wadogo barani Afrika. Washiriki walijadiliana uzoefu miongoni mwa nchi zao ili kubaini maboresho ya kuwezesha kilimo endelevu chenye tija, kikizingatia usalama wa chakula.

Wazungumzaji walikuwa ni pamoja na kutoka Tanzania Horticultural Association, Green Climate Fund, German Federal Ministry of Economic Cooperation and Development, Network of West African Farmers and Agricultural Producer’s Organisations Ghana, East African Farmers Federation, Tanganyika Farmers Association na Pan-African Farmers Organisation.

 

Mada ya 9 iliitwa Mazungumzo Jumuishi ya Halmashauri ya Viongozi Wenye Busara.

Halmashauri ya viongozi wenye busara inatokana na viongozi mashuhuri wa Afrika. Lengo la mada ni viongozi wenye busara kujadili hali iliyopo, kuunga mkono juhudi zinazoondelea na kupendekeza hatua za kuchukuliwa.

Wazungumzaji walikuwa ni pamoja na Rais Mstaafu wa Kenya (Mhe. Uhuru Kenyatta), Rais Mstaafu wa Liberai (Mhe. Ellen Johnson-Sirleaf), Rais Mstafu wa Tanzania (Mhe. Dr. Jakaya Kikwete) na Mfalme wa Lesotho (Lesie III.

Wengine walikuwa ni Rais Mstaafu wa Niger (Mahamadou Issoufou), Rais Mstaafu wa Afrika ya Kusini (Mhe. Thabo Mbeki), Rais Mstaafu wa Malawi (Mhe. Joyce Hilda Banda) na Rais Mstaafu wa Nigeria (Mhe. Jonathan Goodluck).

Wengine ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia (Mhe. Hailemariam Dessalegn), Waziri Mkuu Mstaafu wa Benin (Mhe. Lionel Zinsou) na Waziri Mkuu Mstafu wa Uingereza (Mhe. Tony Blair).

 

Wengine walikuwa ni kutoka Bill & Melinda Gates Foundation, AfDB.

 

Mada ya 10 ilihusu Usalama wa Chakula na Mageuzi Katika Mifumo ya Uzalishaji Chakula.

Mada ilihusu mkutano baina ya viongozi wakuu wa nchi mbalimbali. Viongozi hao walijadili pamoja na masuala ya mifumo ya uzalishaji chakula, upatikanaji wa fedha na mindombinu.

Viongozi walioshiriki ni pamoja na Rais wa Uganda (Mhe. Yoweri Kaguta Museveni), Rais wa Kenya (Mhe. Dr. William Samoei Ruto), Rais wa Rwanda (Mhe. Paul Kagame), Rais wa Burundi (Mhe. Evariste Ndayishimiye), Rais wa Sudan ya Kusini (Mhe. Salva Kiir Mayardit), Rais wa Democratic Republic of Congo (Mhe. Felix Antoine Tshisekedi), Rais wa Afrika ya Kusini (Mhe. Cyril Ramaphosa) na Rais wa Angola (Mhe. Joao Manuel Goncalves Lourenco).

Wengine walikuwa ni Rais wa Zimbabwe (Mhe. Emmerson Mnangagwa), Rais wa Zambia (Mhe. Hakainde Hichilema), Rais wa Namibia (Mhe. Dr. Hage G. Geingob), Rais wa Malawi (Mhe. Lazarus Mcarthy Chakwera), Rais wa Msumbiji (Mhe. Filipe Nyusi), Rais wa Senegal (Mhe. Macky Sall) na Rais wa Misri (Mhe. Abdel Fattah el-Sisi).

Aidha, wengine waliohudhuria kutokana na nyadhifa zao walikuwa ni Waziri Mkuu wa Ethiopia (Mhe. Dr. Abiy Ali Ahmed), Waziri Mkuu wa Barbados (Mhe. Mia Amor Mottley) na AU (Mhe. Moussa Faki Mahamat) Viongozi hawa wakuu wanchi na serikali wengine wamewakilishwa na watu kutoka nchini mwao ama mawaziri au viogozi wengine wa serikali zao.

Taarifa hii ni kwa mjibu wa ratiba ya AGRF septemba 7, 2023 fuatilia taarifa ya hitimisho la kongamano hapo kesho sisi tutakutaarifu yatakayo jili.

 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post